Dar Gizani thanks to Tanesco.

Nikiwafikiria hawa jamaa wa tanesco na serikali tumbo linauma! Jamani kuna yeyote mwenye aidia ya jinsi ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu kwani haya majenereta hayalipi huku kwenye vijiwe vya kuganga njaa uswahilini!
 
Wiki chache zilizopita KM- Nishati na Madini alisikika akiwaagiza mafundi wa Tanesco kufanya kazi usiku na mchana kushughulikia hitilafu ya kiufundi kwenye Transforma ya kipawa (ambayo sina hakika kama ndo inahudumia DSM yote) na kwamba ndani kipindi cha siku nane, tatizo lingekuwa limekwisha. Tangu nisikie kauli hiyo siku nane zimepita. Mgawo unaendelea na sina hakika kama KM huyo amejitokeza kutoa kauli nyingine juu ya kadhia hii. Vyovyote vile iwavyo, nadhani nishati ya umeme Tanzania bado haijapewa umuhimu unaostahili katika kuchangia maendeleo ya nchi. Pengine kama ilivyochangiwa na Sokomoko hapo juu kwamba matatizo ya nchi ni mradi wa wakubwa, kwanini tusiamini hivyo?
 

Kijana hapa bongo tunae mtaalamu wa nyukilia dr gharib bilal sema tatizo siasa ndio inaifanya nchi hii isiendelee kwenye mambo muhimu yenye kuhitaji utaalamu wao wanafanya siasa. Sijui kama tutafika kwenye tanzania yenye neema.

Pili. Mwalimu aliapewa two choices achague moja kati ya reli ( I think ya TAZARA ) na mtambo wa kufua umeme wenye uhakika yeye kwake reli ilikuwa ni muhimu kwa wakati ule, lakini baada ya hapo hakuweka mikakati imara ya kuhakikisha mbeleni Tanzania inapata umeme wenye uhakika! Mwalimu hakuwa na vision kuwa viwanda vingeongezeka na maisha ya watu yangebadilika alitaka watu wabaki wajamaa na ndio maana akawaswaga watu kwenye vijiji vya ujamaa.

PS*

Nimetoka asubuhi saa mbili na dakika tano wameukata na jana waliurudisha saa nane ya usiku!
 

Usiingize yale mambo yako yale kwenye suala la kitaifa. Dr Bilal ni kilaza tu hakuna alowahi fanya na degree yake ya Urusi. Do not count him kama ni mtu muhimu. Hana hata chapisho moja kwenye peer review journal. Hajawahi kuwa na mradi wowote akiwa anafundisha pale UD. Kwangu mimi anakaratasi za theory za nyukilia alizosomea. Hajawahi leta mchango nchini zaidi ya kufundisha. Kuna vijana wenye weledi achana na Mgonjwa Bilal awe mwanasiasa. Miaka yote UD hakuwa hata Associate Prof hahahahaah ama anasubiria kupewa bwerere.

Kuhusu uchaguzi wa Nyerere hizo ni propaganda zako za kule sehemu, kumdiscredited Mwal Nyerere. Weka source hapa tukuelewe otherwise ni kelele za muhadhara.

Masuala ya msingi sisi ni mizaha tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…