Dar itakavyoathirika Serikali ikihama

Dar itakavyoathirika Serikali ikihama

Kuhamia Dodoma kuna faida ya uongozi wa serikali kujiona kuwa wanalo jukumu la kuitazama nchi nzima kwa mapana yake na sio kuishia kuishi maisha ya ufahari yaliyozoeleka hapa Dar.

Tanzania inayo mikoa mingi ambayo bado haijafunguka katika suala la uwekezaji. Pia ni gharama ndogo sana kwa watu kutoka kona ya nchi kama kule Rukwa, Mtwara na Kagera, kuweza kufika Dodoma na kupata huduma za kiserikali kuliko kufunga safari ndefu ya kulitafuta jiji la Dar.

Dodoma panafikika kiurahisi zaidi kulinganisha na Dar. Halafu keki ya taifa ni lazima iwafikie wengi kwa maana ya mtawanyiko wa rasilimali unaotenda haki kwa kila anayejivunia kuitwa mtanzania.
 
1.Idadi ya watu wanaokimbilia kuja dar itapungua kwa kias fulani 2.Idadi ya ombaomba kupungua jijini dar 3. Ajali kuongezeka za magari toka dar-dodoma, 4.ahadi ya serikali ya kujenga Ubungo juction na daraja la salender huenda lisitimie ndani ya miaka mitano ya kwanza ya Magufuli 5.Mpango wa mji mpya wa kigamboni kama vile umekufa kabisa kwani nguvu nyingi itaelekezwa Dodoma 6.Dar kuwa ngome kuu ya maandamano na migomo yaani dar inaweza kuwa kitovu cha wanamabadiliko kudai mabadiliko
 
Kuhamia Dodoma kuna faida ya uongozi wa serikali kujiona kuwa wanalo jukumu la kuitazama nchi nzima kwa mapana yake na sio kuishia kuishi maisha ya ufahari yaliyozoeleka hapa Dar.

Tanzania inayo mikoa mingi ambayo bado haijafunguka katika suala la uwekezaji. Pia ni gharama ndogo sana kwa watu kutoka kona ya nchi kama kule Rukwa, Mtwara na Kagera, kuweza kufika Dodoma na kupata huduma za kiserikali uliko kufunga safari ndefu ya kulitafuta jiji la Dar.

Dodoma panafikika kiurahisi zaidi kulinganisha na Dar. Halafu keki ya taifa ni lazima iwafikie wengi kwa maana ya mtawanyiko wa rasilimali unaotenda haki kwa kila anayejivunia kuitwa mtanzania.

Seriously Cake ya Taifa inawafikia wengi kwa kukaa kati kati ya Taifa, you must be kidding right?
Karne hii ya Teknolojia nani bado anawaza Wananchi wake kutembea umbali mrefu kufuata huduma, hivi unajua kune kitu kinaitwa Egoverment, mtu akiwa Lindi anahudumiwa kama yuko Dar. Tuboreshe miundo mbinu sio kuhama
 
Afadhali na sisi tutaishi masaki. Mungu bariki safari ya Dodoma.
 
Seriously Cake ya Taifa inawafikia wengi kwa kukaa kati kati ya Taifa, you must be kidding right?
Karne hii ya Teknolojia nani bado anawaza Wananchi wake kutembea umbali mrefu kufuata huduma, hivi unajua kune kitu kinaitwa Egoverment, mtu akiwa Lindi anahudumiwa kama yuko Dar. Tuboreshe miundo mbinu sio kuhama
Nyinyi ndio wale wale tu ambao kitu kinachoitwa mazoea kinawasumbua fikra zenu. Egovernment unayoiongelea wewe bado ina safari ndefu kuliko unavyoifahamu. Huwezi kukwepa movement ya watu kuelekea yalipo makao makuu ya nchi. Usijitizame kibinafsi kwa sababu umeshazoea kula bata Dar, mtazame mtu anayeishi kwenye kona ya nchi jinsi anavyolazimika kusafiri kuja Dar. Au kama wewe ni mwenyeji wa mikoa ya mipakani, jaribu kupiga picha gharama za kwenda kwenu na kurudi. Jitahidi uondokane na mawazo ya kwamba Tanzania ni Dar na Dar ni Tanzania, jivue huo utando wa kichwani kwa faida ya kuwa mtu anayepokea mawazo chanya ambayo ni mapya, kila kukicha.
 
