wiki iliyo pita tumetembelewa hapa chuoni kwetu na watu wa damu salama, yule afisa alieleza mambo mengi juu watu wanao paswa kuchangia damu na magonjwa ambayo yanasababisha watu wasichangie. Vile vile tulipata fursa ya kufunzwa juu ya makundi ya damu na yule afisa alisisitiza kwamba watu wenye damu grupu O postive ni wachache sana na huwa inawapa changamoto likitokea hitaji la grupu hiyo.
baada ya semina ya kina, afisa wa damu akawapa fursa wanafunzi kuuliza masweli, na mwanafunzi wakwanza kupewa fursa hiyo huku akiwa na hofu aliuliza hivi!
..... wakati mnapima damu yangu mkigundua kua nina grupu O postive, naomba munibadilishie niwe grupu nyingine!!!