Dar: Gharama zinavyowaweka njiapanda akina Mama wanaojifungua kwa upasuaji

News Tz1

Member
Joined
Nov 28, 2025
Posts
25
Reaction score
30
Makala👇🏼

Simulizi za akina mama Waliojifungua kwa Upasuaji (Dar);

Licha ya Serikali kusisitiza kuwa wajawazito hawapaswi kutozwa gharama wakati wa kujifungua, hali ni tofauti kwa baadhi ya wanawake wanaojifungua kwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na baadhi ya hospitali nyingine za Serikali zilizopo Dar es salaam.

Msingi wa utoaji wa huduma za gharama nafuu unaelezwa katika Kifungu cha 87(1) cha Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya mwaka 2009, ambacho kinakataza utoaji wa huduma za afya kinyume na maagizo ya Serikali, ikiwemo utozaji wa gharama zisizotambuliwa na sheria pamoja na miongozo iliyowekwa na mamlaka husika.
4f7f44a6-d1f2-41d9-8c31-2d60288c5239.jpeg

Mfono wa picha katika chumba cha upasuaji

Miongoni mwa miongozo muhimu iliyotungwa ili kuratibu utoaji wa huduma rafiki kwa wajawazito na wamama wanaojifungua ni pamoja na mwongozo wa kutokutoza wajawazito gharama za huduma muhimu za uzazi (User Fees Exemption for Maternal Health Services), Mwongozo wa Kitaifa wa Huduma za Antenatal (Guideline for Antenatal Care Services), pamoja na Mwongozo wa Huduma Baada ya Kujifungua (National Postpartum Care Guidelines). Mwongozo huu unalenga kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma sahihi ndani ya wiki sita baada ya kujifungua.

Hata hivyo, uchunguzi unaibua hoja kuhusu uzingatiaji wa miongozo hiyo.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza wanasema walitozwa gharama kati ya shilingi laki tano hadi laki nane kwa huduma ya upasuaji wakati wa kujifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Nimejifungulia Muhimbili mwaka huu (2025) na nilitozwa gharama ambayo sikuwahi kuitarajia. Maana tunaambiwa kujifungua ni bure au unachangia kidogo. Lakini mimi nililipa zaidi ya shilingi laki sita baada ya kujifungua kwa upasuaji. Kupata hela hiyo haikuwa rahisi, namshukuru Mungu mume wangu ni mpambanaji, alifanya kila lililowezekana hadi nikapata fedha hizo,” anaeleza Diana Dominic (24).

Anaongeza, “Mfano kama mume wangu angekuwa amenitelekeza, ningetoa wapi hiyo pesa yote? Na kumbuka sikuwa nimejiandaa kwa gharama hizo. Huenda ningezuiwa kutoka hospitalini au ningeuza mali zangu.”

"Nilienda kukopa"
Katika mazungumzo hayo, mume wa Diana, anayejitambulisha kwa jina la Kidevu, fundi ujenzi, anasema alilazimika kukopa shilingi laki tatu ili kugharamia upasuaji wa mkewe. Hata hivyo, anatoa wito kwa Serikali kusimamia utekelezaji wa kauli zake.

“Nitoe wito kwa Serikali isimamie kauli zinazotolewa na viongozi kuhusu unafuu wa gharama kwa wajawazito wanaojifungua, au watuambiwe ukweli mapema ili tujiandae. Maana unategemea unafuu, lakini mwisho wa siku unakuta gharama ni kubwa na unaingia kwenye madeni,” anaeleza Kidevu.
9a388099-3c5f-4a94-bc8c-4be443c652ac.jpeg

sio picha halisi

"Simulizi nyingine"

Naye Binti Esta Lyimo anaeleza kuwa alipitia changamoto kama hiyo alipokuwa akijifungua kwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akilazimika kukopa fedha kupitia vikoba.

“Gharama ni kubwa sana. Sidhani kama ni nafuu kama inavyosemwa. Nilijifungulia Muhimbili miezi sita iliyopita (Machi 2025). Nakumbuka nilipopata ujauzito wangu wa kwanza, mtoto alifariki wakati wa kujifungua katika hospitali moja mkoani Mtwara. Nilishauriwa nikibeba mimba nyingine niende Muhimbili, na kweli nilifanya hivyo,” anaeleza.

