Dar: Mahakama yaruhusu Rugemalira kuleta hoja za kutaka aachiwe huru

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Ruge.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imekubali kupokea hoja za maombi ya mfanyabiashara James Rugemalira anayetaka kuondolewa kwenye kesi ya utakatishaji fedha wa Sh. Bil 309.4.

Hatua hiyo inakuja wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa utetezi, John Chuma amedai kuwa mteja wake ameshawasilisha hoja za pingamizi la awali lakini hajapata majibu yoyote kutoka upande wa Jamuhuri.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai baadhi ya nyaraka amezipata leo mahakamani hapo na kuwa upande wa Jamhuri upo tayari kusikiliza hoja hizo kwa njia ya mdomo kama nyaraka hizo zimeshaingizwa kwenye kumbukumbu ya mahakama hata kwa wakati huo kama ratiba ingeruhusu.

Wankyo amedai mshtakiwa wa pili amekua anajiwasilisha mwenyewe huku akiwa na uwakilishi wa mawakili hivyo anapaswa kusema kama amewaacha ama wanaendelea.

Akijibu suala hilo, Rugemarila amedai kuwa amekua na wawakilishi hata zaidi ya thelasini lakini kuna hoja lazima aziwasilishe mwenyewe na kuwa hilo jambo walitakiwa kulalamika mawakili wake na sio yeye kwani sheria inamruhusu kujiwakilisha.

Baada ya hoja hizo, Hakimu Shaidi Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Machi 12, 2020 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa na upande wa jamuhuri kuwasilisha majibu.

Mbali na Rugemalira, washitakiwa wengine ni Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power (IPTL) na Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege.

Zaidi soma: Dar: Mahakama yaruhusu Rugemarila kuleta hoja za kutaka aachiwe huru
 
Leo magazeti yote yameandika habari dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Rugemialira na wenzake, ukifuatilia kwa mbali na kwa jicho la tatu ninaanza kuona dalili za huyu mzee kushinda hii kesi na niwatahadharishe serikali RUGEMALIRA SIO KABENDERA, yaani Mahakama ikimfutia shitaka la uhujumu uchumi walah nawaambia huyo mzee ataishtaki serikali na ataishinda.

Stay turned!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
leo magazeti yote yameandika habar dhidi ya Kesi ya uhujumu Uchumi inayomkabili Rugemialira na wenzake,ukifatilia kwa mbali na kwa jicho la tatu ninaanza kuona dalili za huyu mzee kushinda hii kesi na niwataazalishe serikali RUGEMALIRA SIO KABENDERA, YANI Mahakama ikimfutia shitaka la uhujumu uchumi walah nawambia huyo mzee ataishitaki serikali na ataishinda

stay turned!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yule mzee ni mtu smart anajua anachofanya, wao wenyewe wanahanya maana mzee anaweza kumwaga ugali na mboga akapasua na sahani.

Najua majadiliano makubwa yanaendelea ndani ya wale watu kuona namna gani watamtoa mzee Ruge as soon as possible washaona haogopi kumwaga ukweli hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kuwa walishasema kuwa ile fedha hazikuwa za mali ya umma
Leo magazeti yote yameandika habari dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Rugemialira na wenzake, ukifuatilia kwa mbali na kwa jicho la tatu ninaanza kuona dalili za huyu mzee kushinda hii kesi na niwatahadharishe serikali RUGEMALIRA SIO KABENDERA, yaani Mahakama ikimfutia shitaka la uhujumu uchumi walah nawaambia huyo mzee ataishtaki serikali na ataishinda.

Stay turned!.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Sipati picha serikali inayo jitapa kuwa ni wasafi watakavyo umbuliwa
Yule mzee ni mtu smart anajua anachofanya, wao wenyewe wanahanya maana mzee anaweza kumwaga ugali na mboga akapasua na sahani.

