Dar es salaam Dar es salaam....Tanzanians needs your Support!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar es salaam Dar es salaam....Tanzanians needs your Support!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meddie, Jun 25, 2011.

 1. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hii ndio capital city yetu lakini inashagaza na kutuangusha sana;
  • Uchafu
  • Foleni; (mwendo wa kilomita 1 unakwenda masaa3). Watu tuliiii – kisa amani!!
  • Barabara mbovu na chafu……...tena ktk maeneo wanakoishi “so called civilized community”
  • Watu wanalipuliwa na kufa kwa mabomu -hakuna maelezo wala uwajibikaji. Watu tuliiii – kisa amani!!
  • Mgao wa umeme masaa 24!! Watu tuliiii – kisa amani!!
  • Vingora kila wakati!! Mnasimama masaa eti kiongozi anapita (hujui anatoka wapi na kwa lipi hasa!)


  • Ukiwa Dar utaona msafara wa magari asubuhi yakienda taratibu kuelekea mjini, jioni msafala unatoka mjini kuelekea Bunju, Mbezi, ruvu, mbagala kuu…. . Mjini wahindi na waarabu kibao lakini kwenye msululu wa magari jioni na asubuhi huwaoni! Hayo ni magari acha wanaofuata reli!! Haya ndiyo maisha siku neda siku rudi.


  • Ikija wakati wa uchaguzi utaona magari yamepambwa kijani, watu wamevaa t-shirt, kofia, kanga wanafuraha kama hawana akili mzuri!! Wanasikiliza mtu akiwaeleza upuuzi kana kwamba ukweli wa maisha yanayowakabili wameyasau/ama hawayaoni. Mkoa huu ndo CCM inajizolea kura kemkem!!!

  • Usiku utaona kila kona mabaa yamefurika hakuna pa kukaa, (utafikiri kuna sherehe furani)! Night activity ni watu kwenda baa tu hakuna jambo jingine!! Utasikia kuna baa mpya imefunguliwa twende…lakini ukifika bia ni ile ile!! Kwenye baa watu wanakaa kwa kustarehe utafikiri hawana hadha yeyote wala haja ya mabadiliko!!

  • Ni mji umesheheni elite wa nchi hii lakini unakosa mchango na msimamo wa dhati inapokuja swala la kuchukua hatua za kuleta mabadiliko ya kweli kisiasa/kiuongozi hapa nchini! Ebu linganisha Dar es Salaam na mikoa kama Arusha, Mbeya, mikoa ya kanda ya Ziwa. Wasomi wengi Dar wanakaa kwanza wanamsikiliza JK anasema nini na wao wanaanza kusupport …aakweli uvunjifu wa amani…aaa udini!!!!

  Kwa kuzingatia umuhimu wa Dar es Salaam kama Capital city, kunahaja kubwa ya wana dar kubadilika na kuhamasika kwa ajili ya kuleta mabadiliko nchini. Najua CHADEMA wanayo support kutoka Dar es Salaam, lakini kama ingekuwa katika kiwango kikubwa kama inayotoka mikoani speed ya mabadiliko ingekuwa kubwa zaidi!

  DAR ES SALAAM PLEASE COME UP AND COME FOR CHANGE WE NEED!

   
 2. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ukiwa na Meya mwenye Phd fake unategemea nini?
   
 3. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanamjua Mbowe na Vog lake la kifahari na club billcanas na wanajua Dr Slaa ana lipwa 7.5 milioni na kodi halipi,wanamjua Haliama Mdee na mambo yale,wanamjua mnyika na harakati za club ambiance! wanaona ni usaniii tu ni bora wafanye kazi zao!
   
 4. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  not clear!!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  eboo.h
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  crap...
   
 7. N

  Ngokongosha JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 708
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 180
  nahisi na wewe unatoka dar
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Strategically unapoongelea wakazi wa Dar unaongelea aina kuu tano, wapo wale wenye kazi zao nzuri tu katika private sector, wanalipwa vizuri sana, hawa wanatoka nyumbani saa kumi na nusu alfariji kurudi saa nne na nusu usiku, Tabaka la pili ni watu wanaofanya kazi serikalini, kwenye mawizara na idara mbalimbali, hawa kila wanapoondoka wanawaza kurudi nyumbani na makusanyo mazuri ama ya kuforge vikao, kuomba rushwa au hata kula madili ya kukwapua pesa za umma, Kundi la tatu ni la wafanyabiashara ndogondogo ambao kila siku wanakuwa busy kuwahi feli au kariakoo shimoni kununua mazao, hawa nao wanakuwa busy kuanzia saa kumi alajiri na kukamilika saa nne asubuhi, kundi la nne ni la commuters, madereva na makonda plus wapiga debe na mateja, hawa nao wanawazia hesabu ya tajiri na hela ya kununulia unga, hawa nao wapo busy kweli. Kundi la tano ni la ma opportunists, hawa wapo mission town, madalali wa kila aina wafanya biashara za kila aina, hawa wote wanawaza kujenga kuwa na usafiri na kama wanao basi kuuhudumia.

  Sasa watu hawa waliopigika kwa kuwa wakazi wa Dar wengi kuwashawishi kuacha shughuli zao ni vigumu sana na ndiyo maana nawapongeza sana CDM kwa kuuweka pending mji wa Dar, watu hawa doesn't care whos's in IKULU wanachofikiria wao ni kutafuta tu. Ndiyo maana wanabinuliwa na kugalagazwa na oleni na migao ya umeme bado wanasema hewala. Hawataki bugudha kwani wanahofia usalama wa vihamba vyao na engine walizo nazo zinazowatafunia mamilioni ya lita za mafuta kwa mwaka kwenye foleni baabarani.
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Foleni kitu gan? Dar hatuangaiki na mambo ya watu! Kila mtu kivyake! Nyie huko mikoan as long as hamna cha kufanya, endeleeni tu kuandamana! Sisi tutatuwa tu tunasoma habari zenu!
   
 10. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanadanganya wajinga wa mikoani,dar watu wanatafuta pesa kwanza,porojo za CDM hawana time nazo
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  ??????
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye bold naona unajidangaya labda Dar es Salaam Kimara bonyokwa au Kimara temboni, wewe unadhani kwa nini CDM hawataki kuitisha maandamano Dar es Salaam? watu huku hawataki huu upuuzi
   
Loading...