DAR: Polisi walizuia Kongamano la chama cha ACT Wazalendo, Millenium Tower

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,019
4,693
Zina sema hivi.

POLISI WAMEZUIA KONGAMANO LA CHAMA LA KUCHAMBUA BAJETI

Tunasikitika kuwataarifu Wananchi Na Umma Kwa Ujumla kuwa Polisi katika Mkoa wa Dar es Salaam wametuzuia kufanya Kongamano letu lililolenga kuchambua Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2016/2017. Polisi wamezingira eneo la ukumbi wa Kongamano (LAPF Millenium Towers) tangu saa 12.00 asubuhi.

Viongozi Wakuu wa chama wanakutana na waandishi wa Habari wa Makao Makuu ya Chama Kijitonyama kuanzia saa 7.30 Mchana kwa taarifa zaidi.

Abdallah Khamis
Afisa Habari Mkuu
Chama cha ACT-Wazalendo.
 
Safi sana.Wacha aendelee kujichongea kwa Wananchi.Anadhani anajiimarisha kumbe anajibomoa.Anadhani anabomoa upinzani kisiasa kumbe anajimaliza Kisiasa


Na tutamuandama kwa njia zote za kiharakati,Kisiasa na Kisheria.Atajuta

Halafu Jeshi la Polisi na Utawala huu wanavunja Katiba.Hatuwezi kuruhusu hili

Hawataki Madudu yao kwenye bajeti Yaanikwe

Wanataka kupandikiza Hofu.
 
image.jpeg
 
Back
Top Bottom