Anaendelea, “Jambo la kufurahia ni kwamba nilimpata mtoto wangu akiwa hai, lakini kilichoniumiza ni gharama kubwa nilizoambiwa nilipie. Nilikuwa na bima ya NHIF, lakini haikunisaidia ipasavyo. Niliambiwa nilipie tena shilingi 547,000, huku kwenye bima wakikata takribani laki mbili. Kwa wakati huo sikuwa na pesa ya kutosha, nikalazimika kukopa kwenye kikoba, kwa makubaliano ya kulipa kidogo kidogo baadaye.”

Sanjari na simulizi hizo, akinamama wengine kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakilalamikia ukubwa wa gharama. Mnamo Agosti 2025, mmoja wa waandishi wa makala hii akiwa katika eneo la Muhimbili, aliwasikia wanawake wawili wakilalamikia ndugu zao kutozwa zaidi ya shilingi laki saba kwa huduma ya kujifungua kwa upasuaji. Alipojaribu kufuatilia, wahusika walidai kuwa malipo hayo yalifanyika kwa fedha taslimu (cash).

Simulizi za aina hii zimekuwa zikisikika mara kwa mara miongoni mwa wanawake wanaojifungulia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, huku maswali mengi yakiibuka kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Serikali na kauli za viongozi kuhusu unafuu wa gharama kwa wajawazito.

Msimamo wa Serikali na Wadau : Wanaona nini?

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali katika kipindi chake cha uongozi imekuwa ikisisitiza kusambaza vifaa na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kupunguza gharama na kupunguza vifo vya mama na watoto.

Vilevile, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Makamu Mwenyekiti wake, Stephen Wasira, kilipiga marufuku utozaji wa fedha kwa wajawazito wanaokwenda kujifungua hospitalini, akisisitiza kuwa huduma hiyo ni bure.

Alitoa kauli hiyo akiwa Mlowo, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, akieleza kuwa sera ya CCM iko wazi kuwa huduma za kujifungua na huduma kwa watoto wenye umri wa miaka 0–5 hazipaswi kutozwa gharama.

Wasira alitoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliodai kuwa wajawazito walikuwa wakitakiwa kulipa hadi shilingi 300,000 ili kupata huduma ya kujifungua, hali aliyosema inakiuka sera na maelekezo ya chama.

“Sera ya CCM iko wazi kabisa. Hairuhusiwi mama mjamzito kulipa fedha ili apate huduma ya kujifungua. Watoto ni baraka, si dhambi. Natoa maelekezo kwa viongozi wa chama ngazi ya wilaya na mkoa kufuatilia na kuchukua hatua pale taratibu hizi zinapokiukwa. Nasisitiza, huduma ya kujifungua ni bure,” alisema Wasira.

Ilani ya CCM inaelekeza nini?
999a6e41-4011-47ff-b6fa-7e553f600c6d.jpeg

Iliani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020/2025 Kipengengele cha 83 (a) ukurasa wa 136 ilieza juu ya mpango wa "Kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto na kuzitoa bila malipo ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano"
Pamoja na msisitizo huo, wadau mbalimbali wamekuwa wakisisitiza utekelezaji wa miongozo inayolenga kuleta unafuu wa gharama kwa wajawazito.

Chama cha ACT Wazalendo, kupitia ilani na mijadala yake ya mwaka 2025, kiliahidi kupinga utozaji wa gharama kwa wajawazito wanapokwenda kujifungua au kupata huduma za mama na mtoto, huku kikidai kuwa utekelezaji wa sera hizo bado una changamoto.

Mei 2025, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, kupitia aliyekuwa Naibu Waziri kwenye Wizara hiyo, Dkt. Godwin Mollel ilisisitiza kuwa huduma za afya kwa wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano zinapaswa kutolewa bure katika vituo vya afya vya umma, ikijumuisha huduma za antenatal, uzazi na huduma za mama na mtoto kwa ujumla.

