Dar: TPA yazuia Makontena 262 yenye Mchanga wa Madini MOFED Kurasini

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
Makontena mengine zaidi ya 200 yenye mchanga kutoka migodini yameshikwa bandarini yakiwa katika yard ya iliyokuwa ZAMCARGO

BSDuDWAgf4X.jpg

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS.

Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutembelea bandari ya Dar es salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa madini kutoka migodi mbalimbali iliyopo Kanda ya Ziwa.

Mhe. Rais Magufuli alifika bandarini siku hiyo kukagua utekelezaji wa agizo lake la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini kutoka migodini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema makontena hayo yaliyokuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kiforodha yamebainika leo tarehe 25 Machi, 2017 katika msako mkali unaoendeshwa na Mamlaka yake.

Mhandisi Kakoko amesema makontena yote hayo yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), na yalikuwa yanashughulikiwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya Freight Forwarders Tanzania Limited iliyopo Dar es salaam.

Mhandisi Kakoko amesema jumla ya makontena 256 yalikuwa katika bandari kavu ya MOFED, wakati makontena mengine sita yalikuwa tayari yameshaingizwa bandarini tayari kwa kusafirishwa.

Ametoa wito kwa makampuni yote ya madini yenye shehena za mchanga yajitokeze yenyewe na kuonesha mizigo yao popote ilipo nchini kabla haijabainika katika msako kabambe unaondeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Orodha ya makontena hayo yaliyobainika inaonesha yalifika bandarini hapo katika nyakati tofauti kutoka migodi ya Buzwagi na Pange Mines.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Bw. Ramadhani Mungi amesema bandari zote nchini ziko salama na kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kuwekwa askari na vifaa vya kisasa vya ulinzi zikiwemo kamera.

1.PNG
2.PNG
3.PNG
4.PNG
 
JPM hakuwepo?, au hakuna tukio lingine lililotokea nchini?

Sasa hayo Makontena yamekamatwa kivipi?, kama yametoka Kahama mpaka Bandarini na yanajulikana yana mchanga wa dhahabu wameyakamata kivipi?

Usahihi ni kuwa hayo Makontena YAMEZUILIWA kusafirishwa kwenda nje
 
View attachment 486812

Makontena mengine zaidi ya 200 yenye mchanga kutoka migodini yameshikwa bandarini yakiwa katika yard ya iliyokuwa ZAMCARGO

Mngemkamata pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Christian Makonda kwa haraka hivyo kama mlivyofanya kwa hayo Makontena Watanzania tungewashukuruni mno kwani yawezekana Vitendo viovu alivyovifanya Makonda vikawa na madhara maradufu ya hayo Makontena yenu Feki ambayo mmecheza tu mchezo ili kutuzuga Watanzania ili kusudi mbadilishe upepo wa fikra za Watanzania wengi ambao bado umelalia kwa Bashite, Vyeti feki na uvamizi wake Clouds.
 
Hapa kuna haja ya kufikiri kwa herufi kubwa. Mfano kama amri ya kuzuia usafirishaji ilitoka tu jukwaani bila kushauriana na wasafirishaji, inakuwaje kwa yale ambayo yalikuwa njiani tayari!? Kwamba yangerudishwa Buzwagi au Geita au truck linayafikisha lilipoelekezwa kuyafikisha.
Sasa kama kabla ya hapo huu mchakato haukuwa HARAMU mpaka lile tangazo la jukwaani lilivyotoka ni kwa nini ukiyakuta sehemu unayatangazia 'uharamu'!? Same applies to Viroba!
 
Full drama... Huko migodini hakuna watu wa serikali kuangalia uchimbaji unavyoendeshwa?? Je waziri wa nishati kwanini hatimuliwi kazini ??
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wataalamu wa marine laws na international laws hebu tuambieni mzigo ulioko melini unaweza shushwa kama abiria wa daladala?

Je niwakati gani FOB inafanyakazi? Au tu basi tunataka kukomoa watu? Hivi huko mgodini sikuna ffu tra tmaa walikuwa wapi hadi yakafika bandarini?
Ijulikane mzigo (FOB) ukishatengenezewa manufest na bill of landing na letter of credit tayari umeshakuwa wa mnunuzi sasa hapo wanaemkomalia ni mchina? Aliyenunua mzigo au acacia aliyeuza?
 
Mchanga wenyewe wa madini upo wapi?
Tutajuaje km wamejaza mchanga wa baharini au mchanga wa macho

Mkileta drama muwe mnajiandaa
 
Mmmh tuache uongo. Hayo yamekwama kutokana na tamko la Mkuu. Nilifanya kautafiti kidogo kujiridhisha kuhusu hii ishu ya mchanga au dhahabu kwenye makontena.
Kwanza inasemekana kuwa kabla hayajatoka makontena mgodini yanakuwa yamekaguliwa na taasisi husika za madini na kushirikana na TRA. Sampuli huchukuliwa na maafisa wa serikali kujiridhisha kilichomo na kupigiwa bei ya soko kwa siku ya kuyafunga na kuweka lakiri za watu wa madini na TRA. Thamani ya madini yote yaliyo kwa kontena hukokotolewa na pia mrabaha kwa kila kontena (4% of Gross Value) hukokotolewa kulingana na sheria ya madini 2010 na hulipwa mapema kabla hawajapewa Export Permit kutoka ofisi ya wizara ya madini na release oder permit kutoka TRA. Malipo hayo hufanyika mapema kabla mzigo haujatolewa kwenye migodi husika ambayo nchini ni Bulyanhulu na Buzwagi yote ya Kahama. Hivyo taarifa sahihi zipo kwa ofisi zetu za umma za Madini na TRA.

View attachment 486812

Makontena mengine zaidi ya 200 yenye mchanga kutoka migodini yameshikwa bandarini yakiwa katika yard ya iliyokuwa ZAMCARGO
 
Back
Top Bottom