Dalili za Utawala unaoelekea 'kaburini'

Dalili za Utawala unaoelekea 'kaburini'

cerengeti

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
3,879
Reaction score
1,631
Na Mwinjilisti Kamara Kusupa.

DALILI ya kwanza na ya wazi ya utawala ulioshindwa ni ukatili. Utawala ulioshindwa kuiendesha nchi lakini bado uko madarakani ni lazima utatawala watu kwa ukatili mkuu.

Dalili nyingine ya watawala walioshindwa kutawala lakini bado wakawako madarakani ili kusogeza siku na kuingoja rasmi siku ya kuondoka kwao, ni "uwongo". Ukiona wameanza kusema uwongo mweupe na hawawaambii watawaliwa ukweli, elewa waai kuwa si kwamba ukweli haupo bali ukweli wa kuwaambia wananchi upo isipokuwa kinachokosekana hapo ni ile Moral authority au sheria ya rohoni, kitu ambacho ni muhimu sana kwa utawala na uendeshaji wa nchi.

Sheria za nchi peke yake pasipo morali hazitoshi kufanya nchi itawalike, wala vyombo vya dola na matumizi ya mabavu havitoshi kuifanya nchi itawalike. Mfano hai ni utawala wa makaburu huko Afrika Kusini, ulikuwa na nguvu zote yaani nguvu za kiuchumi, teknolojia ya hali ya juu, nguvu za kijeshi, nguvu za polisi, pamoja na uimara wenyewe wa mfumo wa kisiasa yaani mfumo wa kibaguzi ambao ulikuwa umedumu kwa miaka mia tatu tangu ulipoasisiwa.

Lakini vyote hivyo havikutosha kuzuia wala kuhimili wimbi la mabadiliko kutoka kwa wananchi (hasa wazalendo), hapo waliposema "utawala huu sasa basi", makaburu walipiga, waliua, walitesa na kufunga watu kwenye jela zao lakini wapi, hakuna kilichowazuia wananchi wasiusukumie kaburini utawala waliouchukia na kuchoka nao.

Mtawala ukiishachokwa njia pekee iliyo bora ni kutoka madarakani kwa amani badala ya kungoja kusukmwa na hasira za wataliwa hadi mtu ang'ang'anie kubaki madarakani kwa gharama zozote.

Tukirudi kwenye dalili ya kwanza ya utawala ulioanguka hali ukingali madarakani, yaani dalili za "ukatili" dhidi ya wananchi wake inaowatawala ni wazi kwamba tunaweza kuutafsiri ukatili huo kama hatua ya mwisho ya kutapatapa ya mtawala mfanya maji ambaye analazimika kushika maji hayo hayo yanayomuua.

Wiki iliopita polisi wameupiga mabomu ya machozi mkutano wa chama cha CUF uliokuwa unafanyika pale Manzese. Kipigo hiki kimetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Afande Mahita akiwa kama mkuu wa jeshi la polisi kutoa tamko ramsi la kuwataka polisi wawe ngunguri kwa kupiga rungu mtu yeyote anayejitambulisha kama mwana ngangari. Je, ukatili wote huo ni wa nini? Na lengo lake hasa ni nini?

Jibu lake tunalipata katika historia ya hapa nchini na ya madola mengine makubwa katika dunia ambayo yalichokwa na wananchi wake, na watawala wao wakapata kiwewe na mwisho wakaamua kupambana na wananchi wao kwa kutumia nguvu zinazozidi kawaida.

Mnamo 1995 Afande Mahita akiwa Mkuu wa polisi wa Mkoa Kilimanjaro (RPC) alimsaidia mgombea wa CCM kwa kupiga mabomu mengi mikutano yote ya Mrema mkoani Kilimanjaro ili kuwatawanya washabiki lakini papo hapo kuwakomoa wananchi kwa kutoipenda CCM na kuamua kushabikia upinzani. Hatimaye baada ya Mkapa kula kiapo cha Urais, akamteua Afande Mahita kuwa Inspekta Mkuu wa Polisi yaani IGP.

