Dar Free Market (DFM): Mmoja aliyedaiwa kuwa Jambazi auawa na Polisi kwa risasi

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,835
Usiku huu DFM kimewaka. Nasikia mwingine kaangushwa!

Screenshot_20210719-225840.png



UPDATE:

Katikati ya Mtaa wa Tunisia na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Kinondoni jijini Dar es Salaam; Polisi wamefanikiwa kumuua mtu mmoja anayedaiwa kuwa Jambazi aliyepora simu akiwa na Pikipiki, kuanza kumimina risasi hewani kwa Bastola aliyokuwa nayo.

Kamamda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhan Kingai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jambazi huyo ameuwawa na Polisi waliokuwa doria wakiwa na mavazi ya kiraia ambao walisikia sauti ya Mwanamke aliyeporwa simu na Majambazi wawili waliokuwa kwenye pikipiki moja.

Kelele za mwanamke huyo ziliwashtua Polisi waliokuwa doria karibu na kuanza kuwakimbiza Majambazi hao na kumpiga risasi mmoja wao huku mwingine akifanikiwa kukimbia.
 
Back
Top Bottom