Nicolas J Clinton Gabone
JF-Expert Member
- Mar 13, 2014
- 892
- 536
Maoni ya mpango wa maendeleo wa miaka 15-25 wa kuifanya Dar es salaam kitovu cha biashara za kimataifa
Nicolas Jovin Clinton Gabone
Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Vijana wa Mageuzi (JUVIMA)- NCCR-Mageuzi
USICHOKE ISOME YOTE
Dar Es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania na kitovu cha Biashara, Utalii, usafiri na usafirishaji katika bara la Afrika, ili kufikia hadhi ya kuwa kituo cha biashara za kimataifa ni muhimu kuwa na mpango mkakati wa miaka 15-25 ambao utazingatia maendeleo endelevu, miundombinu ya kisasa, ushirikiano wa sekta binafsi, sekta ya umma na ushirika wa Wananchi.
Najua kumekuwepo na mipango kadhaa ya kuifanya Dar Es Salaam kuwa kitovu cha biashara lakini kuna uzembe, kutowajibika na kukosa nidhamu na uadilifu katika mipango mingi ya Nchi, mimi leo niko Dar Es Salaam na nitajitaidi kuonesha namna ninavyoona mimi kama mkazi wa Jiji hili.
Maoni haya yanaweza kuongezewa nyama na wataalamu wetu wa ndani na kimataifa na ubunifuni zaidi kuliko mimi na yakatekelezwa kwa nidhamu, uadilifu na uwajibikaji tunaweza pamoja kuibadili Dar Es Salaam ili kuvutia uwekezaji wa mitaji mikubwa ya kimataifa kwa sababu eneo lake kigeographia ni dhahabu tosha ya kuifanya Dar Es Salaam kitovu cha biashara za kimataifa.
Uchambuzi huu utajumuisha mapendekezo ya kina kuhusu upanuzi wa jiji, ujenzi wa miundombinu, uboreshaji wa maeneo ya kibiashara, makazi bora na nafuu kwa wananchi na uwekezaji wa kimataifa, tukiamua kuibadili Dar Es Salaam inawezekana ndani ya miaka 25 ijayo.
IDADI YA WATU NA UKUAJI WA JIJI
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, Dar Es Salaam ina wakazi zaidi ya milioni 5.3 na inakadiriwa kukua kwa kasi hadi kufikia watu milioni 10 ifikapo mwaka 2040 au karibu zaidi kutokana na uhamiaji wa watu na ongezeko la asili.
Ukuaji huu unahitaji upanuzi wa miundombinu, makazi na huduma za msingi kama maji ya uhakika, umeme wa uhakika na usafiri ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.
UCHUMI
Dar Es Salaam inachangia takribani 40% ya pato ghafi Taifa la Tanzania, hasa kupitia bandari, usafirishaji, viwanda na biashara ili kushindana na majiji makubwa kwenye ukanda wa bahari ya Hindi na Asia ni muhimu kuimarisha sekta ya fedha, biashara, teknolojia na utalii wa kimataifa pamoja na kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (Foreign Direct Investment) nafikifiri sote tunajua kuwa Tanzania inatekeleza mpango wa maendeleo wa 2025 - 2050 ambao kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa mpango huu wa maendeleo ya Taifa unalenga uchumi wa $1 tilioni , ifikapo mwaka 2050 na mimi nataka tujenge Dar Es Salaam kufikia mwaka 2050 liwe Jiji lenye pato la $200B na kuendelea.
MIUNDOMBINU
Msongamano wa magari, miundombinu ya zamani ya usafiri na usafirishaji, mafuriko ya mvua chache, ukosefu wa taa za barabarani ni baadhi ya changamoto za sasa zinazohitaji suluhisho la haraka na la kudumu, makala hii itakuwa na sehemu ya pili ya usalama mara baada ya mapendekezo ya mpango huu, hivyo usikosea kufuatilia sehemu ya pili ya makala hii.
Maitaji ya baadaye yatakuwa pamoja na njia za Reli za kisasa, usafiri wa Anga, mabasi yaendayo haraka (BRT) na miundombinu ya kijani inayozingatia mabadiliko ya tabia ya Nchi na
kutunga sheria ya Dar Es Salaam Metropolitan Agency, kuanzisha wakala huu ili kusimamia mapinduzi ya Jiji.
Hapa nashauri Bunge la Jumhuri ya Muungano kutunga sheria kuhusu wakala wa (DMA) na kanuni ambazo sitasimamia kazi hii kwa uadilifu, nidhamu, uwajibikaji, kujitolea na haraka zaidi kwa miaka 25 ijayo kuanzia sasa.
