Daladala Mbeya zagoma, abiria wasota

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Madereva wa daladala wa jijini Mbeya leo Jumatatu Machi 18, 2019 wamegoma kutoa huduma ya usafiri kwa shinikizo la kutaka Bajaji zisipite barabara kuu.

Mwananchi imefika kituo cha Uyole na Makasin na kushuhudia umati wa watu waliokwama kutokana na kukosekana usafiri huo.

Hata hivyo, usafiri ambao unatumika kwa sasa ni bodaboda, gari ndogo za kubeba mizigo maarufu ‘kirikuu’, bajaji pamoja na Noah.

Baada mgomo huo Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani limefika kwenye vituo kutoa msaada kwa wanafunzi kwa kusimamisha mabasi yanayotoka Kyela na Iringa ili kuwasafirisha wanafunzi kwa gharama ya Sh200.

Kwa mujibu wa Issa Kinyunyu dereva wa daladala za Nsalaga/ Stend kuu amesema wataendelea na huduma ya usafirishaji baada ya kukaa kikao na Mkuu wa Mkoa katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.

-Mwananchi
 
Secta ya usafirishaji inapitia changamoto kubwa sana kwa sasa hususani baada ya Noah, boda boda na bajaji kuanza kutumika
 
Watulie tu, wenzao Dar Machinga wameruhusiwa kupanga bidhaa hadi milangoni mwa maduka na wasibugudhiwe.

Halafu hao bajaji wanavitambusho vya Rais, hivyo wameruhusiwa kufanyia biashara zao popote pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli bajaji mbeya imeathiri sana daladala zimezimisha baadhi ya route kama S/KUU - ISYESYE & S/KUU to ITUWA boda boda hawajachwa salama sikwambii Taxi yani hawa madereva wa Tax ndio hawataki kabisa kuona bajaj imefikia hatua kwenye maegesho ya hospital kama RUFAA na META ikikutwa bajaj inapigwa faini aisee vijana wananyang'anyana tonge

Haswaa daladala pale ilomba kwenda isyesye zimehodhiwa na bajaji ilemi ndio haswaaa
Kule ituha route ya daladala sio ya mda mrefu Sana lkn hailipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom