Dalili za Failing state

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Wachambuzi wa mambo wanafahamu dalili zote za mataifa yanayoelekea kwenye anguko. Bahati mbaya zimeanza kuonekana hapa kwetu kwa miaka sasa na viongozi wetu hakika hawajaweza kuliuona hili ama wameliona lakini hawajalielewa ama wamelielewa lakini wameamua waliache tu. Baadhi ni hizi hapa:

1. Watu kutokuwa na imani na mfumo wa kuchagua viongozi kwa njia ya kura. Nafikiri sihitaji kuweka takwimu hapa, ila tumeshuhudia kwa miaka kadhaa sasa watu hawajiandikishi kwenye kupiga kura na hata wakijiandikisha hawaendi kuchagua viongozi. Tanzania ina watu mill takriban 40 hivi au na zaidi, waliojiandikisha ni kama millioni 10 hivi nasikia. Siku ya kura utasikia walioenda kupiga ni 50%

2. Viongozi kuwakaimisha/kurithisha madaraka kwa watoto wao. Hili ni jambo lingine la hatari mno. Miaka ya hivi karibuni tumeona majina yaleyale yanajirudia kwa upya kwenye siasa za Tanzania, sihitaji kutaja majina hapa. Ni kweli ni kuwa kila mtu anao uhuru wa kuchagua au kuchaguliwa lakini nchi inayokuwa inatawaliwa na jamii ile ile kwa miaka nenda rudi hugawanyika kwa kuwa na kizazi cha watawala na watawaliwa. Pia maana nyingine ni kuwa kama hizo koo ni za kifisadi lets say basi ufisadi hauwezi kuisha, kama ni mabepari basi ubepari hauwezi kuishi. Kibaya ni kwamba unawanyima wengine wenye vipaji kuweza kuingia kwenye uongozi wa nchi yao.

3. Kuongezeka kwa pengo kati ya walionacho na wasio nacho. Miaka ya hivi karibuni makundi haya mawili yamezidi kila moja kuelekea kwenye upande wake tofauti na lingine. Matajiri wakiwaka tamaa kuwanyonya masikini zaidi na masikini wakizidi kuishi katika taabu na dhiki za kila namna.

4. Wafanyakazi kuwa tofauti na serikali. Hii ni dalili mbaya pengine kuliko nyingine zote na ni ishara muhimu sana. Chunguza nchi nyingi zilizoingia kwenye mapinduzi na migogoro, purukushani huanzia kwenye vyama vya wafanyakazi. Hawa wakiamua kutia ngumu jamii inakosa huduma kabisa, na hapa uvumilivu wa wananchi huwa unafikia kikomo. Tukumbuke kundi hili lina Polisi, wanajeshi na magereza pia.

5. Kuongezeka kwa kundi la watu wasiojua kusoma na kuandika. Inasemekana Illiteracy kwa Tanzania ni asilimia 30, sina uhakika, lakini maana yake ni kwamba nchi iankuwa na kundi kubwa la watu ambao waoni kamata twende tu, ukiwapa hela kidogo utawaona wamejaa kwenye mabasi wanaimba kwenda Jangwani, Kidongo chekundu n.k kupigia makofi ya kuwasifia watawala bila kujua wala kuchanganua wanachozungumza kina mantiki au hapana.

6. Vyombo ya habari visivyo huru. Hapa ndipo penye kimbembe kingine. Angalia kwa umakini vyombo vyetu vya habari, vingi havina umakini kwenye uchambuzi wa habari na inaonekana wazi vipo kwenye itikadi ya vyama vya siasa. Kila siku utaona habari ya kwanza ni ya mgombea fulani, hata kama yupo mikoani na wenzie wapo hapa dar, habari yake itawekwa ya kwanza na hawa wa dar watawekwa mwishoni ama katikati.

n.k, n.k

MUNGU IBARIKI TANZANIA, ILINDE TANZANIA, IONGOZE TANZANIA.
 
Ndugu yangu, haya maneno uliyosema ni mazito sana. Kipengele cha sita ni cha hatari zaidi. Huko Rwanda ambako JK anatolea mfano, katika kesi nyingi zinazoendelea za kimbari, waandishi wa habari ni kundi linalosakamwa. Na mimi naamini kwa dhati kuwa kama kutakuwa na vita nchini kwetu, vitasababishwa na waandishi wa habari wasiosema ukweli wa mambo. Mathalani:-
-IPPMEDIA, walitangaza na kujipambanua kuwa ni wapiganaji wa ufisadi nchini. Edward Lowassa na Rostam wakamwendea Mzee Mengi kumsihi aache hiyo vita akakataa. Leo hii, media yake inaongoza kwa kutetea ufisadi na kuficha ukweli wa wanaopambana na ufisadi. Kwa nini siku moja, watu wasichukue mawe na kupambana naye? Kwangu mimi, mafisadi ni nafuu kuliko watetezi wao ambao ni vyombo vya habari. Damu na laana ya watanzania ivishukie vyombo vyote vinavyotukuza ufisadi na mafisadi.
 
Back
Top Bottom