Dar: Trafiki wa Tegeta kwa ndevu wanatunyanyasa

kapikita

Senior Member
Jun 8, 2014
131
72
Kumekuwapo na unyanyasaji mkubwa na usumbufu unaofanywa na askari pamoja na mgambo eneo la Tegeta kwa ndevu barabara ya bagamoyo.

Askari hawa huvamia bodaboda kwa nguvu na kuchomoa funguo ukiwa katikati ya barabara suala linaloweza sababisha ajali.

Wakishakukamata kipaumbele chao cha kwanza ili wakuachie au wasikuandikie faini inabidi utoe tsh efu 10, ndio Wanakuachia

Kiongozi wao mashuhuri wa kuchukua rushwa anaitwa afande KICHUYA, huyu hana dogo akikukamata toa buku teni yako anakuachia.

Hii imekua kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hii
 
Jeshi la polisi limeoza, harufu imeshatoka hadi imeisha. Kuanzia juu hadi chini wote ni wala rushwa
 
Ndio kamba zao zinaruhusu hivo mkuu.(joke)

Kiukweli askari ni tatizo na wanakula hela hadharani bila kificho juzi nilikuwa kituo fulani cha polisi kusaka vehicle inspection nikakuta jamaa kashakusanya hamsini elfu mida ya asubuhi tu saa nne anahesabu.
 
hivi haya majina yamitaa ya ajabu ajabu watu wa dar mnayatoaga wapi!?, et tegeta kwa ndevu.
 
Kumekuwapo na unyanyasaji mkubwa na usumbufu unaofanywa na askari pamoja na mgambo eneo la Tegeta kwa ndevu barabara ya bagamoyo.

Askari hawa huvamia bodaboda kwa nguvu na kuchomoa funguo ukiwa katikati ya barabara suala linaloweza sababisha ajali.

Wakishakukamata kipaumbele chao cha kwanza ili wakuachie au wasikuandikie faini inabidi utoe tsh efu 10, ndio Wanakuachia

Kiongozi wao mashuhuri wa kuchukua rushwa anaitwa afande KICHUYA, huyu hana dogo akikukamata toa buku teni yako anakuachia.

Hii imekua kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hii
Kumbe pale tegeta kwa moto eh

Wale wa Tazara wanaudhi hao
 
' Wanakula Kuendana na Urefu Kamba hao '
We Fikiria tu STJ Prado Imekatiza hapo hana Hakika nani Yupo ndani Ya Prado, Wazo La Kukamata Prado hilo Linatoka Wapi?
 
Hadi huko mtwara tumepata taarifa zao, wanavaa kiraia alafu wanakaa karibu na maduka/biashara za watu kuvizia bodaboda hali ambayo inapelekea wateja hawafiki kuwaogopa wao. Wenye nguvu walipazie sauti hili suala...
 
Back
Top Bottom