MAKAZI
Zaidi ya 75% ya makazi ya Dar Es Salaam ni holela holela sana hakuna mpangilio wa makazi unaozingatia usasa wa mazingira ya kizazi cha sasa na kile cha miaka 25 ijayo na kuendelea hasa maeneo kama Tandale, Mbagala, Vingunguti, Buguruni, Gongo la mboto, Manzese , Kigamboni na maeneo mengi ya jiji kwa ujumla sura ya Dar Es Salaam inaitaji mapinduzi ya haraka sana ili kukabiliana na changamoto ya ukuaji holela wa jiji hilo maeneo hayo ni mfano tu wa sura ya Dar Es Salaam.
Mahitaji ya baadaye yatakuwa makazi bora na nafuu yaliyopangwa vizuri yanayofaa matabaka yote kwa kipato cha wananchi wa Dar Es Salaam.
MAZINGIRA
Maeneo kama Kariakoo, Gerezani, Mbagala na Gongo la mboto yana viwango vya juu vya uchafuzi wa mazingira kutokana na msongamano wa magari, watu na viwanda vidogo vidogo, yawezekana haya yote yameandikwa na wataalamu wetu ila utekelezaji wake ni mtiani, sasa mimi naandika tena, ni muhimu kuwekeza katika teknolojia ya kijani na mipango ya kupunguza uchafuzi wa mazingira.
MAPENDEKEZO YA DAR ES SALAAM YA KISASA
1. EXPRESSWAYS
DAR - CHALINZE njia 8 kutoka Chalinze - Morogoro njia 6 hii barabara ni lango la uchumi wa Dar Es Salaam, Halafu
DODOMA - MOROGORO, kutoka katikati ya jiji la Dodoma kwa km 80 njia 8 na kilometers zilibakia kuja Morogoro njia 6 pia.
POSTA - MWENGE njia 6, MWENGE - BAGAMOYO njia 8, BAGAMOYO - SAADANI - TANGA njia 6.
DAR/Mbagala rangi 3 - Mkuranga mjini njia 8, halafu MKURANGA - LINDI - MTWARA njia 6 hii inaweza kuvutia mitaji mikubwa kutoka kusini mwa Afrika na kuifanya Dar Es Salaam kuwa jiji pendwa kutoka kusini mwa Afrika kwa shughuli za utalii, anasa na biashara
POSTA - KISARAWE mjini njia 8
2. UJENZI WA OUTER RING ROAD
BAGAMOYO - CHALINZE- KISARAWE - MKURANGA - KIGAMBONI njia 6
3. LIGHT TRAINS
Line 1, BAGAMOYO - CHALINZE - KIBAHA - MBEZI - POSTA
Line 2, KISARAWE - MKURANGA - KIGAMBONI - POSTA
4. SUBWAY TRAINS
Line 1, POSTA - KARIAKOO - MAGOMENI - MWENGE - MLIMANI CITY/ UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM - MBEZI
Line 2, FERRY - MASAKI - MIKOCHENI - MOROCCO - MWENGE.
Naamini katika mipango ya jiji yawezekana kuna mpango kama huu na yawezekana ukawa tofauti na huu au vinafanana, mimi natoa maoni yangu kulingana na maono yangu.
5. UPANUZI WA BRT
BOKO - KIGAMBONI - MKURANGA
KIBAHA - POSTA
MKURANGA - POSTA
KISARAWE - POSTA - CHALAMBE - MBAGALA RANGI 3
BRT, Subway na Light Trains zinatakiwa kuunganisha Halmashauri mpya za jiji ambazo nitazitaja mbele kidogo na nitaendelea kurudia baadhi ya maeneo kwa sababu ya uitaji mkubwa wa njia za usafiri na usafirishaji hapa Dar Es Salaam miaka 25 ijayo na kuendelea.
6. UPANUZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM
Upanuzi wa Jiji la Dar Es Salaam uunganishe Halmashauri za miji ya Kibaha, Chalinze, Bagamoyo, Mkuranga na Kisarawe Ili kufanikisha upanuzi huo ni muhimu kuunganisha Halmashauri hizi ili kuunda eneo kubwa la kijiografia linaloitwa "Dar Es Salaam Metropolitan Area", mapendekezo ya kuunganisha Halmashauri hizi na Jiji la Dar Es Salaam yanalenga kuubadili Mkoa wa Pwani jina na kuunda Mkoa mpya wa Kilwa/Pwani unaounganishwa na Wilaya za Kibiti, Mafia, Rufiji, Kilwa na kumega sehemu ya Mkoa wa Lindi ili kuunda Mkoa Mpya wa Kilwa/Pwani.
7. MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI
Kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi wa miaka 25 unaozingatia maeneo ya biashara, makazi, viwanda na hifadhi za mazingira, hapa tutumie watalaamu wa ndani kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam, Ardhi University na Dar Es Salaam Institute of Technology wataalamu kutoka vyuo hivi na wataalamu wachache kutoka United Emirates, Korea kusini na Uchina nasema wachache sana ili kazi hii ifanywe na wazawa kwa ushirika wa utaalamu kutoka maeneo mengine ya Dunia ili kuwa na mfumo wa matumizi bora ya Ardhi.
Kupanga maeneo ya Kibaha, Chalinze na Bagamoyo kuwa miji mipya ya kisasa yenye vyuo vikuu na Hospitali za kimataifa, Kisarawe na Mkuranga zipangwe kama maeneo ya kilimo cha kisasa, viwanda vya kusindika chakula na viwanda vikubwa zaidi visiendelee kujengwa Mkoa wa Pwani ila vielekezwe kwenye Mikoa ambayo mimi naiona ya kimkakati ambayo ni Morogoro na Tabora, huku makazi yakiboreshwa na kupangwa upya, Mkoa wa Pwani kusiendelee kujengwa viwanda vizito, serikali ielekeze viwanda vizito kuendelea kujengwa Morogoro na Tabora kwa kuandaa mazingira na miundombinu ya kupeleka viwanda vikubwa zaidi kwenye Mikoa hiyo.
Viwanda ambavyo vimeisha jengwa Mkoa wa Pwani zikiwemo Industrial Parks zinatosha na sasa tunaweza kujenga miundombinu bora ya usafiri na usafirishaji kuelekea Morogoro na Tabora hii ni pamoja na taasisi kubwa za utafiti za Majeshi yetu yote, Kampuni na mashirika ya uzalishajimali ya Majeshi na shughuli za technologia na majaribio yote ya kijeshi vielekezwe Morogoro na Tabora.
Kuunda mamlaka ya Maendeleo ya Dar Es Salaam Metropolitan Agency
Mamlaka hii itasimamia maendeleo ya eneo lote la Dar Es Salaam kama tulivyokuwa na Kigamboni Development Agency ikafa na mamlaka hii itaratibu ujenzi wa miundombinu, upangaji wa ardhi, ushirikiano na wawekezaji wa ndani na nje kwa hatau za awali.
8. UJENZI WA MIJI MIPYA
● BAGAMOYO
Kujenga mji wa kisasa unaolenga utalii wa kimataifa, viwanda vya teknolojia na bandari mpya kubwa zaidi hapa Afrika ya Bagamoyo ambayo itakuwa kitovu cha Biashara kati ya Afrika, Asia, mashariki ya kati na Ulaya, hii ni kutokana na Geographia ya Dar Es Salaam
● CHALINZE
Kupangwa kama kitovu cha Viwanda vidogo vidogo na Logistiki kwa ukaribu na barabara ya Morogoro, Barabara ya Kasikazini na Reli ya SGR, barabara hizi kama ya Morogoro lazima ipanuliwe kuwa njia 8 ili kuruhusu shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
● KIBAHA
Iwe kitovu cha Elimu na Afya ikiwa na vyuo vikuu vya kimataifa na hospitali za hali ya juu, makazi ya kisasa na taasisi za utafiti za kati.
9. UPANUZI WA BARABARA ZILIZOPO
Barabara ya Morogoro ipanuliwe na kuwa njia 8 (4 kwenda 4 kurudi) kutoka Jangwani hadi Chalinze ili kupunguza msongamano, hii nimeisema hapo juu.
Najua Barabara ya Morogoro inafanyiwa upanuzi lakini kwa maono yangu upanuzi huu haukidhi maitaji ya kile ninachokiona mimi kwa miaka 25 ijayo.
Barabara ya Bagamoyo ipanuliwe kuwa njia 8 Mwenge hadi Bagamoyo
Barabara ya Nyerere/Pugu ipanuliwe kuwa njia 8 Posta hadi Kisarawe na ujenzi wa barabara mpya ya mzunguko njia 6 hadi Mkuranga.
