Duuuu, mbona mim naona kama zitakua mwarobaini wa kukatiza ovyo barabara lkn pia zitasaidia kulinda bustan zetuu?? Anyway sikuhiz kila jambo la serikali linaonekana baya! Hata Bombadier ziliitwa mapanga boi
Sijapingana na hili kabisa labda tu kwakuwa umenisoma kwa haraka...ni nacho maanisha ni kwamba ingependeza zaidi kama hili jambo lisingefanywa kwa kukurupuka na kuna maeneo haya hitaji kabisa hizo pingili. ...
Naamini umefika kimara mwisho kwenye stand ya Strabag na kile walichokifanya pale! Ishu ya kukatiza barabara pale imedhibitiwa, lakini angalia wamefanya penye uhitaji tuu na imependeza sio barabara yote
Mwanzoni mwa post nimezungumzia kuhusu Lumbuma na kupongeza na nikaja kuongelea kuhusu Sam Nujoma, na kile kilichofanyika pale (nikijaaliwa nitaweka picha kesho isionekane kama napayuka na kukosoa bila ithibati
kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba kilichopaswa kufanyika pale Sam Nujoma kwanza ni kuondoa vile vifusi vilivyotengeneza matuta na vilima (kumbuka pia hii ni tenda alipewa mtu ya kusafisha barabara lakini kwa uzembe na kubania pesa michanga ikawa haizolewi bali inalundikwa kwenye bustani na pembezoni mwa barabara)
Baada ya kuondoa hivyo vifusi na kutengeneza level ile ya asili vizuri then mashimo yale ya kusimika pingili yangechimbwa na kingefuatia kusimika pingili sasa .... kwa mtazamo wa kawaida pingili nzuri za miti au za plastic ngumu zingekuwa nzuri zaidi kama ungefanyika utafiti wa kutosha kuliko pingili za vyuma! Je huu sio mradi wa mtu?
Pamoja na hayo yote kilichofanyika ni kwenda kinyume nyume kiasi kwamba sasa levelling imekuwa shida kufanyika kwa tingatinga, kuna maeneo ya mawasiliano hasa upande zinapojengwa hostel kule imebidi ile kazi ifanyike kwa mikono kwakuwa bustani ni nyembamba
Ungefuatwa utaratibu kama nilivyoainisha hapo hakika matokeo yangekuwa mazuri sana na kwa gharama ndogo