Dar: Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha SADC chazinduliwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,445
SADC imezindua kituo cha Kupambana na Ugaidi jijini Dar es Salaam ili kuweza kukabiliana na ugaidi unaotamalaki barani Afrika.

Waziri wa ulinzi mama Tax amesema kituo hicho ni muhimu sana kufuatia tishio la ugaidi linaloikumba kanda yetu hasa kule Msumbiji.

=====

SADC yazindua kituo cha kupambana na ugaidi

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Sadc leo zimezindua kituo cha kukabiliana na ugaidi huku wimbi hilo la uhalifu huo likionekana kuota mizizi katika baadhi ya nchi wanachama.


Kituo hicho kilichozunduliwa jijini Dar es salaam ni sehemu ya mkakati wa jumuiya hiyo kukabiliana na tishio la matukio ya kigaidi hasa wakati ambako mataifa kama Msumbiji na Eswatini yakiendelea kuandamwa na matukio ya kigaidi.

Nchi wanachama zinaamini kuwa kituo hicho kitakuwa kiini cha kukusanya na kuchakata taarifa za kiintelijensia ambazo zitasaidia kuzibaini njia watumiazo wenye makundi ya kigaidi.

Uzinduzi huo ambao mchakato wake ulianzishwa tangu mwaka 2019 unakuja katika wakati ambapo mataifa kama Afrika Kusin na Malawi yakilazimika kuongeza idadi ya askari kwenda kukabiliana na wapiganaji wa kigaidi kaskazini mwa Msumbiji.

Mkoa wa Cabo Delgado unakumbwa na ugaid

Kulingana na Waziri wa ulinzi wa Tanzania, Stergomena Taxi, nchi wanachama zinatambua namna ugaidi unavyoendelea kuwa tishio la usalama duniani kote, hivyo kuanzishwa kwa kituo hicho kumekuja katika wakati muafaka.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusin, Candith Mashego-Dlamini amesema ni mihimu kwa nchi za kanda hii kuendelea kuimarisha ushirikiiano ili kushinda vita dhidi ya vitendo vya kigaidi, vinavyoendelea kushuhudiwa katika baadhi ya nchi wanachama wake. Nchini Msumbiji tuna vikosi vya Sadc viko huko… Jeshi la Afrika Kusini limetumwa huko, kadhalika jeshi Malawi pia ili kuisaidia Msumbiji kukabiliana na magaidi wanaangamizi watu wa msumbiji.

Afrika ni kati ya maeneo ambayo vitendo vya kigaidi vinaonekana kuendelea kuongezeka na kuzidisha wasiwasi juu ya majaliwa ya bara hili kwa siku za usoni.

Ripoti iliyotolewa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inaonyesha kuwa kati ya mwaka 2007 hadi 2016 afrika ilipoteza kiasi cha dola za Marekani bilioni 119 katika mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi, kiasi cha fedha ambazo kinaelezwa kuwa kingeweza kutumika katika shughuli nyingine za uharakishaji maendeleo.

George Njogopa/DW Dar es Salaam
 
Naona tunautafuta ugaidi kwa nguvu....wanasiasa watakuja kutuvurugia nchi kwa kupenda sifa. Kwanini hicho kituo wasingekipeleka huko huko msumbiji au Kenya
 
Jambo jema sana..nchi zetu zinahitaji amani na usalama kwaajili ya maendeleo yetu.

Mbowe sio gaidi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Department X hoyee! Afande Urio hoyee! Bila wewe Mbowe angekuwa ni gaidi, sasa wanasema si gaidi kwa vile uliwawahi wasipate maiti ya ole Sabaya wasimuue kupata ushahidi.
 
Naona tunautafuta ugaidi kwa nguvu....wanasiasa watakuja kutuvurugia nchi kwa kupenda sifa. Kwanini hicho kituo wasingekipeleka huko huko msumbiji au Kenya
Mmh! Naukumbuka Wimbo wa Lucky Dube "Crazy World" nanukuu " Leaders start the war any time they want, Some for there rights some for fun"
 
Back
Top Bottom