Daladala zagoma baada ya Sumatra kushusha nauli

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
BAADHI ya daladala katika jiji la Dar es Salaam zimegoma kuendelea kubeba abiria kutokana na Sumatra kushusha bei za nauli.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Nifahamishe baadhi ya madereva ambao walionekana kuegesha magari yao pembeni na kutochukua abiria walisema hawapakii abiria hadi abiria wakiri kuwa wataendelea kulipa nauli ya awali.

Akizungumza kwa jazba mmoja wa dereva wa ruti inayofanya safari yake kati ya Msasani na Ubungo aliyejitambulisha kwa jina la Sekion John alisema magari yote yanayofanya ruti hiyo wamekutana kwa pamoja na wamekubaliana hakuna kufanya kazi kwa kuwa Sumatra imefanya kitu cha ajabu cha kupunguza nauli bila kuzingatia gharama za uendeshaji.

Alisema wamesikitishwa na kitendo cha Mamlaka hiyo kupunguza nauli bila kuzingatia umbali wa ruti hiyo na kudai kuwa kama wataendelea na bei iliyoshushwa basi watakuwa wakifanya kazi kihasara.

Nayo magari yanayofanya ruti kati ya Mwenge na Mikoroshini yaligoma na kuegesha magari pembeni huku abiria wakibaki hawana la kufanya kutokana na uamuzi uliochukuliwa na madereva hao.

Nifahamishe ilibahatika kuonana na kiongozi wa madereva hao Frank Willium aliyekuwa anaendesha gari ya abiria yenye namba za usajili T 545 ADZ na kusema kuwa Sumatra imeamua kushusha nauli bila kuwajali na kuangalia umbali wa njia wanayotumia.

Alisema ruti yao ni ndefu na inachukua kama kilomita 14 kati ya Mikoroshini na Mwenge tofauti na njia nyingine nyingi zinazotembea kilomita 10 ka ruti.

Aliongeza kuwa kama nauli hizo hazitarudishwa kama awali kwa ruti yao basi wataendelea kupaki magari pembeni na watafanya safari zao pale tu abiria watakaoridhia kulipa nauli ya awali watakapopatikana.

Source: Nifahamishe.com
 
Back
Top Bottom