Barabara ya Kilwa ipanuliwe kuwa njia 6 hadi rangi 3 kutokea rangi 3 hadi Mkuranga mji njia 8 kwa ajili ya biashara, utalii na usafirishaji wa usindikaji wa chakula
Kujenga barabara mpya za juu kwenye maeneo ya msongamano, barabara ya juu inayounganisha uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na katikati ya Jiji ambayo inaweza kutumia dakika 15 tu kufikia katikati ya Jiji
Kujenga barabara za mzunguko za nje na za ndani ili kupunguza msongamano katikati ya jiji.
Inner Ring Road, Barabara ya njia 4 kwa kuunganisha Ilala, Kariakoo, Upanga na Kivukoni.
Outer Ring Road, Barabara ya njia 6 kuunganisha Chalinze, Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga na Kigamboni
Uboreshaji wa uwanja wa ndege, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ni lango la kimataifa la Tanzania, Ili kuifanya Dar es Salaam kitovu cha usafirishaji na usafiri wa biashara za kimataifa
Upanuzi zaidi wa Terminal III, kukamilisha upanuzi wa Terminal III na ujenzi wa Terminal IV yenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 20 kwa mwaka ifikapo 2035 na milioni 100 kufikia mwaka 2050 na kuongeza maeneo ya biashara, Hoteli za kimataifa naaegesho ya kisasa ndani ya uwanja huo.
Njia za ndege za ziada, kujenga njia mbili nyingine za ziada ili kuruhusu ndege za mizigo na abiria kwa wakati mmoja, lakini maono yangu ni kutenga eneo lingine kubwa kuliko kule Kisarawe kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege mwingine na mkubwa zaidi, yawezekana miaka 70 ijayo (JNIA) itazeeka na kuzidiwa kwa sababu ya maendeleo makubwa ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa anga na biashara kubwa za kimataifa, nimetangulia kusema eneo la Geographia ya Dar Es Salaam ni dhahabu tufanye mapinduzi ya kuibadili Dar Es Salaam kuanzia sasa ni suala la kuamua tu inawezekana.
Terminal I na II ziboreshwe na kuwa majengo ya abiria ya kisasa na usafiri wa BRT, SUBWAY na LIGHT TRAINS uunganishwe kwenye uwanja huo
Kuuganisha (JNIA) na katikati ya Jiji kupitia Light Train, BRT na SGR, upanuzi huo ulenge kuunganisha Terminal zote za uwanja kwa vituo vya kisasa, hapa niseme hivi, BRT ya sasa ina mapungufu ya kimkakati ikiwa pamoja na vituo vya abiria kukosa hadhi ya njia hiyo, unawekaje milango ya "Roller shutter" kwenye hivyo vituo, BRT phase III imezingua kwenye milango ya vituo vya abiria na kwa njia za BRT I, II na zinazojengwa sasa ziwekewe mkakati wa kuzibadili na kuwa za njia za Light Trains na BRT inaweza kuanza kuhudumia maeneo mapya ya Jiji kwenye maeneo niliyoyataja huko katika katika upanuzi wa Jiji.
10 UWEKEZAJI WA SEKTA BINAFSI
Kushirikisha makampuni ya kimataifa ya usafiri wa anga kama Emirates na Qatar Airways kwenye kusaidia usimamizi wa JNIA kutoa utaalamu na uzoefu kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani.
• Light Trains
Kujenga mtandao wa Light Trains unaounganisha maeneo ya ndani ya jiji na nje.
Laini 1, Katikati ya Jiji – Ubungo – Kimara – Kibaha.
Laini 2, Kivukoni – Upanga – Mwenge – Tegeta – Bagamoyo.
Laini 3, Uwanja wa ndege Kisarawe – Mbagala – Kigamboni – Mkuranga.
• Subway Trains
Ujenzi wa Subway Trains ifikapo 2030 katika maeneo ya msongamano wa juu.
Laini ya msingi, Kariakoo – Posta – Upanga – Oysterbay – Mikocheni, yawezekana zipo ambazo zimebuniwa, unaitaji uongozi madhubuti na unaofanya maamuzi ya haraka, mipango hiyo itekelezwe tunaweza kuandaa future ya Dar Es Salaam isijiendeshe kama inavyoonekana leo makazi holela na ujenzi wa miundombinu isiyo ya kimkakati.
