Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,314
Nilikuwa Dar kwa ajili ya mapumziko kwenye kipindi cha Pasaka. Ilipofika siku ya Ijumaa Kuu nilihama kutoka hotelini kwenda kwa dada kwa nia ya kuwa karibu na nyumba ya ibada.
Maeneo anayoishi ni watu wenye uwezo ki-maisha. Hapo kwa dada kuna kijana wa kazi. Siku ya Jumamosi kijana alipokea zawadi mbali mbali. Kuna zawadi ya suti, kuna viatu na mkanda, Kuna uturi. Binafsi nikampongeza kwa kujua jinsi ya kuishi na watu.
(Huenda kwa sababu ya ujana) Kijana alifunguka na kuniambia zawadi hizo zimetoka kwa mahawara zake ambao ni mabinti na kina mama wa maeneo hayo. Kwa kujigamba akanionyesha ushahidi wa mawasiliano na hao watu wake. Nikistaajabu kuona wengi wanaomsifia kwa uhodari wake huku wakiapa kuendelea kumpa kama atawatunzia siri zao (miongoni mwao kuna wake za watu).
Bado najiuliza Dar kuna nini? Hali kama hii nini chanzo chake?