Vijana wengi wamekuwa wanapenda mapenzi kuliko kazi. Leo hii kijana unaweza ukamkuta anafanya kazi pesa yake haionekani inaishia kwa wanawake tu, anashindwa kujihudumia yeye kama yeye kisa ampe mwanamke fulani hivi.
Vijana tumekuwa tunapenda sana tundu zile kuliko kuzipenda afya zetu. Hivi mnajua kwanini mwanamke kapewa zile sehemu na unajua kwanin mwanaume kapewa mashine ile? Tupo katika kupeana somo ili tujirekebishe tusipostuka mapema utazeeka huku ukiwa hujafanya kitu chochote katika maisha yako.
Kijana usipoamua kutafuta pesa sasa basi usitegemee kama kuna nafasi ya kuokota embe chini ya mnanasi. Hivi mnajua vijana wengi tumetokea mazingira magumu sana? Leo hii unaweza ukamkuta kijana anakopi maisha kuliko kuishi maisha yake ya uhalisia.
Unaweza ukamkuta kijana maisha ya nyumbani kwao ni magumu sana, mlo mara tatu au mara mbili kwa siku haupatikani, ukamkuta anafanya vitu ili aonekane maisha yake ni mazuri kumbe magetoni mwake kuna kitanda cha kamba tu.
Pia hizi smartphone zimetulemaza sana sasa hivi, kijana hataki kazi eti kisa na anatambo utandawazi ulivyokuwa ni mkubwa sana dunian. Siyo kijana tu adi wazee wapo pia, asipomiliki macho matatu basi haonekani mtu katika watu.
Katika maisha kuna vitu viwili, kuna pesa na mapenzi; ukiacha kimoja ukashika kimoja basi we utatoboa tu. Ukiacha mapenz ukatafuta pesa kutoboa ni must sana. Fikiria unafanya kazi ya kubeba zege then ile pesa yako unayopata unaenda kukosha uchinjo, kwanini ushindwe kuwekeza katika maisha yako ili utoke maisha unayoishi kwa sasa?
Vijana tuamke tuache mambo fulani hivi ayana mana usipostuka sasa usitegemee ukizeeka utazinduka unajiongopea. Fikiri kabla ya kufika miaka 20 ulikuwa na maisha gani na baada ya kuvuka miaka 20 utakuwa ni mtu waina gani.
Amka kijana, chini kunauwa, danga alivimbiwi tafuta pesa! Utastukia umezeeka hakuna ulichokifanya katika maisha yako.