Lakini tatizo liko pale pale utawala uliodumu kwa miaka yote tangu nchi ipate uhuru umechokwa na wananchi kwa sababu umefanya madhambi mengi, hauna dalili yoyote ya kutubu wala kujirekebisha, na hapo ndipo inapoanzia sera ya ukatili ya piga! Kanyaga umiza! Kisa eti hao wananchi kwanini wanasusia mikutano ya CCM (Chama tawala) na kuamua kuhudhuria kwa wingi mikutano ya chama cha upinzani cha CUF.

Nia halisi ni kutaka kuwatisha na kuwaogopesha watu kuhudhuria mikutano ya CUF. Na sababu nyingine labda ni kuwakomoa hao wananchi kwa kuwa tu wameonyesha waziwazi kwamba wanaichukia CCM na wangependa kutawaliwa na chama kingine.

Hata hivyo, hiyo gia ya ukatili anayokwenda nayo Afande Mahita siyo dawa ya kuiokoa CCM, badala yake ni kuisindikiza CCM kaburini. Nasema hivyo kutokana na kujua wazi kwamba mkutano ule uliitishwa kutokana na kujua wazi kwamba mkutano na CUF lakini wote waliohudhuria siyo CUF wengine ni wana CCM, wana TPP, na wengine hawana chama chochote bali ni wakereketwa wa maendeleo na utawala bora, ndiyo maana wanajitokeza kwa wingi kumsiliza mgombea anayetarajiwa kushinda na kuwaongoza ili waweze kuamua kumpa yule aliyeshibisha nafsi zao miongoni mwa wagombea wengi.

Sasa kosa lao ni nini hata waumizwe na mabomu? Afande Mahita asingeweza kuupiga mabomu mkutano wowote ambao unafanywa na CCM hata kungetokea fujo za kusababisha watu kufa. Tumeyaona hayo kwenye zoezi la kura za maoni za CCM ambapo watu wamekatana mapanga, wamepigana, na kutishana kwa bostola lakini polisi wakafumba macho yao na kujifanya hawaoni kwakuwa tu madhambi yanayofanyika ni ya chama tawala.

Vivyohivyo nao wazuia rushwa wakaifumbia macho rushwa ya CCM iliyotembezwa wazi wazi kwenye kura za maoni. Hii ndiyo aina ya viongozi wanaotaka kushika makali ya dola baada ya uchaguzi wa Oktoba 29..
Je, chini ya utawala wao unatarajia kupata Tanzania ya namna gani? Ukweli ni kwamba kama CCM ikishinda tutakuwa na Tanzania inayofanana na "kuzimu". Vyombo vya dola chini ya uongozi kama wa akina Mahita vitazidi kuwa butu lakini papo hapo katili sana kwa raia wema, sheria za nchi zibataki kuwa kama mapambo tu, na udhalimu utajiendesha kwa uhuru zaidi refarii wa kuuchezesha udhalimu wote atakuwa ni Bwana na Bibi rushwa.

Sasa hivi mtu anayeijia Tanzania kwa nguvu ya fedha ni sawa na ajaye na nguvu ya Mungu ambayo mambo yote yawezekana na hakuna lisilowezekana. Kwa nguvu ya fedha mtu anaweza kumnunua Afisa yeyote. Nguvu ya fedha inawezesha lolote hata kama litakuwa tendo la uhaini wa hali ya juu wa kuangamiza nchi.

Hii ni kwa sababu watu sasa wanajali maslahi ya muda mfupi na faida za papo kwa papo. Hali hii imetokana na watu kukata tamaa ya maisha na kuamua kubangaiza na neno ambalo kwa lugha nyingine linatiwa "survaival".

"Survival" ni maisha yaliyokusudiwa wanyama siyo watu. Sisi wanadamu tulikusudiwa "tuishi" yaani "life" na siyo "Survival". CCM ndiyo iliyopindua maisha ya Mtanzania na kuyateremsha chini hadi kuwa sawa na maisha ya Sungura aliyeko mbuga za wanyama ambaye kuishi kwake kunategemea ujanja wake wa porini na chenga nyingi.

Chini ya mfumo huo au mapinduzi ya aina hii, mtu mwaminifu anageuka kuwa mkosaji.

Wapo watu waaminifu ambao wametumikia serikali au mashirika ya umma kwa uaminifu hadi muda wao wa kustaafu, hawakuiba wala kuhujumu, hivi sasa wengi wao wanajuta kwa mateso wanayoyapata wala utawala hauwajali.

