Dalili kumi za kukujulisha kuwa umeshika mimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili kumi za kukujulisha kuwa umeshika mimba

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mimba.jpg


  Hutokea mara nyingi kina mama na wasichana kuwa na kipindi cha msongo wa mawazo pale wanapokosa siku zao na hasa kama hawakutumia njia ya uzazi wa mpango au kinga nyingine ya kushika mimba.

  Kukosa siku zako sio dalili pekee ya kushika mimba, bali kuna dalili zingine utalazoziona. Kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza kukufanya ukose siku zako, hivyo soma dalili za mimba ili ikusaidie kupata uhakika.

  Moja, ni mabadiliko katika siku zako. Hii kitaalamu tunaita spotting. Unaweza kushika mimba ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza kwenye kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa kwenye ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo amabazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango na siku za damu hubadilika.

  Pili, ni kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa. Hii inasababishwa na ongezeko la homoni za istrogen pale unapokuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

  Tatu, ni kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapoToka kulala. Hii ni kwa sababu ya homoni ya ‘projestroni’ ambayo husababisha kupungua nguvu kwa misuli ya mrija wa chakula au koromeo.

  Nne, ni uchovu usiokuwa na usingizi usiokuwa na sababu. Hii hutokea kwa sababu ya ongezeko la homoni ya ‘projestroni’ na mama utajikuta unasinzia mara kwa mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba ila hata kipindi cha mwisho wa mimba hujisikia uchovu.

  Tano, kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hasa kama unapata mimba kwa mara ya kwanza, utachukia harufu za vyukula na vinywaji mabalimbali. Wakati mwingine hata harufu za watu walio karibu nawe zinaweza kukukera.

  Sita, ni kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi hasa sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinazokufanya kijisikia tumbo kujaa.

  Saba, Kukojoa mara kwa mara. Hii kwanza hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa rishe ya kutosha kwako na kwa kiumbe tumboni. Ukiwa na damu nyingi pia utakojoa sana za kikemia mwilini. Pili utajisikia kwenda haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitakapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

  Nane, kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa kina mama ambao hupima joto lao kama njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfurulizo.

  Tisa, kutoona siku sako kabisa. Kwa wale ambao siku zao hazibadiliki na huenda vizuri yawezekana kugundua pale wanapokose siku nap engine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona kawaida ila kama ameshika mimba taona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu na kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

  Kumi, kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Famasi nyingi huuza vipimo ambavyo ikikichovya kwenye mjojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo.

  Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani hata kazini. Kipimo hiki ukisha kichovya kwenye mkoja kama katatsi inavyoelekea utaona mistali baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini.

  Ikitokea mistari miwili basi unaweza kuwa na mimba na ukitokea mmoja utakuwa huna mimba. Kilingana na kiwango cha homoni mwilini, kuna kina mama hakionyeshi majibu mpaka upitishe wiki moja bila kuona siku zako.

  Pamoja na dalili hapo juu, unatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  ahsante sana Mzizimkavu!
   
 3. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  asante sana mzizi mkavu
   
 4. K

  Kafuta Senior Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwenye namba tatu hapo.nini kifanyike ili kukabiliana na hali hiyo..au kuindosha kabisa..kama kuna dawa labda na mambo yanaofanana kama hivyo.
   
 5. K

  Kafuta Senior Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwenye namba tatu hapo.nini kifanyike ili kukabiliana na hali hiyo..au kuindosha kabisa..kama kuna dawa labda na mambo yanaofanana kama hivyo.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Tumia juisi ya Tangawizi kwa namba tatu.
   
 7. muhomakilo jr

  muhomakilo jr JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2013
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 10,121
  Likes Received: 3,222
  Trophy Points: 280
  safi mzizi nimekupata.
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2013
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hapo no mbili bana sijui kama ni kweli maana wengine siku za ovulation matiti huvimba na kuongezeka..sasa nitatofautishaje hii ni mimba na hii ni yai !
   
 9. Chocs

  Chocs JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2013
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 8,202
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. f

  frog New Member

  #10
  Jan 15, 2014
  Joined: Jan 14, 2014
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :majani7:
  Ahsante sana mzizi
   
 11. f

  frog New Member

  #11
  Jan 15, 2014
  Joined: Jan 14, 2014
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nmekupata mzizimkavu
  :majani7:
   
 12. ilu

  ilu JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2015
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 809
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80

  MziziMkavu naitengenezaje juice ya Tangawizi? Nachanganya na tunda au peke yake?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. tomjelly

  tomjelly JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2015
  Joined: Jul 29, 2013
  Messages: 562
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  thanks mkuu
   
 14. kubwalamaadui

  kubwalamaadui JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2015
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mi mdomo mchungu tu na pia back pain mara moja moja
   
 15. C

  Chrspina Chris New Member

  #15
  Jun 10, 2016
  Joined: Jun 1, 2016
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hi
   
 16. decomm

  decomm JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2016
  Joined: Dec 10, 2013
  Messages: 451
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  There are few good men, you are! Ahsante kwa post nzuri nzuri mara kwa mara.
   
 17. o

  odera Member

  #17
  Aug 3, 2016
  Joined: Apr 8, 2016
  Messages: 10
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  inawezekana MTU akawa anapata siku zake alafu akawa mjamzito? na kwa nn mwanamke tumbo linakuwa kubwa?
   
 18. m

  mwalisa jr Member

  #18
  Aug 4, 2016
  Joined: Aug 18, 2015
  Messages: 50
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
  Mchumba wangu alipitisha siku tano, lkn siku ya sita asubuhi aliona kidogo damu lkn ikakata mpaka Leo hii, but Mara nyingi sana analala na kula sana, lkn dalili hiz zingine zinajitokeza na kupotea na kwa kiwango kidogo, je anaweza kuwa anaujauzito?
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mpeleke akapime ili uthibishe kama ameshika mimba usikisie tu
   
 20. Uni mwanitu

  Uni mwanitu Senior Member

  #20
  Feb 26, 2017
  Joined: Oct 25, 2014
  Messages: 182
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mtu anaweza akawa na Mimba na akapata hedhi.? Hasa kwa Hawa ambao siku zao zinabadilika kila mara.?
   
Loading...