Daladala na trafiki: Buguruni-kwanyerere

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
Hivi mkuu wa Trafiki tuseme ndiyo hajui kinachotokea siku za Jumatatu kila wiki, mara 52 kwa mwaka katika barabara ya Buguruni-Kwa Nyerere?

Invyoelekea usalama au uchafuzi barabarani katika barabara hiyo wameamua hii ndio siku ya kuwakamua madereva na makonda wa daladala.

Kwa hiyo daladala hizo kwa kutambua hili na kuona serikali imelala na haiwashughulukii wachawi wao zimeamua kutokuganya kazi siku hiyo isipokuwa kwa chache ambayo inayumkinika ni za maaskari wenyewe au za jamaa wa maaskari.

Matokeo yake ni kwamba:
. Wagonjwa barabara hiyo wanaoelekea hospitali za Amana, Magomeni, Mwananyamala na kadhalika wanateseka kupita kiasi,
. Wafanyakazi mbalimbali wanachelewa kazini.
. Walimu wanachelewa madarasani,
Madaktari, manesi na wafanyakazi wengine wa hosopitali wanachelewa mahospitalini,
. Maelfu ya wanafunzi wanachelewa shule,
. mamia ya wafanyabiashara wanaingia hasara kutokana na kuchelewa kuwahi masokoni, migahawani na magengeni na wengine hasara kutokana na kuoza kwa bidhaa zao njiani,


Kwa hakika haya ndiyo maudhi mwananchi wa kawaida anayetumia barabara ya Buguruni-Kwanyerere anayopata kila Jumatatu hapa jiijini.

Ni vyema mkuu wa trafiki na wizara husika ikalishughulikia jambo hili kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Wameamua hii iwe siku ya kuwakamua kivipi mkubwa? sijakupata vizuri, kwani kuna nini huko hebu tuelezee tuelewe
 
Unajua unapotaka kuleta hoja lazima iwe imekamilika ili tujue cha kuchangia, sasa hii story mimi binafsi sielewi imeanzia wapi, nimejaribu kuangalia labla kabla ya IGA kutoa hayo maoni kuna mtu kaelezea vizuri sijaona, huyu ni aliyeanzisha thread siajona. Hebu weka maelezo kabla ya wewe kutoa mchango wako kwanza ili tuelewe what's behind the scene.
 
Back
Top Bottom