Chini ya hali hiyo uzalendo ni lazima ufe, na anayeua uzalendo katika nchi hii ni utawala wa CCM. Uzalendo ukisha kufa kabisa na isiwepo japo chembe ndogo tu kwa watu wachache, hapo ndipo nchi inapofanana na Sodoma na Gomora ambapo walihitajika wenye haki watano tu ili nchi isiangamizwe lakini wakakosekana.

source:
 
Kila mtu kaguswa na utawala huu. Hakuna uhuru wa habari & Utawala wa sheri, Hakuna Ajira wala motivation kwa wafanyakazi kwa miaka 5, wafanyabiasha wanalalamika hali ngumu ya mifumo ya kodi, mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini, nchi kuwa na mikosi ya majanga kwa takribani miaka 5. Nchi kutawaliwa kimabavu kwa police kudhibiti watu na ulinzi wa Rais kuongezeka.

Hakuna dalili za tume huru kuelekea uchaguzi, kitu kitakachoongeza mgogoro wa kisiasa. Nchi kuwa kwenye rada za Marekani, UN na Umoja wa Ulaya; Nchi kuanza kutengwa na majirani. Mwisho taifa huenda likawekewa vikwazo kama ambavyo tayari tushakosa pesa za corona kutoka IMF.

Kibaya zaidi na hatari ni washauri kuanza kuwa kimya, Wazee kunyamaza, Wananchi hasa walioenda shule na kukosa ajira kuishi kwa hasira, wale wasioenda shule kuishi kwa kukata tamaa.

Na mwisho ahadi hewa mil 50 kila kijiji, ajira, uchumi, bwawa la umeme bado, ndege na SGR vimegubikwa na usiri mkubwa wa harufu ya ufisadi. Kama haujaguswa basi malaika.

Je, utawala huu unasalimika?
 
Usiseme kila mtu kaguswa. Wanajeshi, meno, mataga, lumumba buku saba na mapolisi hawajaguswa hata kidogo. Kama wangeguswa hata kidogo (wanajeshi, meno na polisi) wangefanya mapinduzi kama aliyofanyiwa Mugabe. Kwa hiyo pambana mkuu. Cha msingi jikinge na corona.
 
Je utawala huu unasalimika?
Salama yake inajulikana ilipo.

Hata kama waTanzania wangekuwa ni watu wajinga kuliko wote duniani, pakiwepo na uchaguzi huru na haki, hawawezi kamwe kuchagua kiongozi wa ajabu sana kama huyu.

Yaani itakuwa na maana kwamba hata huko CCM kwenyewe hakuna viongozi wenye sifa za uongozi; hata kama kwenye upinzani hakuna wanayemtaka?
 
Kila Mtu kaguswa na utawala huu, Hakuna uhuru wa habari & Utawala wa sheri, Hakuna Ajira wala motivation kwa wafanyakazi kwa miaka 5, Wafanyabiasha wanalalamika hali ngumu ya mifumo ya kodi, Mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini, Nchi kuwa na mikosi ya majanga kwa takribani miaka 5, Nchi kutawaliwa kimabavu kwa police kudhibiti watu na Ulinzi wa Rais kuongezeka.

Hakuna dalili za tume huru kuelekea uchaguzi kitu kitakachoongeza mgogoro wa kisiasa, Nchi kuwa kwenye rada za Marekani, Un na Umoja wa ulaya, Nchi kuanza kutengwa na majirani, Mwisho taifa uenda likawekewa vikwazo kama ambavyo tayari tushakosa pesa za corona kutoka IMF.

Kibaya zaidi na hatari ni washauri kuanza kuwa kimya, Wazee kunyamaza, Wananchi hasa walioenda shule na kukosa ajira kuishi kwa hasira wale wasioenda shule kuishi kwa kukata tamaa.

Na mwisho ahadi hewa mil 50 kila kijiji, ajira, uchumi, Bwawa la umeme bado, Ndege na SGR vimegubikwa na usiri mkubwa wa harufu ya ufisadi.kama haujaguswa basi malaika.

