Chocolate, Manispaa ya Temeke siyo kiboko ya uchafu kama ulivyodai ila kwa ujumla Manispaa zote ni chafu mno mno...Pamoja na yote hayo lakini Manispaa ya Temeke ndio kiboko yao ni chafu kupindukia iko nyuma kwa kila kitu sina uhakika kama kweli kuna Uongozi wa kueleweka katika Manispaa hii wa kufuatilia maendeleo yake
Chocolate, Manispaa ya Temeke siyo kiboko ya uchafu kama ulivyodai ila kwa ujumla Manispaa zote ni chafu mno mno...
(1)Ilala...
Maeneo ya ( City centre,Kariakoo,Ilala Area,Buguruni,Vingunguti nk)
(2)Kinondoni...
Maeneo ya (Magomeni,Tandale,Manzese,Mabibo,Sinza,Mlalakuwa nk)
Ni machafu kuliko maeneo mengi ya Temeke...
Heshima mbele Mzalendohalisi!!Tusker Bariiiidi,
Manzese iondolewe! sii chafu tena siku hizi WB wamefadhili miradi mikubwa ya mitaro ya maji machafu hadi kule Uwanja wa fisi! Maeneo kama Tiptop kuna mahoteli mazuri ya nguvu..na taa za barabarani karibu kila mtaa! Barabara ziko fresh na Manzese kuna biashara kubwa za Kimataifa sasa..wafanyabiasha wakubwa wa Kongo, Zambia, Malawi siku hizi hushukia Masenze kwa vile ni karibu na Ubungu stendi ya Mkoa!
Lini umefika Manzese?
Manzese sii ile ya zamani! Hata juzi tu Mkurugenzi Mkuu IMF alienda Manzese!