11. UPANUZI WA BRT
Mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT) umepunguza msongamano wa magari ili kuimarisha huduma hii
• Awamu za ziada
Kukamilisha awamu ya III katikati ya Jiji – uwanja wa ndege – Gongo la mboto ifikapo 2026, ziada Gongo la mboto - Kisarawe - Chanika - Homeboza - Mvuti - Mbande - Chalambe unganisha na BRT II Mbagala - Vikundu.
• Kuendelea na awamu ya IV Kivukoni – Tegeta - Boko - Bagamoyo.
• Ujenzi awamu ya V Kigamboni Ferry kupitia Darajani - Mandela Raod - Ubungo kufikia 2035, Mandela Raod na Sam Nujoma zijengwe kwa njia 8
• Ujenzi awamu ya VI
Morocco - Mwai Kibaki Road - Kawe - kwa Zena - kutokea Afrikana, hii awamu nafikiri ni upanuzi wa BRT I na II.
• Vituo vya kisasa
Upanuzi wa BRT ulenge vituo vya abiria vya kisasa vilivyo na Wi-Fi, viyoyozi na taa za Sola, lakini wakati huo BRT iendelee kuboresha na kuwa mifumo ya Light Trains.
• Muunganisho na njia nyingine
Bila kushahau ni muhimu mpango huu uunganishe vituo vya BRT, Light Trains, Subways na vivuko vya majini kwa usafiri wa pamoja.
11. UBORESHAJI WA KARIAKOO NA POSTA
Kariakoo na Posta ni maeneo ya kihistoria yanayohitaji uboreshaji wa kisasa na wa kijani
● KARIAKOO
Kujenga masoko ya kisasa ya ghorofa nyingi yenye maegesho ya chini ya ardhi, maduka makubwa (Malls), hapa nataka kusema baadala ya wamiliki wa viwanja pale Kariakoo kila mtu kujenga kajengo kake kama mpango wa sasa ulivyo, serikali idhamini ujenzi wa pamoja wa maduka makubwa (Malls) na majengo marefu zaidi, huku serikali kupitia NHC na TBA ikishirikiana na sekta ya umma na binafsi kujenga majengo makubwa kwa ajili ya kubadili sura ya Kariakoo kama soko la biashara za Kimataifa.
Kuboresha na kupanua barabara za ndani na kuweka taa za sola za kisasa na Camera za CCTV ili kubeba sura nzuri ya Kariakoo, hii inalenga pia kuondoa biashara ndogo ndogo za machinga katikati ya barabara za Kariakoo ili kuruhusu smooth movement ya biashara, magari na watu.
Kuunda maeneo ya wafanyabiashara wadogo wadogo (SME Zones) zenye maduka nafuu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo wote ili waondoke kwenye mitaa na barabarani, teknolojia ya ujenzi wa kudhibiti majanga ya tetemeko la Ardhi na moto izingatiwe vyema, ujenzi wa maghorofa Kariakoo uende mpaka ghorofa 40 + 50 na maduka ya kisiasa ya kimataifa (Malls)
Gerezani kuna uchafuzi wa mazingira vile viwanda vidogo vidogo vyote vielekezwe maeneo mengine yenye miundombinu ya kisasa SIDO inahusika kimkakati hapa kwenye usimamizi wa viwanda vidogo vidogo vyote kwenye maeneo ya makazi mapendekezo viwanda hivi vidogo vidogo vielekezwe Mkuranga.
● POSTA
Kuboresha majengo ya kihistoria kuwa vitovu vya biashara na utalii, kujenga maghorofa ya biashara yenye muonekano wa kisasa kuanzia ghorofa 60 + 80, ujenzi wa kudhibiti tetemeko na majanga mengine uzingatiwe vyema.
Ujenzi wa Dar Es Salaam Financial Tower jengo lenye ghorofa 80 ambalo litakuwa na Bank za kimataifa, ofisi za makapuni na Hotels na kuvutia uwekezaji wa majengo marefu, barabara zote za posta ziboreshwe au kujengwa upya na kuwa na mifumo bora ya maji taka, taa na miti inayolinda asili ya Dar Es Salaam.
● KUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Kuzuia viwango vya juu vya uchafuzi wa hewa na kelele kwenye maeneo yote ya Jiji, mapinduzi ya mkakati huu yanalenga Dar Es Salaam kushindana na majiji makubwa kutoka Asia, halafu majiji kama Nairobi tuiwezeshe Arusha iwe mshindani wa Nairobi na majiji mengine jirani
12. MAKAZI BORA NA NAFUU
Ili kushughulikia changamoto za makazi holela kama yanavyoonekana sasa kwenye makazi ya zamani na yanayoendelea kujengwa sasa hivi;
• Makazi ya ghorofa
Kujenga majengo ya ghorofa za gharama nafuu katika maeneo kama Mbagala, Ukonga, Kigamboni kwa tabaka la chini na la kati, tunaweza kutumia mifano ya Singapore ya makazi ya umma (HDB Flats).