Je utawala huu unasalimika?
Utawala wa Magufuli ni imara na wa mfano katika Afrika
1. Umeme kila kijiji kwa bei chee kupitia REA
2. Bima ya Afya na mfuko wa Afya ya jamii nchi nzima
3. Elimu bure hadi kidato cha NNE
4. Amefufua reli ya kati na reli ya Tanga, saivi ni kutekeleza SGR
5. Umeme wa uhakika nchi nzima kupitia Kinyerezi 1&2 na sasa mpango ni Stiglers Gorge
6. Amani, ulinzi na usalama, hakuna uvamizi wala ujambazi
7. Uwajibikaji wa viongozi kwa umma, saivi unaingia ofisi yoyote na kupata huduma bila shida, Ni rahisi kuonana na Waziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi na kuhudumiwa
8. Amedhibiti safari za nje na kuokoa fedha za kigeni
9. Amedhibiti ujangili na kukuza utalii nchini
10. Amedhibiti utoroshaji madini, kuongeza mrahaba wa madini na mapato kwa ujumla
11. Amerejesha heshima ya nchi kimataifa
NB: Zipo sababu zaidi ya 100 zinazoufanya utawala wa JPM kuwa utawala wa mfano.
 
Wameshabatizwa Ostrich Allience
🤣

Huku Tanzania members wa Ostrich Alliance wanawaza tu uchaguzi... Wanajua hata tukifa watabaki wao wachaguane...
Post ya Gerson Msigwa inafikirisha sana...
Screenshot_20200503-063850.jpg
 
Utawala wa Magufuli ni imara na wa mfano katika Afrika
1. Umeme kila kijiji kwa bei chee kupitia REA
2. Bima ya Afya na mfuko wa Afya ya jamii nchi nzima
3. Elimu bure hadi kidato cha NNE
4. Amefufua reli ya kati na reli ya Tanga, saivi ni kutekeleza SGR
5. Umeme wa uhakika nchi nzima kupitia Kinyerezi 1&2 na sasa mpango ni Stiglers Gorge
6. Amani, ulinzi na usalama, hakuna uvamizi wala ujambazi
7. Uwajibikaji wa viongozi kwa umma, saivi unaingia ofisi yoyote na kupata huduma bila shida, Ni rahisi kuonana na Waziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi na kuhudumiwa
8. Amedhibiti safari za nje na kuokoa fedha za kigeni
9. Amedhibiti ujangili na kukuza utalii nchini
10. Amedhibiti utoroshaji madini, kuongeza mrahaba wa madini na mapato kwa ujumla
11. Amerejesha heshima ya nchi kimataifa
NB: Zipo sababu zaidi ya 100 zinazoufanya utawala wa JPM kuwa utawala wa mfano.

Shukrani sana, watu wamejitoa ufahamu hawataki kusikia wala kuona, kila wakiamka alfajiri wanawahi kwenye mitandao kuponda, kukomoa na kutukana tu, hata ukijenga barabara hadi kwenye milango yao lazima wataponda tu.
Afrika tuna majitu ya ajabu sana.
 
Usiseme kila mtu kaguswa. Wanajeshi, meno, mataga, lumumba buku saba na mapolisi hawajaguswa hata kidogo. Kama wangeguswa hata kidogo (wanajeshi, meno na polisi) wangefanya mapinduzi kama aliyofanyiwa Mugabe. Kwa hiyo pambana mkuu. Cha msingi jikinge na corona.
Wameguswa Wana ndugu zao ambao wamemaliza vyuo Wana ndugu zao wafanyabiashara pia Kama nihali mbaya ya maisha Wana watu wanaowategemea, hawawezi kukwepa mzigo mkubwa wakuwasaidia wanaowategemea, hii unafanya wanachoongezewa hakina maana kwao.ili pesa unayoongezewa iwe na thamani lazima kusiwepo naongezeko lakupanda kwa gharama zamaisha.
 
Shukrani sana, watu wamejitoa ufahamu hawataki kusikia wala kuona, kila wakiamka alfajiri wanawahi kwenye mitandao kuponda, kukomoa na kutukana tu, hata ukijenga barabara hadi kwenye milango yao lazima wataponda tu.
Afrika tuna majitu ya ajabu sana.

Jamani naomba kujulishwa vyema, kwani TEA na Kinyerezi 1 & 2 vyote kaanzisha MAGUFULI? Au ndo sisi team prays and worship tunajitoa ufahamu?
 