Msimamo huo ulitolewa kufuatia maelekezo ya aliyekuwa Spika wa Bunge wakati huo Dr. Tulia Ackson, aliyemtaka Waziri wa Afya kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyokuwa yakiripotiwa kwenye vyombo vya habari, yanayodai kukiukwa kwa Kifungu cha 5 cha Sera ya Afya kinachoeleza wazi kuwa Serikali ina wajibu wa kutoa huduma za afya bure kwa wanawake wajawazito, watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

"Serikali itenge bajeti ya kutosha"

Mshauri wa Sera na Bajeti kwenye eneo la Afya na Maendeleo ya Jamii, James Malali, amesema licha ya sera kuelekeza wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kupata matibabu bure, utekelezaji unasuasua na kuacha pengo la uwajibikaji.

“Sera inatoa mwongozo kwamba akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano wapate matibabu bure, lakini Serikali haitengi fedha za kutosha kugharamia makundi hayo. Hivyo, vituoni changamoto ya kutozwa gharama hujitokeza,” anasema James Malali

Anaongeza, “Gharama za kujifungua zinaathiri wengi wasioweza kumudu, hivyo baadhi hukwepa huduma au kuingia madeni.”

Ameitaka Serikali kutenga na kupeleka bajeti ya kutosha vituoni na kujumuisha huduma za uzazi wa mpango kwenye Bima ya Afya kwa wote. Ambapo anadai kwamba huduma hiyo ikijumuishwa itawezesha mazingira ya familia kuzingatia mipango ya uzazi.

LHRC: Kuna changamoto ya usimamizi wa Sera

Pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Henga, anasema kuwa licha ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 kuelekeza huduma za msingi kwa akina mama wajawazito na wanaojifungua kutolewa bure, bado kumekuwepo na changamoto katika utekelezaji wake. Anashauri kuwa wale wanaokumbana na changamoto ya kutozwa gharama wawasilishe malalamiko yao kwa mamlaka husika.

“Kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, huduma za msingi za afya, ikiwa ni pamoja na huduma za mama na mtoto, zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vya afya vya Serikali. Hii ni sehemu ya jitihada za Serikali za kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga,” anasema Anna Henga.

Hata hivyo, amedai kuwa changamoto zimekuwa zikijitokeza katika utekelezaji wake, ikiwemo ukosefu wa vifaa vya msingi kama vile mkasi, pamba na vifaa vingine. Amesema kuwa vifaa muhimu vinatakiwa kupatikana katika hospitali. Ikiwa akina mama wanatozwa gharama kwa huduma zinazopaswa kutolewa bure katika hospitali za umma, wanatakiwa kutoa taarifa kwa ngazi za uongozi wa kituo cha afya husika au kwa Wizara ya Afya.

Naye Janeth Rithe ambaye ni mwenyekiti wa ngome ya wanawake Chama cha ACT Wazalendo anasema kwamba akina mama wanaojifungua kwa upasuaji wamekuwa wakitwishwa mzigo mkubwa wa gharama ambao unawaweka katika mazingira magumu ya kiuchumi.
c5204fa8-a13c-41bd-b87d-470a39026ecd.jpeg

Anasema kwamba mzigo huo unatokana na Serikali kushindwa kusimamia vyema mipango inayoiweka. Anashauri rasilimali za Taifa kama madini kwamba zikitumika vyema zinaweza kusaidia kupata bajeti ya kuhudumia kundi hilo.

"Akina mama wanapata shida, huku anaambiwa huduma bure lakini ukienda kwenye vituo vya afya ni gharama. Hata wanaojifungua bila upasuaji ni shida nao wanaambiwa wapeleke vifaa sasa hiyo bure hiko wapi?, kuna akina mama wanaenda kujifungua kwenye vituo vya afya wanaambiwa waende na madumu mawili ya maji kwa ajili ya kujifungulia. Sisi Chama chetu tunapinga huu utaratibu na tumeeleza kwenye Ilani yetu na mikakati yetu namna tunavyoweza kutumia rasilimali zetu kama madini kusaidia wananchi ikiwemo kundi la wajawazito" anasema Janeth Rithe