Maeneo ya makazi yote duni kama Mbagala, Temeke, Tandale, Manzese, Ubungo, Mabibo, Buguruni, Vingunguti, Tabata, Sinza, Buza, Kiwalani, Gongo la mboto, Chanika, Pugu na maeneo mengine mengi.
Yajegwe majengo ya ghorofa 10 + 20 nyenye nyumba za gharama nafuu kwa wananchi
Mfano,
MBAGALA na TEMEKE
Kujenga nyumba za tabaka la kati na chini zenye uduma ya maji, umeme na barabara bila kusahua Internet ya uhakika.
TANDALE na MANZESE
Kubadilisha maeneo ya holela kuwa makazi yaliyopangwa vizuri yenye shule na Hospitali za kawaida.
UBUNGO na BUGURUNI
Kujenga makazi ya pamoja yenye biashara ndogo ndogo.
Kawe
Eneo la Pwani lenye fukwe na Hoteli, kujenga "Kawe Entertainment District" yenye Hoteli za kimataifa, vilabu vya usiku na migahawa ya anasa kando ya Beach za Kawe, kutengeneza eneo la matembezi (Promenade) lenye maduka na burudani na kujenga "Kawe Arena" ukumbi wa kisasa wa matamasha ya michezo, burudani na mikutano ya kisiasa wenye uwezo wa watazamaji 20,000.
Sinza
Eneo la makazi lenye msongamano na biashara ndogo ndogo, eneo hili tunabadilisha kuwa "Sinza Lifestyle Hub" yenye sinema za kisasa, viwanja vya michezo, maduka ya rejareja na kujenga "Sinza Culture Arena" ukumbi wa maonesho ya kitamaduni, muziki na matukio ya kisiasa wenye uwezo wa watazamaji 10,000, kupanua barabara za ndani na kuweka taa za sola kwa usalama.
Tabata
Eneo la makazi duni lenye changamoto ya miundombinu huku tunaboresha miundombinu ya Tabata kwa kujenga barabara za lami na mifumo ya maji taka, kujenga "Tabata Family Park" bustani ya umma yenye viwanja vya michezo, sinema za wazi na migahawa ya familia na "Tabata Sports Complex" yenye matukio ya kisiasa, mihadhara ya kidini na matamasha makubwa ya muziki wa injili na bongo flavor
Ujenzi wa "Dar Es Salaam Grand Arena" huko Masaki pia wenye uwezo wa watazamaji 40,000 kwa ajili ya matamasha ya kimataifa, michezo na maonyesho, kutumia teknolojia ya kijani kama paneli za sola na mifumo ya kukusanya maji ya mvua katika Arena hizo na kushirikisha makampuni ya kimataifa kama Live Nation na AEG katika usimamizi wa Arena huku wataalamu wetu wakipewa kipaumbele.
Ujenzi wa majengo marefu ya biashara kando ya barabara ya Bagamoyo, barabara ya Bagamoyo ni moja ya barabara zinazo vutia sana inaweza kubadilishwa kuwa eneo la biashara la kimataifa.
• Usanifu wa skylines
Kujenga maghorofa marefu ya 60+80 kando ya barabara ya Bagamoyo kutoka Posta hadi Tegeta, kwa kutumia muundo wa kisasa unachanganya glasses, chuma na teknolojia ya kijani kama paneli za sola na udhibiti wa tetemeko kwenye majengo ya kisiasa.
Mwenge
Kujenga "Mwenge tech hub" majengo ya ghorofa 30 yenye viwanda vya teknolojia na vituo vya uvumbuzi.
Tegeta
Kujenga "Tegeta trade center" majengo ya ghorofa 50 yenye masoko ya kimataifa na maeneo ya maonyesho.
• Miundombinu ya msingi
Huduma za maji safi ya uhakika, mifumo ya maji taka na umeme wa uhakika, upanuzi wa barabara za ndani na kuweka taa za barabarani.
• Uwekezaji wa kiuchumi wa biashara ndogo ndogo za machinga
Kuunda maeneo ya biashara ndogo ndogo (SME Zones) katika kila eneo lenye masoko ya kisasa na kutoa mikopo, mafunzo ya ujasiliamali na fursa za ajira kwa miradi ya ujenzi.
