Jinsia yangu ni ME na hizi ni baadhi ya dalili KE huonesha;
Dharau
Anajibu kifupi mf. "K"
- Anakuwa busy sana mf. Anaweza akakuta missed call na asikutafute na ukipiga kimya inakuwa imeisha hiyo kihivyo
Atakereka na chochote utakachofanya hata huko nyuma alikuwa anapenda umfanyie na hata vitu vidogo vidogo ufanyavyo vitamkera pia mf: unaweza ukachukua dawa ya meno ukaiminya katikati na akakumind kwa nini umeiminya ktkt badala ya kuanza kuminyia chini kabisa na ukanuniwa siku nzima
Utapigwa vizinga non-stop na ukishindwa kuvimudu atalalamika humjali kwa hiyo humfai. N.k
Masharti yatakuwa mengi sana mf. Hupewi k bila kutimiza baadhi ya vitu anavyopenda kama simu n.k
Ushauri:
Usije ukamng'ang'ania asiyekupenda mwisho wake unakuwa sio mzuri. Chukua hamsini zako nae achue zake.
Weka akiba ya maneno
Penda kwa kiasi
Fanya mambo yako na uyape umuhimu kuliko yeye itakusaidia akiamua kusepa hutakuwa na majuto sana
Msemo wa leo:
Don't make yourself learn the hard way
Wakati ambao unajiuliza kama kweli anakupenda au anakupotezea muda hapo penzi huwa sio limekufa bali limeshazikwa. Ukiwa kwenye mahusiano ya mapenzi watu wawili mnaopendana huwa hamna kujiuliza kama kweli anakupenda, atakuambia na utaona kwa vitendo.