Dar: Polisi wakusanya tsh 304 milioni kwa siku tatu, Sirro adai mapato kushuka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Polisi mkoa wa Dar es Salaam wamekusanya milioni 304 kama faini za barabarani kutoka tarehe 22/5 hadi 25/5. Kamanda Sirro amesema mapato yameshuka sababu ya mvua na watu wanaacha magari nyumbani.

Labda watu wameanza kufuata sheria barabarani hivyo kupunguza ajali na kuongeza usalama kwa watumia barabara. Mapato ya faini inabidi yashuke na usalama barabarani uongezeke. Sio sifa kutumia makosa barabarani kama chanzo kikuu cha mapato inamaana usalama upo at stake.
 
Kumbe ni kwa ajili ya mvua!

Kwahiyo anakiri jeshi lake halina uwezo wa kutoa elimu ya usalama barabarani na inapotokea kupungua kwa makosa hayo basi kuna external force inayosababisha na sio elimu!

Hii nchi hapa tulipofikia usije kushangaa kusikia akina Sirro nao wana target yao ya makusanyo kwa mwezi!!

Sasa badala ya kuwa na target ya kutoa elimu ya usalama barabarani, lengo linabadilika na kuwa elimu ya kutafuta makosa barabarani!
 
naona mpaka aibu, kumbe ndio umekuwa mradi wa kuchangia pato la Taifa. nilitegemea atasema tunashukuru watu wamekuwa wanatii sheria za barabarani na target tuje kukusanya zero kuonesha uelewa wa watu kuhusu sheria. poor Tanzania
 
Watu wameonewa hapo kabla mpaka sasa nadhani wameamua kuji equip na wakamataji wanaona hadi aibu!
 
Kumbe ni kwa ajili ya mvua!

Kwahiyo anakiri jeshi lake halina uwezo wa kutoa elimu ya usalama barabarani na inapotokea kupungua kwa makosa hayo basi kuna external force inayosababisha na sio elimu!

Hii nchi hapa tulipofikia usije kushangaa kusikia akina Sirro nao wana target yao ya makusanyo kwa mwezi!!

Sasa badala ya kuwa na target ya kutoa elimu ya usalama barabarani, lengo linabadilika na kuwa elimu ya kutafuta makosa barabarani!
Inatisha kwa kweli...
Eti kisa mvua. Khaaaaaa
 
Back
Top Bottom