Kwa muda mrefu sasa,jiji la dar es salaam limekosa mkuu wa mkoa! Toka baraza la mawaziri litangazwe,ambapo Ndg. William Lukuvi aliyekuwa anashika nafasi hiyo alipoteuliwa kuwa waziri-ofisi ya raisi Bunge,jiji hili liko chini ya mtu anayekaimu tu! Maswali yafuatayo yanajitokeza
Hivi kuteua mtu tu nayo ni kazi? Au hatuna 'shemeji aliyebaki' au bado wanasoma?
Je kama tunaweza kukubali jiji kubwa na lenye umuhimu kitaifa na kimataifa likaimiwe, je wakuu wa mikoa wana umuhimu kweli?
Mimi nashindwa kuelewa wana JF nisaidieni!
Mie issue ni huko LINDI ambako KAIMU RC wetu ndio kituo chake cha kazi ina maana nao WANAKAIMIWA TUU kama sisi.....???
tetesi ni kwamba mzee tibaigana ndio anatayarishwa kua mkuu wa mkoa huu
Yupo mtu anaKAIMU jamani. Ana nguvu zote kiutendaji. Sio kwamba mkoa hauna RC.mara ya mwisho nlipata taarifa kuwa mzee Tibaigana kakataa uteuzi huo,kuna afsa uhamiaji mmoja ambaye alikuwa anajiandaa kuwa kampeni meneja wake ila Mama Tibaij uka akazidi kura za maoni,alisema mzee Tiba hataki uteuzi wowote kwanza apumzike,labda kama wameshakubaliana. Ila kwa upande wa pili ndo huone kuwa kuwepo maRC ni kutengenezeana Ulaji. Kama nusu mwaka mkoa hauna Rc na uko salama,si bora cheo kifutwe?
Kwa nini maDC wa mkoa husika wasikaimu nafasi hizi? Jordan Rugimbana wa Kinondoni angefaa sana kuwa Kaimu RC wa Dar. Gama wa Ilala kama Komba wa TOT!
hivi mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya kazi zao ni zipi? si ajabu hata jk haoni umuhimu wao, maana hata kamati za kudumu za bunge zinawachachamalia wakurugenzi wa wilaya na si wakuu wa wilaya au kada yo yote ya mkoa.
sijakuelewa kijana, hebu fafanuwa hapo kwenye RED, nikiamka nikute jibu.