Mwisho: Sehemu ya kwanza
 
Attachments

  • 9a388099-3c5f-4a94-bc8c-4be443c652ac.jpeg
    9a388099-3c5f-4a94-bc8c-4be443c652ac.jpeg
    86.7 KB · Views: 4
Bora mmeliona hili, ni changamoto kubwa na inachanganya watu wengi
 
Makala👇🏼

Simulizi za akina mama Waliojifungua kwa Upasuaji (Dar);

Licha ya Serikali kusisitiza kuwa wajawazito hawapaswi kutozwa gharama wakati wa kujifungua, hali ni tofauti kwa baadhi ya wanawake wanaojifungua kwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na baadhi ya hospitali nyingine za Serikali zilizopo Dar es salaam.

Msingi wa utoaji wa huduma za gharama nafuu unaelezwa katika Kifungu cha 87(1) cha Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya mwaka 2009, ambacho kinakataza utoaji wa huduma za afya kinyume na maagizo ya Serikali, ikiwemo utozaji wa gharama zisizotambuliwa na sheria pamoja na miongozo iliyowekwa na mamlaka husika.
View attachment 3549138
Mfono wa picha katika chumba cha upasuaji

Miongoni mwa miongozo muhimu iliyotungwa ili kuratibu utoaji wa huduma rafiki kwa wajawazito na wamama wanaojifungua ni pamoja na mwongozo wa kutokutoza wajawazito gharama za huduma muhimu za uzazi (User Fees Exemption for Maternal Health Services), Mwongozo wa Kitaifa wa Huduma za Antenatal (Guideline for Antenatal Care Services), pamoja na Mwongozo wa Huduma Baada ya Kujifungua (National Postpartum Care Guidelines). Mwongozo huu unalenga kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma sahihi ndani ya wiki sita baada ya kujifungua.

Hata hivyo, uchunguzi unaibua hoja kuhusu uzingatiaji wa miongozo hiyo.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza wanasema walitozwa gharama kati ya shilingi laki tano hadi laki nane kwa huduma ya upasuaji wakati wa kujifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Nimejifungulia Muhimbili mwaka huu (2025) na nilitozwa gharama ambayo sikuwahi kuitarajia. Maana tunaambiwa kujifungua ni bure au unachangia kidogo. Lakini mimi nililipa zaidi ya shilingi laki sita baada ya kujifungua kwa upasuaji. Kupata hela hiyo haikuwa rahisi, namshukuru Mungu mume wangu ni mpambanaji, alifanya kila lililowezekana hadi nikapata fedha hizo,” anaeleza Diana Dominic (24).

Anaongeza, “Mfano kama mume wangu angekuwa amenitelekeza, ningetoa wapi hiyo pesa yote? Na kumbuka sikuwa nimejiandaa kwa gharama hizo. Huenda ningezuiwa kutoka hospitalini au ningeuza mali zangu.”

"Nilienda kukopa"
Katika mazungumzo hayo, mume wa Diana, anayejitambulisha kwa jina la Kidevu, fundi ujenzi, anasema alilazimika kukopa shilingi laki tatu ili kugharamia upasuaji wa mkewe. Hata hivyo, anatoa wito kwa Serikali kusimamia utekelezaji wa kauli zake.

“Nitoe wito kwa Serikali isimamie kauli zinazotolewa na viongozi kuhusu unafuu wa gharama kwa wajawazito wanaojifungua, au watuambiwe ukweli mapema ili tujiandae. Maana unategemea unafuu, lakini mwisho wa siku unakuta gharama ni kubwa na unaingia kwenye madeni,” anaeleza Kidevu.
View attachment 3549142
sio picha halisi

"Simulizi nyingine"

Naye Binti Esta Lyimo anaeleza kuwa alipitia changamoto kama hiyo alipokuwa akijifungua kwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akilazimika kukopa fedha kupitia vikoba.

“Gharama ni kubwa sana. Sidhani kama ni nafuu kama inavyosemwa. Nilijifungulia Muhimbili miezi sita iliyopita (Machi 2025). Nakumbuka nilipopata ujauzito wangu wa kwanza, mtoto alifariki wakati wa kujifungua katika hospitali moja mkoani Mtwara. Nilishauriwa nikibeba mimba nyingine niende Muhimbili, na kweli nilifanya hivyo,” anaeleza.