• Ushiriki wa wananchi
Wananchi wajulishwe kuhusu maendeleo kupitia mikutano ya hadhara na kuwapa wakazi hisa katika miradi ya makazi kupitia mifumo ya ushirika na kuelimisha wananchi juu ya fidia na nia ya kutaka Dar Es Salaam kuwa kitovu cha biashara za kimataifa kwa sababu ya Geographia yake ya kimkakati kuvutia biashara na mitaji mikubwa ya kimataifa.
• Ushiriki wa sekta binafsi
Kutoa motisha kama punguzo la kodi kwa wawekezaji wanaojenga nyumba za gharama nafuu, shirikisha Bank za ndani kama CRDB, NMB, TCB, AZANIA, TIB na mashirika ya umma kama TBA, NHC Watumishi Housing kwenye ujenzi wa makazi bora na nafuu, kutia wawekezaji kwa mikataba ya PPP kwa wawekezaji wa kimataifa katika ujenzi wa Reli, Barabara na Bandari na makampuni ya China, UAE na Singapore kwa ujenzi wa maghorofa marefu na miji mipya.
• Uboreshaji na upanuzi wa Oysterbay, Morocco, Victoria, Mikocheni, Masaki, Msasani na Upanga
Maeneo ya Oysterbay, Mikocheni, Masaki na Msasani ni maeneo ya kifahari yenye Makapuni ya kimataifa na makazi ya viongozi pamoja na Balozi, serikali ya Tanzania imeisha hamia Dodoma hivyo makazi ya viongozi na mabalozi yaelekezwe Dodoma na makampuni ya kimataifa yabakie, huku Arusha nayo ikiendelea kuvutia makampuni na mashirika ya kimataifa ikishindana na Nairobi, nimetangulia kusema Arusha nayo iwekewe mikakati ya kushindana na Nairobi.
1. Upanuzi wa barabara ya Toure Drive kwa njia 6, barabara hii inatakiwa kuwa ya mzunguko kuizunguka Bahari ya Hindi kwa kuunganisha Bagamoyo, Tanga, Kigamboni, Chalinze na Mkuranga, ujenzi wa barabara za matembezi kando ya Pwani ya Habari ya Hindi.
2. Mikocheni, upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki + BRT kwa njia sita na ujenzi wa barabara za juu kwenye msongamano.
3. Masaki, upanuzi wa barabara zote za eneo hilo, bila kusahua maeneo haya yote mifumo ya maji taka na taa za barabarani
4. Msasani, upanuzi wa barabara zilizopo na kuzingatia yale niliyoyasema huko juu
5. Kuunganisha Oysterbay, Mikocheni, Msasani, Masaki, Upanga Posta, Kariakoo, Ilala, Kinondoni, Mwenge Kawe, Sinza, Mbezi beach, Kunduchi, Ununio, Goba, Ubungo, Sinza, Victoria, Morocco kwa usafiri wa Light Trains vyenye vituo vya kisasa vya abiria na Internet ya uhakika
6. Maeneo ya Biashara na utalii, kubadilisha Oysterbay kuwa eneo la Hoteli za anasa na vilabu vya Pwani, kujenga "Mikocheni business park" kuwa eneo la ofisi za makapuni ya kimataifa na kupanga Msasani kama eneo la makazi ya kifahari yenye majengo ya ghorofa 30.
• Ujenzi wa maghorofa marefu Ubungo, Kinondoni, Victoria, Mikocheni, Morocco na Upanga
Ubungo
Kujenga jengo la ghorofa 50 lenye ofisi, makazi na maeneo ya biashara na kujenga eneo la maduka ya biashara ya rejareja na sinema.
Kinondoni na Ilala
Kujenga majengo ya ghorofa 30-40 yenye makazi ya tabaka la kati na juu na kujenga eneo la "Kinondoni innovation hub lenye viwanda vya teknolojia.
Morocco
"Kujenga Morocco trade center" jengo la ghorofa 60 lenye masoko ya kimataifa na Hoteli, Ikumbukwe upanuzi wa BRT kwenye eneo hili uzingatie vigezo niliyoyataja hapo awali.
Victoria
Kujenga maghorofa ya makazi ya kifahari yenye muonekano wa Bahari ya Hindi na kuwepo kwa eneo la biashara lenye ofisi za makapuni ya teknolojia.
