Dar ni sehemu salama?Maeneo yanayofaa na yasiyofaa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,906
Wengi wanalalamika na kuandika posts za kuukandia jiji la Dar es Sallam mengi yanayosemwa na ndo maana niliwahi kusema Dar tupo kimaisha tu

Lakini ukiachana na yote dar kuna kila kitu unachotaka!!

Ukitaka maeneo yenye utulivu kama upo mkoani yapo ni mengi tu....Wadau watayataja

Ukitaka maeneo yenye ubaridi sana kama vile upo milimani au maeneo yasiyo na joto kabisa yapo ni ya kutosha tena mwaka nzima huwashi feni wala AC......Wadau watayataja

Ukitaka maeneo yenye uswahili na fujo fujo....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo yenye mzunguko mkubwa wa hela na biashara zinaenda Wadau watayataja

Ukitaka maeneo mazuri yenye miundombinu muhimu yote huko hakunaga shida za maji wala umeme wala foleni....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo yenye watu wa kipato cha chini, kujenga ni rahisi kila kitu kipo chini yapo....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo yenye kipato cha kati yaani sio maskini sana wala sio matajiri sana yapo pia.....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo wanayokaa watu wazito tu ushuani huko ni matajiri tu na wenye pesa zao....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo ya kujenga na unataka kulima yapo nje ya mji huko....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo ambayo unaweza kupata viwanja kwa dar ila bei yake ni ghali yapo bado....Wadau watayataja


Ukitaka maeneo ambapo ni uchumi wa kati viwanja vya bei ya kawaida, pametulia kiasi, ni pakuishi tu na hakuna mzunguko wa pesa pia yapo....Wadau watayataja
 
 
Back
Top Bottom