Dar: RC Makalla akiwa na mfanyabiashara, amesimamisha uchimbaji kokoto machimbo ya Boko

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
1,022
1,590
Nimekuona ukiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe askari pamoja na mfanyabiashara mwenye asili ya Kiarabu.

Umezungumza na wachimbaji hao kwa lugha ya vitisho ukiwaambia waondoke eneo hilo ndani ya wiki na ukiwauliza nani anayebisha, wakanyamaza, kisha mfanyabiashara huyo alipopewa nafasi ya kuzungumza akasema eneo hilo ni lake toka mwaka 2002, kama ndivyo toka mwaka 2002 alikuwa wapi kuwekeza? Huu ni uhalifu mwingine unaanza taratibu.

Mbona mnataka kuzitaabisha familia hizi kiasi hicho?

Mmesubiri Magufuli amekufa mmeanza utekaji holela wa maeneo kwa nguvu kubwa sana.

Wizara ya Ardhi kwa sasa imeingiliwa, yajayo ni hatari kwa wananchi wa kipato cha chini.

Haya mambo yalifanyika sana awamu ya nne na sasa yanarudi awamu ya sita. Nchi yangu inaelekea wapi?

Cha kusikitisha wananchi hao wamesema kinyonge sana kwamba wataondoka kwenda kubangaiza mjini wakiwa na huzuni sana.

Rais Samia endelea kuupiga mwingi.

Mkuu wa mkoa tafadhali pata maelezo kutoka kwa wakuu wa wilaya wa zamani wa Kinondoni, Ally Hapi na hata Katibu Mkuu wa CCM, Mr Chongolo ili kujua undani wa uchimbaji kokoto na huyo aliyejimilikisha eneo Al Hoshoom.

1. Eneo hilli mara nyingi limekuwa likifungwa kwa sababu ya usalama wa wachimbaji wadogo na uharibifu wa mazingira.

2. Manispaa ya Kinondoni iliamua kipindi fulani kutaka kutumia hilo eneo kama Dampo kwa ajili ya maeneo ya wilaya ya kinondoni.

3. Eneo kwa sasa Halifai kwa uwekezaji mkubwa wa uchimbaji kokoto kwa sababu ipo karibu na makazi ya watu.

MAONI

1. Mwekezaji atafutiwe eneo jingine nje ya jiji ili aweze kufanya uchimbaji mkubwa wenye tija.

2. Wachimbaji wadogo watambuliwe wasimamiwe kulinda usalama wao na uharibifu wa mazingira .

3. Kama itaonekana shughuli za uchimbaji zisitishwe basi wote pamoja na mwekezaji waondolewe na manispaa ya kinondoni itumie eneo kwa manufaa ya wote ikiwepo kuanzisha dampo la kisasa.

4. Mkuu wa mkoa ni mwanasiasa mkongwe lugha unayotumia kwa wananchi inaharibia serikali na chama na kutengeneza mtazamo hasi kwa serikali na chama kinachojinasibu kutetea watu wake bila kuangalia vipato.

Mkuu wa mkoa asisahau jinsi nguvu kubwa iliyotumika kuweka mtazamo mzuri kwenye maamuzi dhidi ya machinga.
Matajiri hawapigi kura peke yao.

====

RC MAKALLA ASIMAMISHA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI BOKO.

- Atoa Wiki moja kwa wavamizi kuondoka na kuondoa kokoto walizochimba.

- Akemea tabia ya wananchi kuvamia maeneo ya watu kiholela.

- Tamko la mkuu wa mkoa linafuatia Amri ya mahakama kutambua Kampuni ya Al Hushiim Investment ltd ambao ndio mmiliki halali.

- Aelekeza Jeshi la Polisi kuanza doria ya kulinda eneo Hilo Na kufikia tarehe 4/6/2022 Asionekane Mwananchi yeyote ili kampuni ijenge kiwanda cha Saruji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameamuru kusimamia kwa Shughuli zote za uchimbaji wa madini kwenye eneo la mwekezaji Boko lililovamiwa na kutoa wiki moja kwa Wavamizi kuondoa mali na kokoto walizochimba Mara moja.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea eneo Hilo lenye ukubwa wa hekta 70 ambapo tayari Mahakama ilishatoa haki kwa Kiwanda Cha Al Hushiim Investment ltd ambao ndio mmiliki halali.

Aidha RC Makalla amesema eneo Hilo ni mahususi kwaajili ya Shughuli za uchimbaji wa madini ambapo amepiga marufuku eneo kutumika Kama Makazi na kuelekeza kuanza kwa mchakato wa Kiwanda Cha saruji.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza doria ya kulinda eneo Hilo kwa kushirikiana na walinzi wa kampuni hiyo ambapo amesema Magari yatakayoruhusiwa kuingia ni Yale yanayokwenda kuchukuwa mzigo pekee na sio uchimbaji.

Pamoja na hayo RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe kufika kwenye eneo baada siku Saba kuanzia leo ili kujirudhisha.
 