Tupo pamoja na JPM.

Mzee mie nipo tayari kujaza nafasi ya Evod Mmanda pale Mtwara.
Utawala wa Magufuli ni imara na wa mfano katika Afrika
1. Umeme kila kijiji kwa bei chee kupitia REA
2. Bima ya Afya na mfuko wa Afya ya jamii nchi nzima
3. Elimu bure hadi kidato cha NNE
4. Amefufua reli ya kati na reli ya Tanga, saivi ni kutekeleza SGR
5. Umeme wa uhakika nchi nzima kupitia Kinyerezi 1&2 na sasa mpango ni Stiglers Gorge
6. Amani, ulinzi na usalama, hakuna uvamizi wala ujambazi
7. Uwajibikaji wa viongozi kwa umma, saivi unaingia ofisi yoyote na kupata huduma bila shida, Ni rahisi kuonana na Waziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi na kuhudumiwa
8. Amedhibiti safari za nje na kuokoa fedha za kigeni
9. Amedhibiti ujangili na kukuza utalii nchini
10. Amedhibiti utoroshaji madini, kuongeza mrahaba wa madini na mapato kwa ujumla
11. Amerejesha heshima ya nchi kimataifa
NB: Zipo sababu zaidi ya 100 zinazoufanya utawala wa JPM kuwa utawala wa mfano.

Sent using iphone pro max
 
Kila Mtu kaguswa na utawala huu, Hakuna uhuru wa habari & Utawala wa sheri, Hakuna Ajira wala motivation kwa wafanyakazi kwa miaka 5, Wafanyabiasha wanalalamika hali ngumu ya mifumo ya kodi, Mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini, Nchi kuwa na mikosi ya majanga kwa takribani miaka 5, Nchi kutawaliwa kimabavu kwa police kudhibiti watu na Ulinzi wa Rais kuongezeka.

Hakuna dalili za tume huru kuelekea uchaguzi kitu kitakachoongeza mgogoro wa kisiasa, Nchi kuwa kwenye rada za Marekani, Un na Umoja wa ulaya, Nchi kuanza kutengwa na majirani, Mwisho taifa uenda likawekewa vikwazo kama ambavyo tayari tushakosa pesa za corona kutoka IMF.

Kibaya zaidi na hatari ni washauri kuanza kuwa kimya, Wazee kunyamaza, Wananchi hasa walioenda shule na kukosa ajira kuishi kwa hasira wale wasioenda shule kuishi kwa kukata tamaa.

Na mwisho ahadi hewa mil 50 kila kijiji, ajira, uchumi, Bwawa la umeme bado, Ndege na SGR vimegubikwa na usiri mkubwa wa harufu ya ufisadi.kama haujaguswa basi malaika.

Je utawala huu unasalimika?
Wanaoabudu mwenge hawawezi kuelewa wanakuambiwa wako pa zuri
 
Usiseme kila mtu kaguswa. Wanajeshi, meno, mataga, lumumba buku saba na mapolisi hawajaguswa hata kidogo. Kama wangeguswa hata kidogo (wanajeshi, meno na polisi) wangefanya mapinduzi kama aliyofanyiwa Mugabe. Kwa hiyo pambana mkuu. Cha msingi jikinge na corona.
Umewahi kaa nao ukawasikia, wanufaika wa udhalimu ni wa juu yao,wa chini njaa kali tu.
Uoga wa wananchi ndio unaowaangusha,wamekosa pa kuanzia hawawezi anza pasipoanzishwa
 
Na Mwinjilisti Kamara Kusupa.

DALILI ya kwanza na ya wazi ya utawala ulioshindwa ni ukatili. Utawala ulioshindwa kuiendesha nchi lakini bado uko madarakani ni lazima utatawala watu kwa ukatili mkuu.

Dalili nyingine ya watawala walioshindwa kutawala lakini bado wakawako madarakani ili kusogeza siku na kuingoja rasmi siku ya kuondoka kwao, ni "uwongo". Ukiona wameanza kusema uwongo mweupe na hawawaambii watawaliwa ukweli, elewa waai kuwa si kwamba ukweli haupo bali ukweli wa kuwaambia wananchi upo isipokuwa kinachokosekana hapo ni ile Moral authority au sheria ya rohoni, kitu ambacho ni muhimu sana kwa utawala na uendeshaji wa nchi.

