Daktari akamatwa kwa kutibu Wagonjwa Nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Jeshi la Polisi wilaya ya Tandaimba mkoani Mtwara linamshikilia Daktari Karim Bakari kutoka kijiji cha Maheha kwa kosa la kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa nyumbani kwake kinyume na taratibu na sheria inayosimamia sekta ya afya nchini.

Mkuu wa wilaya ya Tandaimba Kanali Patick Sawala ambaye ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya imefanikiwa kubaini na kumkamata daktari huyo ambaye si mwajiriwa.

Amesema kukamatwa kwa daktari huyo kumetokana na uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wananchi na kulitaka jeshi la polisi wilayani humo kufatilia ni wapi alikuwa anapata dawa na vifaa tiba hivyo.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Tandahimba Daktari Silas Sembiko amesema daktari huyo alifukuzwa kazi mwaka jana katika hospitali ya wilaya ya Newala kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.

Hata hivyo amewataka wananchi kuacha tabia ya kupata huduma za afya vichochoroni kwa madai ni hatari kwa afya zao na kuwa tayari kutoa ushirikiano mara wanapobaini kuwapo kwa matibabu ya aina hiyo.

Akijitetea daktari huyo amesema aliamua kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao na kuomba serikali imsamehe.

ITV
 
Madaktari wamekua wengi mtaani na ajira hamna.

Utakuta wagonjwa wengi wanamkubali vibaya mno huyo daktari kutokana na ufanisi wake katika kuwahudumia.

Hapo daktari tatizo linalomsumbua ni umaskini tu wa kukosa mtaji wa kufungua dispensary yake.
 
ASAMEHWE NA ARUDISHWE KAZINI. KWANI BADO ANAIPENDA KAZI YAKE. HUYO NI LULU, TUENDELEE KUITUMIA TAALUMA YAKE. TAIFA LINA UHABA WA MADAKTARI.
 
Mimi mwenyewe niko huku bariadi ninawatibu wanyantuzu mtaani....ni juzi tu nimenunua set nzima ya vifaa vya kutolea meno akipatikana mgonjwa namhudumia vizuri.......siku mkinikamata kama dr bakari sijui mtanila wiiti ?..
 
Hapo wamefeli.

Ni kama mwalimu kuanzisha tuisheni tu, sio lazima mtu aende.
 
Ukute ni njama tuza kumharibia,kule Ngara kuna mganga mmoja wa Kituo Cha Afya kuna wakati huwa anawatolea meno watu nyumbani kwake.

Mimi mwenyewe niliwahi kumpeleka binti yangu wa kazi ili amng'oe jino na alimng'oa fresh tu.ilikuwa hivyo kwasababu kuna wakati anakuwa off na watu wanamuamini.
 
Wivu tuu Kama wanazego bado wanmfuata ninyi kinawauma nini Sasa.

Huduma isipo fuata wahusika ,wahusika watafuata huduma
 
Haya ni maisha tu, mtaani au huko hospital zote ni biashara tu, mimba itolewe hospital au mtaani kote huko ni kutoa mimba tu, hata uzinzi ufanyike guest au porini wote ni uzinzi tu. Cha msingi usalama uzingatiwe.

Tusipangiane kazi za kufanya
 
Tatizo la wizara ya afya huwa haina control ya rasilimali watu katika secta zote za serikali na binafsi.

Ikumbukwe kuwa wateja wa huduma za afya ambazo ni muhimu sana ni wananchi wote bila kujali ni sekta ya serikali au binafsi

Imetokea mara nyingi, madaktari na watoa huduma za afya wanspotumbuliwa serikalini kwa sababu za kimaadili, abuse of proportional na wengine kutokuwa na sifa za kitaaluma kama wale wa VYETI VYA MAGUMASHI wanakwenda kuajiriwa kwenye hospitali binafsi na kuendelea kutoa huduma za Afya wakati serikali imekwishaona hawafai kutoa huduma za afya sekta binafsi zinasimamiwa na sheria gani?
 
Back
Top Bottom