Miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya imejengwa bila kufuata ramani na idadi kubwa ya wakazi katika majiji haya wanaishi kwenye maeneo yasiyopimwa. Miji yote hii haina maeneo makubwa ya wazi ya kupumzika watu ?City Parks?. Mwaka 1985 Botha aliwahi kusema ?Pretoria has been made by the white mind for the white man? hii ilionyesha kwamba watu weusi si watu wanaoweza kuwa na mipango mizuri na endelevu. Kwa wale waliobahatika kutembelea nchi za wenzetu miji yao imepangwa vizuri na ni mipango ya mda mrefu sana. Maeneo kama bonde la msimbazi lilitakiwa lisijengwe toka zamani, kwanini tulishindwa kusimamia?
Jiji la Mwanza limejengwa holela milimani halina hata mvuto, Tuseme maeneo haya ya milimani yamejengwa holela bila idara ya mipango miji kuzuia ujenzi holela. Kulingana na report za UN-Habitat watu wanaendelea kuongezeka mijini na ndio yatakuwa makazi ya watu wengi , tunaomba serikali iunde chombo maalumu cha wataalam kitakachosimamia mipango miji na tuwe na bajeti ya kutosha kupima maeneo mengi zaidi ili watu wajenge maeneo yaliyopimwa.