Nimekuona ukiongozana na mkuu wa wilaya ya kinondoni Godwin Gondwe,askari pamoja na mfanyabiashara mwenye asili ya kiarabu.
Umezungumza na wachimbaji hao kwa lugha ya vitisho ukiwaambia waondoke eneo hilo ndani ya wiki na ukiwauliza nani anayebisha ,wakanyamaza ,kisha mfanyabiashara huyo alipopewa nafasi ya kuzungumza akasema eneo hilo ni lake toka mwaka 2002,kama ndivyo toka mwaka 2002 alikuwa wapi kuwekeza?,huu ni uhalifu mwingine unaanza taratibu.

Mbona mnataka kuzitaabisha familia hizi kiasi hicho?,

Mmesubiri Magufuli amekufa mmeanza utekaji holela wa maeneo kwa nguvu kubwa sana.

Wizara ya ardhi kwa sasa imeingiliwa, yajayo ni hatari kwa wananchi wa kipato cha chini.
Haya mambo yalifanyika sana awamu ya nne na sasa yanarudi awamu ya sita.
Nchi yangu inaelekea wapi?

Cha kusikitisha wananchi hao wamesema kinyonge sana kwamba wataondoka kwenda kubangaiza mjini,wakiwa na huzuni sana.
Rais Samia endelea kuupiga mwingi.
Mzee wa msoga alishasema "ukiona nchi hii ngumu hamaa kaishi nchi rahisi kwako"
 
DAB na Lukuvi pamoja na mapungufu yao yote ila issue ya ardhi walijitahidi sana.

Nway baniani mbaya kiatu chake dawa.

Maeneo km haya watu walikua
wanakubaliana na mwenye eneo wanamlipa wanapewa ardhi yy akapambane mbele kwa mbele. Hii imefanyika sana e.g wazo, Mbweni, Mkuranga na kwingineko.

Now naona wamepindua meza.
Mawaziri wa hio wizara tangu walambe teuzi hatuwaoni site.
 
Mkuu wa mkoa tafadhali Pata maelezo kutoka kwa wakuu wa wilaya wa zamani wa Kinondoni Ally Hapi na hata katibu mkuu wa CCM Mr Chongolo ili kujua undani wa uchimbaji kokoto na huyo aliyejimilikisha eneo Al Hoshoom.

1. Eneo hilli mara nyingi limekuwa likifungwa kwa sababu ya usalama wa wachimbaji wadogo na uharibifu wa mazingira.

2. Manispaa ya Kinondoni iliamua kipindi fulani kutaka kutumia hilo eneo kama Dampo kwa ajili ya maeneo ya wilaya ya kinondoni.

3. Eneo kwa sasa Halifai kwa uwekezaji mkubwa wa uchimbaji kokoto kwa sababu ipo karibu na makazi ya watu.

MAONI
1. Mwekezaji atafutiwe eneo jingine nje ya jiji ili aweze kufanya uchimbaji mkubwa wenye tija.

2. Wachimbaji wadogo watambuliwe wasimamiwe kulinda usalama wao na uharibifu wa mazingira .

3. Kama itaonekana shughuli za uchimbaji zisitishwe basi wote pamoja na mwekezaji waondolewe na manispaa ya kinondoni itumie eneo kwa manufaa ya wote ikiwepo kuanzisha dampo la kisasa.

4. Mkuu wa mkoa ni mwanasiasa mkongwe lugha unayotumia kwa wananchi inaharibia serikali na chama na kutengeneza mtazamo hasi kwa serikali na chama kinachojinasibu kutetea watu wake bila kuangalia vipato.

Mkuu wa mkoa asisahau jinsi nguvu kubwa iliyotumika kuweka mtazamo mzuri kwenye maamuzi dhidi ya machinga.
Matajiri hawapigi kura peke yao.
 
Nimekuona ukiongozana na mkuu wa wilaya ya kinondoni Godwin Gondwe,askari pamoja na mfanyabiashara mwenye asili ya kiarabu.
Umezungumza na wachimbaji hao kwa lugha ya vitisho ukiwaambia waondoke eneo hilo ndani ya wiki na ukiwauliza nani anayebisha ,wakanyamaza ,kisha mfanyabiashara huyo alipopewa nafasi ya kuzungumza akasema eneo hilo ni lake toka mwaka 2002,kama ndivyo toka mwaka 2002 alikuwa wapi kuwekeza?,huu ni uhalifu mwingine unaanza taratibu.

Mbona mnataka kuzitaabisha familia hizi kiasi hicho?,

Mmesubiri Magufuli amekufa mmeanza utekaji holela wa maeneo kwa nguvu kubwa sana.

Wizara ya ardhi kwa sasa imeingiliwa, yajayo ni hatari kwa wananchi wa kipato cha chini.
Haya mambo yalifanyika sana awamu ya nne na sasa yanarudi awamu ya sita.
Nchi yangu inaelekea wapi?

Cha kusikitisha wananchi hao wamesema kinyonge sana kwamba wataondoka kwenda kubangaiza mjini,wakiwa na huzuni sana.
Rais Samia endelea kuupiga mwingi.
CCM IPO CHINI YA WAARABU NA WAINDI WANAOJIDAI UTANZANIA ,hivyo wanasomba watakavyo pesa zetu na mali
 
Yaani bado nafuatilia na kujifunza mengi sana nchi hii dhidi ya viongozi wanaopigiwa makofi pindi wakichukua nchi.

Haya leo wengine wanalia wengine wanacheka huku wimbo ukiwa ni ule ule 'anaupiga mwingi' sijui mwingi gani huo.
 
Back
Top Bottom