Sheria za nchi peke yake pasipo morali hazitoshi kufanya nchi itawalike, wala vyombo vya dola na matumizi ya mabavu havitoshi kuifanya nchi itawalike. Mfano hai ni utawala wa makaburu huko Afrika Kusini, ulikuwa na nguvu zote yaani nguvu za kiuchumi, teknolojia ya hali ya juu, nguvu za kijeshi, nguvu za polisi, pamoja na uimara wenyewe wa mfumo wa kisiasa yaani mfumo wa kibaguzi ambao ulikuwa umedumu kwa miaka mia tatu tangu ulipoasisiwa.

Lakini vyote hivyo havikutosha kuzuia wala kuhimili wimbi la mabadiliko kutoka kwa wananchi (hasa wazalendo), hapo waliposema "utawala huu sasa basi", makaburu walipiga, waliua, walitesa na kufunga watu kwenye jela zao lakini wapi, hakuna kilichowazuia wananchi wasiusukumie kaburini utawala waliouchukia na kuchoka nao.

Mtawala ukiishachokwa njia pekee iliyo bora ni kutoka madarakani kwa amani badala ya kungoja kusukmwa na hasira za wataliwa hadi mtu ang'ang'anie kubaki madarakani kwa gharama zozote.

Tukirudi kwenye dalili ya kwanza ya utawala ulioanguka hali ukingali madarakani, yaani dalili za "ukatili" dhidi ya wananchi wake inaowatawala ni wazi kwamba tunaweza kuutafsiri ukatili huo kama hatua ya mwisho ya kutapatapa ya mtawala mfanya maji ambaye analazimika kushika maji hayo hayo yanayomuua.

Wiki iliopita polisi wameupiga mabomu ya machozi mkutano wa chama cha CUF uliokuwa unafanyika pale Manzese. Kipigo hiki kimetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Afande Mahita akiwa kama mkuu wa jeshi la polisi kutoa tamko ramsi la kuwataka polisi wawe ngunguri kwa kupiga rungu mtu yeyote anayejitambulisha kama mwana ngangari. Je, ukatili wote huo ni wa nini? Na lengo lake hasa ni nini?

Jibu lake tunalipata katika historia ya hapa nchini na ya madola mengine makubwa katika dunia ambayo yalichokwa na wananchi wake, na watawala wao wakapata kiwewe na mwisho wakaamua kupambana na wananchi wao kwa kutumia nguvu zinazozidi kawaida.

Mnamo 1995 Afande Mahita akiwa Mkuu wa polisi wa Mkoa Kilimanjaro (RPC) alimsaidia mgombea wa CCM kwa kupiga mabomu mengi mikutano yote ya Mrema mkoani Kilimanjaro ili kuwatawanya washabiki lakini papo hapo kuwakomoa wananchi kwa kutoipenda CCM na kuamua kushabikia upinzani. Hatimaye baada ya Mkapa kula kiapo cha Urais, akamteua Afande Mahita kuwa Inspekta Mkuu wa Polisi yaani IGP.

Lakini tatizo liko pale pale utawala uliodumu kwa miaka yote tangu nchi ipate uhuru umechokwa na wananchi kwa sababu umefanya madhambi mengi, hauna dalili yoyote ya kutubu wala kujirekebisha, na hapo ndipo inapoanzia sera ya ukatili ya piga! Kanyaga umiza! Kisa eti hao wananchi kwanini wanasusia mikutano ya CCM (Chama tawala) na kuamua kuhudhuria kwa wingi mikutano ya chama cha upinzani cha CUF.

Nia halisi ni kutaka kuwatisha na kuwaogopesha watu kuhudhuria mikutano ya CUF. Na sababu nyingine labda ni kuwakomoa hao wananchi kwa kuwa tu wameonyesha waziwazi kwamba wanaichukia CCM na wangependa kutawaliwa na chama kingine.

