Daktari wa maradhi ya moyo Mtanzania atambuliwa Marekani

kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,092
2,128
Daktari mshauri mwandamizi wa magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro, nchini Tanzania amepewa tuzo na Chuo Kikuu cha Magonjwa ya Moyo Marekani (American college of Cardiology).

Dkt Harun Emalda Nyagori ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis, amepewa tuzo ya kutambuliwa kwa utafiti na uzoefu wake katika ushauri kuhusu magonjwa ya moyo barani Afrika.

Baadhi ya utafiti uliofanywa na Dkt Nyagori ni pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa dawa za maradhi ya moyo nchini Tanzania na changamoto za magonjwa ya moyo nchini humo.

Tuzo nyingine alizopata ni kutoka kwa Jumuiya ya madaktari bingwa wa maradhi ya moyo barani Ulaya na Jumuiya ya Umoja wa Madaktari bingwa wa maradhi ta moyo nchini Mexico.

Dkt Nyagori ni kati ya madaktari bingwa wachache nchini Tanzania wanaoshauri na kutibu maradhi ya moyo yasiyohusiana na upasuaji.

Amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka saba sasa akiwasaidia wangonjwa katika mkoa wa Morogoro na mikoa jirani inayopakana na Morogoro.

Dkt. Nyagori pia aliwahi kupokea tuzo nyingine. Septemba 2015 alipokea tuzo kutoka Jumuiya ya Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo Barani Ulaya, London.

Tuzo nyingine ni kutoka Jumuiya ya Umoja wa madaktari bingwa wa maradhi ya Moyo nchini Mexico mwaka 2016.

Kwa kushirikiana na madaktari wengine, Dkt Nyagori amekuwa akiwatibu kwa wastani wagonjwa 40 hadi 60 kwa siku.

Idadi inayofikia wastani wa wagonjwa 160 - 200 kwa wiki.

Daktari wa maradhi ya moyo Mtanzania atambuliwa Marekani - BBC Swahili
 
kilam huyu Dr ana kashfa, kutokana na maelezo ya madaktari wenzie hana sifa za kuwa cardiologist, hizi short courses si sifa ya kutosha kukufanya cardiologist bila ya kufanya Masters ya hiyo kitu.

Ila si haba jamaa huko Moro amejenga hospitali nzima na ina vifaa vya kutosha hadi CT -scan, kwa ufupi jamaa ni mjasiriamali mzuri ila hana reputation nzuri mbele ya madaktari wa Tz.
 
Utakuwa na ujasiri wa hali ya chini kabisa kuamini maneno hayo. Hao wote waiotambua uwezo wake na kumzawadia hawamjui??? Tafiti zilizomtambulisha duniani je hazikukidhi vigezo? HUsda tu hapo hamna kingine.
 
Umezaliwa 1989?
 
BabM hayo ni maneno ya wataalamu wenzie, wao wanaamini cardiologist ni ambaye amesomea Masters kabisa na sio short courses, je wewe unaamini mtu anaweza fanya short courses tu na kuwa Cardiologist ?
 
Sasa kama ni Daktari wa Tanzania kwa nini huu uzi uko kwenye JUKWAA LA KENYA??????!!!!!!
 
kilam huyu Dr ana kashfa, kutokana na maelezo ya madaktari wenzie hana sifa za kuwa cardiologist, hizi short courses si sifa ya kutosha kukufanya cardiologist bila ya kufanya Masters ya hiyo kitu.

Ila si haba jamaa huko Moro amejenga hospitali nzima na ina vifaa vya kutosha hadi CT -scan, kwa ufupi jamaa ni mjasiriamali mzuri ila hana reputation nzuri mbele ya madaktari wa Tz.

Mkuu hizo unazoziita short course amezifanya au amegushi vyeti? Kama amesoma na ameweza kufanya tafiti zilizokubaliwa sio tu na madaktari wengine wasomi bali na taasis kubwa zinazoshughulika na magonjwa ya moyo. Kwangu na muona ana uwezo wa kipekee na anamchango mkubwa sana kwa jamii.

Unaposema madaktari wenzake wanatofautiana nae unamaanisha akina nani? Na wamefanya nini cha kuonyesha tofauti kwa kutumia Masters zo? Kwangu cha muhimu kabisa, ni unaweza kufanya kitu gani kwa elimu yako na sio kuwa na elimu usiyoitumia.
 
kilam huyu Dr ana kashfa, kutokana na maelezo ya madaktari wenzie hana sifa za kuwa cardiologist, hizi short courses si sifa ya kutosha kukufanya cardiologist bila ya kufanya Masters ya hiyo kitu.

Ila si haba jamaa huko Moro amejenga hospitali nzima na ina vifaa vya kutosha hadi CT -scan, kwa ufupi jamaa ni mjasiriamali mzuri ila hana reputation nzuri mbele ya madaktari wa Tz.

Nilidhani hana sifa labda hana ufanisi katika utaalamu wa moyo kumbe majungu tu ya wenzake. Matokeo chanya kwenye kazi ni zaidi ya masters au Phd isiyo na tija. Tukumbuke tu, cardiologist wa mwanzo kabisa hakuwa na degree yoyote zaidi ya kipaji cha kuzaliwa.
 
Back
Top Bottom