Dalili za mwanaume asiyekuwa na mapenzi ya kweli

Dalili za mwanaume asiyekuwa na mapenzi ya kweli

angelita

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Posts
3,017
Reaction score
2,446
1. Anaahadi nyingi hazitekelezeki muongo.

2. Msiri hapendi kuweka mambo yake wazi.

3. Anakutafuta akiwa na pesa kwaajili ya starehe, akiwa hana hakutafuti kabisa.

4. Hajali matatizo yako.

5. Mawasiliano sio mazuri, hana tabia yakukujulia hali mara kwa mara.

6. Hutishia kuachana mara kwa mara.

7. Hana mipango wala malengo yeyote kuhusu maisha yenu ya badaye.

8. Anapenda starehe na kujirusha na wewe akiwa na mashiko.

9. Hakutambulishi kwa ndugu zake wa karibu, na anaweza asikupeleke hata anapoishi.

10.Haonyeshi hisia zake kwako mbele za watu.

11.Anakutafuta akiwa na shida zake akimaliza wasalimie kigoma.

12.Mbinafsi anajifikiria yeye tu.
 
Duu huyo mwanamme lazima apate mwanamke wa kumshughulikia hasa hapo kwenye No, 3,8.mengine yake mwenyewe..
 
Weka na dalili za mwanamke asiye na mapenzi ya ukweli
 
1. Anaahadi nyingi hazitekelezeki muongo.
Anasema subiri kidogo, kidogo kisichofika mwisho

2. Msiri hapendi kuweka mambo yake wazi.
Mambo yake anakwambia, utajuaje kama ni yote?

3. Anakutafuta akiwa na pesa kwaajili ya starehe, akiwa hana hakutafuti kabisa.
Huwa hatoki out, out ni kwake / kwako

4. Hajali matatizo yako.
Anajali lakini kwa hasira kama vile hataki ila hana jinsi

5. Mawasiliano sio mazuri, hana tabia yakukujulia hali mara kwa mara.
Hapa ni kweli kabisa

6. Hutishia kuachana mara kwa mara.
Hasemi muachane wala muendelee yupo yupo tu.. Utasikia subiri kwanza

7. Hana mipango wala malengo yeyote kuhusu maisha yenu ya badaye.
Mipango ipo ila ni lini... Utajaza mwenyewe

8. Anapenda starehe na kujirusha na wewe akiwa na mashiko.
Hapendi starehe, hatoki toki. Akitoka ni kikazi tu

9. Hakutambulishi kwa ndugu zake wa karibu, na anaweza asikupeleke hata anapoishi.
Kwake utapafahamu, ila ndugu zake wako nje ya nchi

10.Haonyeshi hisia zake kwako mbele za watu.
Huchangamka mbele za watu ila hataki watu wajue kuna mahusiano

11.Anakutafuta akiwa na shida zake akimaliza wasalimie kigoma.
Anakutafuta mara moja kwa siku 2, just salamu tu hakuna kingine

12.Mbinafsi anajifikiria yeye tu.
Kwa 75%

Je mwanaume wa hivyo [RED COLOR] yuko katika kundi gani????
 
Weka na dalili za mwanamke asiye na mapenzi ya ukweli

1. Anaahadi nyingi hazitekelezeki muongo.

2. Msiri hapendi kuweka mambo yake wazi.

3. Anakutafuta Ukiwa na pesa kwaajili ya starehe, ukiwa huna hakutafuti kabisa.

4. Hajali matatizo yako.

5. Mawasiliano sio mazuri, hana tabia yakukujulia hali mara kwa mara.

6. Hutishia kuachana mara kwa mara.

7. Hana mipango wala malengo yeyote kuhusu maisha yenu ya badaye.

8. Anapenda starehe na kujirusha na wewe ukiwa na mshiko.

9. Hakutambulishi kwa ndugu zake wa karibu, na anaweza asikupeleke hata anapoishi.

10.Haonyeshi hisia zake kwako mbele za watu.

11.Anakutafuta akiwa na shida zake akimaliza wasalimie kigoma.

12.Mbinafsi anajifikiria yeye tu.
 
Na mwanamke anayekubali kuwa na mwanaume wa aina hii na yeye pia sio mzima wakupima akili.
 
Ngoma droo dalili zinafanana haya bhana mimi dalili zote hizo sina.
 
Ila kuna wanawake/wasichana anataka umtafute kwenye raha tu.
 
Vipi yule anayekufanyia kila kitu utakacho duniani, lakini kitu kimoja tu hafanyi---> hasemi "will you marry me". Wakati wewe kila akifungua kibox cha zawadi unadhani ni engagement ring..lol
 
Itabidi nijirekebishe kama ndo ivi
 
asante mwaya ila nishaachana nae miaka mingi sana na sasa nimeolewa na mstaarabu mno!

Ukiona mwanaume yuko ivo ujue na wewe hadhi yako ni ndogo kwake.
Wanaume tunatabia ya kupenda kutokana na class ya mwanamke ulie nae.
 
tumekutana kwenye daladala,nikachukua namba afu usiku tunatoka outing na ninakula mzigo. unategemea mapenzi ya kweli. hapo ni kutafutana Rungu ikiwa inatoa povu. una rambo,mimi nina muwa (yamoto band)
 
Back
Top Bottom