Asante kwa kunitoa utando kwenye ubongo, lakini naomba utafakari haya kwa kina;
1. Mahitaji ya huduma za Mtanzania wa kawaida sio lazima yapatikane Dar au Dodoma kumbuka Serikali yetu ilisha fanya Ugatuzi wa Madaraka
2. Mwananchi wa kawaida anaihitaji huduma yenye tija kwa wakati na gharama nafuu, huo umbali unao usema wewe utapungua kwenye nauli lakini ataulipa kwenye Guest House na Mama Lishe akisubiri huduma Idodomya.
3. Badala ya kuhamia Dodoma bora Serikali ingeimarisha Ofisi au Mamlaka za Kikanda ili niweze kukubali hoja yako ya umbali kuwa na mantiki.
4. Serikali makini inajali Bajeti yake ambayo imetengeneza yenyewe na kuipitisha yenyewe, hujanieleza hizi Pesa au gharama za kuhamia Dodoma zinatoka wapi, yani bora twende tu bila hata kuuliza kisa tunapenda Bata za Dar
 
Biashara:

Nyumba nyingi Masaki, Osterbay zimepangwa na watumishi waserikali pale Serikali itakapo ondoka na watumishi nyumba zitapungua kodi na masaki itapungua thamani na ulizi utapungua.

Hotel nyingi zitadorora kama zinavyodorora sasa watumishi wengi washazoea kupiga na kufanya party hotel. Sasa uko wanakoelekea hela ipo kwenye mzunguko mdogo maana hapa kazi hii sera inahitaji kuwa makini na majukumu uliyopangiwa.

Magari yatapungua sana hapa mjini na kelele za ving'ora zitapungua

Soko la wasichana;
Kwa wale wanaopenda slope kwa mtumishi anakupa lift au ela ujue imekula Kwako jipange sasa.

Karibu ndugu ulichoona kwenye uchumi wa Dar utakuaje /effect of gvt after go Dodoma Chamwino.
HAYO ULIOANDIKA NI FAIDA TUPU SI ATHARI
 
Kuhamia Dodoma kuna faida ya uongozi wa serikali kujiona kuwa wanalo jukumu la kuitazama nchi nzima kwa mapana yake na sio kuishia kuishi maisha ya ufahari yaliyozoeleka hapa Dar.

Tanzania inayo mikoa mingi ambayo bado haijafunguka katika suala la uwekezaji. Pia ni gharama ndogo sana kwa watu kutoka kona ya nchi kama kule Rukwa, Mtwara na Kagera, kuweza kufika Dodoma na kupata huduma za kiserikali kuliko kufunga safari ndefu ya kulitafuta jiji la Dar.

Dodoma panafikika kiurahisi zaidi kulinganisha na Dar. Halafu keki ya taifa ni lazima iwafikie wengi kwa maana ya mtawanyiko wa rasilimali unaotenda haki kwa kila anayejivunia kuitwa mtanzania.
Labda Rukwa kwa Dar ni Shida. Ukiwasha gari lako Dodoma, na mwenzako akawasha la Kwake Lindi, munafika muda sawa sawa. Kwani zote ni Kilometa 460 hivi. Na ukiwasha Mtwara zitaongezeka Dakika 40 tu kwa yule aliyeanzia Dodoma.

Hivyo kwa Dar-Mtwara ni karibu kuliko Dar Arusha.
 
Kwa uelewa wako unaona hamna athari ila kwa mfanya biashara wa hotel. Anaetegemea mikutano ili kuingiza income ili akulipe we mfanyakazi hujaona hapo
 
Dah.. Ila ingekuwa poa sana kama wangehamishia Moshi kwa sababu ni karibu na mlima Kilimanjaro 🙂🙂
 
Makao makuu ya China ni Beijing but still Shangai na sehemu nyingine zinatesa.

Unaongeleaje Dubai wakati makao makuu ya serikali yapo Abudhabi..

So still Dar itabaki kuwa business city na kioo cha Tz
 
Dar majungu mengi bora ahamie dom tu, yaani dar itakuwa mji mkongwe kama ujiji, dodoma tunajenga na ikulu mpya tunaachana na ile ya mkoloni,
Mnahama na majungu yenu
 
Dar walianza kuikataa ccm na kuamua kuchagua ukawa, ccm kwa visasa uta waweza wameamua kuelekea Dodoma waliko chaguliwa majimbo yote wakakae na wawapendao.
Wapiga kura za hasira haooo wanakuja kubadili upepo
 
Makao makuu ya China ni Beijing but still Shangai na sehemu nyingine zinatesa.

Unaongeleaje Dubai wakati makao makuu ya serikali yapo Abudhabi..

So still Dar itabaki kuwa business city na kioo cha Tz
Kwani kuna tatizo?
 
..Magufuli alitakiwa awe na vipaumbele vichache vyenye multiplier effect ktk uchumi wa nchi.

..kuhamia Dodoma na kujenga uwanja wa ndege Chato siyo vipaumbele sasa hivi.
Shauri yenu mnao dhani huyu ndugu ana nia thabiti ya kuiletea maendeleo Nchi hii. Nilipo ona anapanga kujenga uwanja chato nikajua tumeingia chaka kumchagua MTU huyu.
 
Back
Top Bottom