Hata hivyo, hiyo gia ya ukatili anayokwenda nayo Afande Mahita siyo dawa ya kuiokoa CCM, badala yake ni kuisindikiza CCM kaburini. Nasema hivyo kutokana na kujua wazi kwamba mkutano ule uliitishwa kutokana na kujua wazi kwamba mkutano na CUF lakini wote waliohudhuria siyo CUF wengine ni wana CCM, wana TPP, na wengine hawana chama chochote bali ni wakereketwa wa maendeleo na utawala bora, ndiyo maana wanajitokeza kwa wingi kumsiliza mgombea anayetarajiwa kushinda na kuwaongoza ili waweze kuamua kumpa yule aliyeshibisha nafsi zao miongoni mwa wagombea wengi.

Sasa kosa lao ni nini hata waumizwe na mabomu? Afande Mahita asingeweza kuupiga mabomu mkutano wowote ambao unafanywa na CCM hata kungetokea fujo za kusababisha watu kufa. Tumeyaona hayo kwenye zoezi la kura za maoni za CCM ambapo watu wamekatana mapanga, wamepigana, na kutishana kwa bostola lakini polisi wakafumba macho yao na kujifanya hawaoni kwakuwa tu madhambi yanayofanyika ni ya chama tawala.

Vivyohivyo nao wazuia rushwa wakaifumbia macho rushwa ya CCM iliyotembezwa wazi wazi kwenye kura za maoni. Hii ndiyo aina ya viongozi wanaotaka kushika makali ya dola baada ya uchaguzi wa Oktoba 29..
Je, chini ya utawala wao unatarajia kupata Tanzania ya namna gani? Ukweli ni kwamba kama CCM ikishinda tutakuwa na Tanzania inayofanana na "kuzimu". Vyombo vya dola chini ya uongozi kama wa akina Mahita vitazidi kuwa butu lakini papo hapo katili sana kwa raia wema, sheria za nchi zibataki kuwa kama mapambo tu, na udhalimu utajiendesha kwa uhuru zaidi refarii wa kuuchezesha udhalimu wote atakuwa ni Bwana na Bibi rushwa.

Sasa hivi mtu anayeijia Tanzania kwa nguvu ya fedha ni sawa na ajaye na nguvu ya Mungu ambayo mambo yote yawezekana na hakuna lisilowezekana. Kwa nguvu ya fedha mtu anaweza kumnunua Afisa yeyote. Nguvu ya fedha inawezesha lolote hata kama litakuwa tendo la uhaini wa hali ya juu wa kuangamiza nchi.

Hii ni kwa sababu watu sasa wanajali maslahi ya muda mfupi na faida za papo kwa papo. Hali hii imetokana na watu kukata tamaa ya maisha na kuamua kubangaiza na neno ambalo kwa lugha nyingine linatiwa "survaival".

"Survival" ni maisha yaliyokusudiwa wanyama siyo watu. Sisi wanadamu tulikusudiwa "tuishi" yaani "life" na siyo "Survival". CCM ndiyo iliyopindua maisha ya Mtanzania na kuyateremsha chini hadi kuwa sawa na maisha ya Sungura aliyeko mbuga za wanyama ambaye kuishi kwake kunategemea ujanja wake wa porini na chenga nyingi.

Chini ya mfumo huo au mapinduzi ya aina hii, mtu mwaminifu anageuka kuwa mkosaji.

Wapo watu waaminifu ambao wametumikia serikali au mashirika ya umma kwa uaminifu hadi muda wao wa kustaafu, hawakuiba wala kuhujumu, hivi sasa wengi wao wanajuta kwa mateso wanayoyapata wala utawala hauwajali.

Chini ya hali hiyo uzalendo ni lazima ufe, na anayeua uzalendo katika nchi hii ni utawala wa CCM. Uzalendo ukisha kufa kabisa na isiwepo japo chembe ndogo tu kwa watu wachache, hapo ndipo nchi inapofanana na Sodoma na Gomora ambapo walihitajika wenye haki watano tu ili nchi isiangamizwe lakini wakakosekana.

source:
Tupo kwenye utawala mbaya sana nadhani Africa nzima tunaongoza sasa. Ni kweli kabisa utawala mbaya unakuwa na agenda za siri nyingi na hivyo hufifisha demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari. Kwa kifupi utawala huu ni hovyo mno na inabidi tufanye kitu kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
 
Back
Top Bottom