Ukisoma Gazeti la Mwananchi na baadhi ya magazeti yamelipoti athari inayoletwa na serikali ya magufuli Kubana matumizi, ukiangalia karibu walalamikaji wote wa mashirika ya ndege, mahoteli, etc ni wakazi wa Dar es Salaam, Mwandishi alitakiwa aende mbali zaidi kuona kwa kiasi gani hizo athari zimeikumba tanzania nzima. Cost-benefit analysis ni muhimu. Mi naamini Kubana matumizi kunafaidisha watanzania wengi zaidi na si wakazi wa Dar es Salaam pekee. Uandishi wa aina hii una mapungufu makubwa na uliokosa weledi. Tuache kuona dar es salaam pekee ndio inastahili kila kitu. Tanzania ni kubwa na watanzania ni wengi.