Mikocheni
Kujenga "Mikocheni sky towers" yenye ghorofa 50 na Hoteli na kupanga eneo la biashara lenye Bank za kimataifa.
Upanga
Kujenga "Upanga financial district" eneo la majengo ya ghorofa 60+ lenye Bank, masoko ya hisa na ofisi.
Mipango miji
Kupanga maeneo mapya ya makazi yenye shule, hospitali na bustani za umma.
Ushiriki wa dekta binafsi, wananchi na taasisi za elimu ya juu ni muhimu, ili kufanikisha mpango huu, ushirikiano wa pande zote ni muhimu sana
Sekta binafsi
Kutoa mikataba ya PPP (Public-Private Partnerships) kwa miradi ya miundombinu kama BRT, Reli na maghorofa marefu zaidi, kuvutia wawekezaji wa kimataifa kutoka China, UAE na Singapore kwa ujenzi wa maghorofa marefu na miji mipya.
Wananchi
Wananchi wajulishwe kuhusu faida za miradi na fidia kupitia mikutano ya hadhara na vyombo vya habari, wapewe fursa za ajira katika miradi ya ujenzi.
Taasisi za serikali
Kuunganisha juhudi za TANROADS, TARURA, DAWASCO/DAWASA, TANESCO, Mamlaka ya Dar Es Salaam Metropolitan Area (DMA) na Manispaa 10 za Jiji la Dar Es Salaam
1. Ilala
2. Kinondoni
3. Kigamboni
4. Temeke
5. Ubungo
6. Mkuranga
7. Kisarawe
8. Bagamoyo
9. Kibaha
10. Chalinze.
Hapa lazima kuwepo uwazi katika utoaji wa tenda kwa haraka na utekelezaji wa miradi kwa nidhamu, uadilifu na kujitolea haya yote yatokee na uajibikaji.
Kushirikisha vyuo vikuu kama UDSM, Ardhi University na DIT kwenye usanifu wa miji na miradi ya teknolojia ya kijani na kuunda vituo vya utafiti vya biashara na teknolojia ili Dar Es Salaam iweze kuhudumia na kuhodhi majiji ya mengine ya Afrika Mashariki, Kati na kusini mwa Afrika.
Uwekezaji katika maghorofa marefu, ili kubadilisha skyline ya Dar es Salaam, ni muhimu kuwekeza katika maghorofa marefu katika maeneo ya Posta, Kigamboni, Kariakoo, Upanga, Oysterbay, Mikocheni, Morocco na Victoria, Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Mwenge mpaka Tegeta na Sinza.
Motisha za wawekezaji
Kutoa maeneo ya ardhi bila malipo kwa wawekezaji wanaojenga maghorofa marefu zaidi na kupunguza kodi ya biashara kwa miradi ya maghorofa marefu.
Upanuzi wa Bandari ya Dar Es Salaam na kujenge Bandari mpya huko Bagamoyo yenye uwezo wa kushughulikia ukubwa wa meli za aina yoyote.
Kujenga maeneo ya kifedha Dar Es Salaam International Financial Centre (DIFC) kwenye eneo la Upanga na kuboresha fukwe za Bahari ya Hindi, kujenge Hoteli za kimataifa Bagamoyo na Kigamboni, kupanga maeneo ya kihistoria kama Kariakoo na Posta kuwa vivutio vya utalii na kuunda Silicon Valley ya Afrika Mashariki na Kati pale Kibaha yenye viwanda vya teknolojia na vituo vya uvumbuzi.
Hitimisho
Mpango wa miaka 15-25 wa kufanya Dar es Salaam jiji la kisasa unahitaji maono ya pamoja, uwekezaji mkubwa wa ndani na kimataifa na ushirikiano wa sekta binafsi, umma na Wananchi.
Kwa kuunganisha Halmashauri za Kibaha, Chalinze, Bagamoyo, Mkuranga na Kisarawe kuwekeza katika miundombinu ya usafiri, makazi bora na nafuu na maghorofa marefu, Dar es Salaam inaweza kushindana na majiji kama Hong Kong, Beijing na Dubai.
Utekelezaji wa mapendekezo haya utahitaji uwazi, uwajibikaji na dhamira ya dhati ya mapinduzi ya kufanya jiji hili kuwa kitovu cha biashara, utalii na teknolojia.
Jina; Nicolas Jovin Clinton Gabone
Elimu; Shahada ya kwanza katika mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia
Mawasiliano; 0710543730
Email address; nicolasjclinton2@gmail.com