Najua majadiliano makubwa yanaendelea ndani ya wale watu kuona namna gani watamtoa mzee Ruge as soon as possible washaona haogopi kumwaga ukweli hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Yaani kweli maana serikali wao walitegemea labda jamaa anaachia mzigo mambo yaishe ila ruge yeye kumbe alishagawa mzigo wote kwa ndugu jamaa na watoto yaani hana acount yeye hela yoyote na alisema bora akae huko jela kuliko kujishusha kwa mtu maana anadai hana hatia yoyote

Kumbu kumbu nilo nayo Ni kuwa lile eneo la mitambo ya ipeteli pale kudushi Ni lake,Sasa kwenye kesi kwa Nini kajumuishwa hapo ndo Kuna maswali,na sirikali kusema hiyo pesa syo mali ya sirikali Ni ushahidi tosha kuwa Kuna madudu na wajamaa hawana kosa, sirikali ilitakiwa kuomba Kodi yake Kama haikulipwa,ila Kama Kodi ililipwa yajayo yanafurahisha.
 
Yule mzee ni mtu smart anajua anachofanya, wao wenyewe wanahanya maana mzee anaweza kumwaga ugali na mboga akapasua na sahani.

Najua majadiliano makubwa yanaendelea ndani ya wale watu kuona namna gani watamtoa mzee Ruge as soon as possible washaona haogopi kumwaga ukweli hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiondoa usmart wake pia nimwanasheria kitaaluma....ila nomwerevu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rugemalila anaonewa

Fedha za Escrow si za Serikal na hata Jakaya pamoja na CAG wamelizungumzia hilo kwa nyakati tofauti ila wasiopenda kusikia Ukweli wanatahayari

Upelelezi hautokamilika miaka yote 5 iliyobaki

Tanesco wameletewa Bili ya Umeme toka IPTL ya Umeme waliouziwa wakalipa lakin kwa kuwa IPTL wenyewe kwa wenyewe walikuwa wana ugomvi ikakubaliwa Tanesco waendelee kulipa lakin fedha hizo zikae sehemu salama mpaka Ugomvi uishe, wamemaliza ugomvi wanakuja kuchukua chao unawageuka unasema zako, kama zako ilikuaje ukaziweka kwny Escrow Account?

Awamu ya Tano iliingizwa Mkenge na Zitto Kabwe pamoja na David Kafulila.

Ukifahamu hata maana ya Escrow Accounts utajua kwanini inasemwa si fedha ya Serikal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yenyewe ilisema sio za umma
Hakuna serikali iliyowahi kusema siyo za umma. Aliyesema ni Kikwete akizungumza na wazee wa Dar. Bahati mbaya pia munaleta uzi bila kujua mashitaka yake ni yapi.
 
Yule mzee ni mtu smart anajua anachofanya, wao wenyewe wanahanya maana mzee anaweza kumwaga ugali na mboga akapasua na sahani.

Najua majadiliano makubwa yanaendelea ndani ya wale watu kuona namna gani watamtoa mzee Ruge as soon as possible washaona haogopi kumwaga ukweli hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
Sipati picha serikali inayo jitapa kuwa ni wasafi watakavyo umbuliwa

In God we Trust
Yaani kweli maana serikali wao walitegemea labda jamaa anaachia mzigo mambo yaishe ila ruge yeye kumbe alishagawa mzigo wote kwa ndugu jamaa na watoto yaani hana acount yeye hela yoyote na alisema bora akae huko jela kuliko kujishusha kwa mtu maana anadai hana hatia yoyote
Tapeli anaitwa 'Smart'. Sifa hizo zilishasikika sana kabla, sasa anataabika mahabusu pamoja na kuwa smart. Tatizo ktk thrd zilizopita, tulimshabikia hata kwa ukabila tukiamini akiiba wahaya wote tumenufaika. Ni ka-tabia kanaendelea nchini kupeana likes kiukabila. Huyu ni Tapeli. Ashinde asishinde ni tapeli na siyo 'smart'

Hata hivyo subilia uone atakavyogeukwa na sheria. Kilichoko mahakamni hata siyo ushindi ni kusikilizwa kama kesi ni uhujumu au siyo. Ikiwa siyo uhujumu, itakuwa kesi gani? watu munaleta ushabiki eti ni 'smart' Rubbish!
 
Back
Top Bottom