kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,686
Ugonjwa huu ni uvimbe unaotokea shingoni na hufahamika kwa kitalaamu kama cervical/neck lympadenopathy .
Uvimbe huu unapozidi sentimita moja, tezi hizi hugawanywa katika makundi matatu; tezi moja au fungu moja, yaani tezi zilizovimba sehemu moja, tezi zilizosambaa (generalized) sehemu mbalimbali na tezi zitokanazo na ngozi ya shingo (dermatopathic ).
Pia tezi hizi hugawanywa kulingana na muda kama vile tezi za muda mfupi tangu kutokea (acute).
Hizi hutokea ndani ya wiki mbili, tezi za muda wa kati (subacute) zilizo ndani ya wiki mbili hadi sita na tezi za muda mrefu (chronic) yaani zaidi ya wiki sita.
Makundi matatu makubwa ya magonjwa husababisha tatizo hili na ndiyo dalili mojawapo ya kuwepo kwa magonjwa hayo katika mwili.
Kundi la kwanza ni magonjwa ya kuambukiza (infections), kwa mfano maambukizi mdomoni, puani, masikioni, kwenye njia ya chakula au koromeo.
Kwa kawaida maambukizi husababisha matezi kuvimba kwa watoto zaidi kuliko kwa watu wazima. Ugonjwa mkubwa katika kundi hili ni TB ya matezi, hili halichagui umri wala jinsia. Kuudi la pili ni kinga za mwili kushambulia sehemu ya mwili wake (auto-immune diseases) na kundi la tatu ni saratani.
Saratani ya damu kwa mfano au ya tezi yenyewe au ya ngozi au ya viungo vilivyopo shingoni au kichwani huleta kuvimba kwa tezi, ifahamike pia kwamba saratani kutoka sehemu nyingine ya mwili kwa mfano tumboni au kifuani huweza kutembea na kuja kujitokeza katika tezi za shingo na kusababisha kuvimba. Hii huashiria kwamba tayari saratani imesambaa.
Ni muhimu kwa mgonjwa kwenda kwa daktari au hospitali kuweza kupata matibabu bila kupuuzia, hasa kwa matezi ya muda mrefu yasiyokwisha, matezi yanayoongezeka ukubwa kwa kasi na yale yasiyoambatana na maumivu kwa kupitia vipimo ni rahisi kujua chanzo cha tatizo na mgonjwa kuanza matibabu bila kuchelewa.
http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Kuvimba-kwa-tezi-za-shingo/-/1597592/1876960/-/75jv6nz/-/index.html