Anaendelea, “Jambo la kufurahia ni kwamba nilimpata mtoto wangu akiwa hai, lakini kilichoniumiza ni gharama kubwa nilizoambiwa nilipie. Nilikuwa na bima ya NHIF, lakini haikunisaidia ipasavyo. Niliambiwa nilipie tena shilingi 547,000, huku kwenye bima wakikata takribani laki mbili. Kwa wakati huo sikuwa na pesa ya kutosha, nikalazimika kukopa kwenye kikoba, kwa makubaliano ya kulipa kidogo kidogo baadaye.”

Sanjari na simulizi hizo, akinamama wengine kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakilalamikia ukubwa wa gharama. Mnamo Agosti 2025, mmoja wa waandishi wa makala hii akiwa katika eneo la Muhimbili, aliwasikia wanawake wawili wakilalamikia ndugu zao kutozwa zaidi ya shilingi laki saba kwa huduma ya kujifungua kwa upasuaji. Alipojaribu kufuatilia, wahusika walidai kuwa malipo hayo yalifanyika kwa fedha taslimu (cash).

Simulizi za aina hii zimekuwa zikisikika mara kwa mara miongoni mwa wanawake wanaojifungulia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, huku maswali mengi yakiibuka kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Serikali na kauli za viongozi kuhusu unafuu wa gharama kwa wajawazito.

Msimamo wa Serikali na Wadau : Wanaona nini?

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali katika kipindi chake cha uongozi imekuwa ikisisitiza kusambaza vifaa na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kupunguza gharama na kupunguza vifo vya mama na watoto.

Vilevile, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Makamu Mwenyekiti wake, Stephen Wasira, kilipiga marufuku utozaji wa fedha kwa wajawazito wanaokwenda kujifungua hospitalini, akisisitiza kuwa huduma hiyo ni bure.

Alitoa kauli hiyo akiwa Mlowo, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, akieleza kuwa sera ya CCM iko wazi kuwa huduma za kujifungua na huduma kwa watoto wenye umri wa miaka 0–5 hazipaswi kutozwa gharama.

Wasira alitoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliodai kuwa wajawazito walikuwa wakitakiwa kulipa hadi shilingi 300,000 ili kupata huduma ya kujifungua, hali aliyosema inakiuka sera na maelekezo ya chama.

“Sera ya CCM iko wazi kabisa. Hairuhusiwi mama mjamzito kulipa fedha ili apate huduma ya kujifungua. Watoto ni baraka, si dhambi. Natoa maelekezo kwa viongozi wa chama ngazi ya wilaya na mkoa kufuatilia na kuchukua hatua pale taratibu hizi zinapokiukwa. Nasisitiza, huduma ya kujifungua ni bure,” alisema Wasira.

Ilani ya CCM inaelekeza nini?
View attachment 3549560
Iliani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020/2025 Kipengengele cha 83 (a) ukurasa wa 136 ilieza juu ya mpango wa "Kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto na kuzitoa bila malipo ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano"
Pamoja na msisitizo huo, wadau mbalimbali wamekuwa wakisisitiza utekelezaji wa miongozo inayolenga kuleta unafuu wa gharama kwa wajawazito.

Chama cha ACT Wazalendo, kupitia ilani na mijadala yake ya mwaka 2025, kiliahidi kupinga utozaji wa gharama kwa wajawazito wanapokwenda kujifungua au kupata huduma za mama na mtoto, huku kikidai kuwa utekelezaji wa sera hizo bado una changamoto.

Mei 2025, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, kupitia aliyekuwa Naibu Waziri kwenye Wizara hiyo, Dkt. Godwin Mollel ilisisitiza kuwa huduma za afya kwa wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano zinapaswa kutolewa bure katika vituo vya afya vya umma, ikijumuisha huduma za antenatal, uzazi na huduma za mama na mtoto kwa ujumla.

