Hatimaye nimetinga makwetu Ngara Kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Safari yangu Toka Dar Kwa basi kama ilivyo Kwa miaka mingine hadi makwetu haikupungukiwa vimbembe, vibweka, udhalimu, manyanyaso, adha, na yote ya aina hiyo tokea kwa hawa mabwana: polisi ambao haijulikani kwa uhakika haki ya dhalili za namna hii wanazitoa wapi. Kiasi inasikitisha kuwa tunaishi katika nchi ya namna gani. Kwa uhakika kwingine polisi ni kimbilio makwetu polisi ni janga.
Nimeshuhudia polisi wakiendeleza utumaji wa picha kwenda kwenye simu na kuzifanyia kazi ya wanazoita tochi za spidi kinyume cha maelekezo ya Wizara.
Hii imeendelea kuleta malumbano na kero kubwa njiani. Hili la hizo picha batili ni janga kubwa hasa katika wilaya za Manyoni Singida na Ushirombo mkoani Geita. Hii ni pamoja na kuwa ipo katika record kuwa utaratibu wa matumizi ya simu binafsi kwenye hili la tochi ulipigwa marufuku.
Kuna ulazimishaji mabasi kuiangia stendi za wilayani hata kama gari husika halipakii wala kushusha abiria humo. Hii pia ipo katika record kuwa ilishapigwa marufuku.
Nimeona polisi waking'oa namba za mabasi wilayani kahama 'jana' katika Hali ya dhalili kubwa isiyo na sababu.
Hivi kweli kama nia ni kuzuia gari husika isisafiri kwanini nguvu kubwa hivyo hata kusababisha uharibifu mwingine kwenye gari la watu? Utadhani Wana ugomvi na gari. Hakuna utaratibu mwingine kweli? Hivi hakuna documents ambazo zikichukuliwa gari husika itasimama?
Polisi anapata wapi haki ya kumdhalilisha mtu, mtuhumiwa au dereva kwa chochote ambacho anadhani kuwa kakosea?
Hivi polisi hawa wanaweza kujivunia weledi upi wa mfano walio nao wao wawapo barabarani dhidi ya raia wengine? Juzi juzi msafara wa mkuu wao umeua mtoto asiyekuwa na hatia barabarani.
Hii tabia polisi ya kuvizia barabarani ili kudhalilisha wengine, ilikuwa muhimu ikafanyiwa kazi. Ana dhalilishwa mtu katika Tv Kwa kosa la kuviziwa pasi na kujali heshima yake wala staha yake katika jamii. Huu ni unyanyasaji usio mithilika.
Hakika hii ni katika Tanzania ya kijima tu. Dhalili za namna hii zaweza shabikiwa Tanzania tu, tena haiyumkiniki na ile class ya wale ambao TWAWEZA iliwabaini kuwa ndiyo mabingwa wa shabiki hizo zisizokuwa tija wala mashiko.
Marafiki yote tuyaonayo leo ni maendeleo wa kuachia haya yanayodhaniwa kuwa yanawahusu wale na kuwa site wengine hayatuhusu.