Msimamo huo ulitolewa kufuatia maelekezo ya aliyekuwa Spika wa Bunge wakati huo Dr. Tulia Ackson, aliyemtaka Waziri wa Afya kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyokuwa yakiripotiwa kwenye vyombo vya habari, yanayodai kukiukwa kwa Kifungu cha 5 cha Sera ya Afya kinachoeleza wazi kuwa Serikali ina wajibu wa kutoa huduma za afya bure kwa wanawake wajawazito, watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

"Serikali itenge bajeti ya kutosha"

Mshauri wa Sera na Bajeti kwenye eneo la Afya na Maendeleo ya Jamii, James Malali, amesema licha ya sera kuelekeza wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kupata matibabu bure, utekelezaji unasuasua na kuacha pengo la uwajibikaji.

“Sera inatoa mwongozo kwamba akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano wapate matibabu bure, lakini Serikali haitengi fedha za kutosha kugharamia makundi hayo. Hivyo, vituoni changamoto ya kutozwa gharama hujitokeza,” anasema James Malali

Anaongeza, “Gharama za kujifungua zinaathiri wengi wasioweza kumudu, hivyo baadhi hukwepa huduma au kuingia madeni.”

Ameitaka Serikali kutenga na kupeleka bajeti ya kutosha vituoni na kujumuisha huduma za uzazi wa mpango kwenye Bima ya Afya kwa wote. Ambapo anadai kwamba huduma hiyo ikijumuishwa itawezesha mazingira ya familia kuzingatia mipango ya uzazi.

LHRC: Kuna changamoto ya usimamizi wa Sera

Pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Henga, anasema kuwa licha ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 kuelekeza huduma za msingi kwa akina mama wajawazito na wanaojifungua kutolewa bure, bado kumekuwepo na changamoto katika utekelezaji wake. Anashauri kuwa wale wanaokumbana na changamoto ya kutozwa gharama wawasilishe malalamiko yao kwa mamlaka husika.

“Kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, huduma za msingi za afya, ikiwa ni pamoja na huduma za mama na mtoto, zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vya afya vya Serikali. Hii ni sehemu ya jitihada za Serikali za kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga,” anasema Anna Henga.

Hata hivyo, amedai kuwa changamoto zimekuwa zikijitokeza katika utekelezaji wake, ikiwemo ukosefu wa vifaa vya msingi kama vile mkasi, pamba na vifaa vingine. Amesema kuwa vifaa muhimu vinatakiwa kupatikana katika hospitali. Ikiwa akina mama wanatozwa gharama kwa huduma zinazopaswa kutolewa bure katika hospitali za umma, wanatakiwa kutoa taarifa kwa ngazi za uongozi wa kituo cha afya husika au kwa Wizara ya Afya.

Naye Janeth Rithe ambaye ni mwenyekiti wa ngome ya wanawake Chama cha ACT Wazalendo anasema kwamba akina mama wanaojifungua kwa upasuaji wamekuwa wakitwishwa mzigo mkubwa wa gharama ambao unawaweka katika mazingira magumu ya kiuchumi.
View attachment 3549561
Anasema kwamba mzigo huo unatokana na Serikali kushindwa kusimamia vyema mipango inayoiweka. Anashauri rasilimali za Taifa kama madini kwamba zikitumika vyema zinaweza kusaidia kupata bajeti ya kuhudumia kundi hilo.

"Akina mama wanapata shida, huku anaambiwa huduma bure lakini ukienda kwenye vituo vya afya ni gharama. Hata wanaojifungua bila upasuaji ni shida nao wanaambiwa wapeleke vifaa sasa hiyo bure hiko wapi?, kuna akina mama wanaenda kujifungua kwenye vituo vya afya wanaambiwa waende na madumu mawili ya maji kwa ajili ya kujifungulia. Sisi Chama chetu tunapinga huu utaratibu na tumeeleza kwenye Ilani yetu na mikakati yetu namna tunavyoweza kutumia rasilimali zetu kama madini kusaidia wananchi ikiwemo kundi la wajawazito" anasema Janeth Rithe

Mwisho: Sehemu ya kwanza
MIMBA sio Dharula, Unamiezi 9 ya kujiandaa, acheni kulia lia.
 
Back
Top Bottom