Daktari ajinyonga na kufa ndani ya gesti huko morogoro

Daktari ajinyonga na kufa ndani ya gesti huko morogoro

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,742
[h=3]DAKTARI AJINYONGA NA KUFA NDANI YA GESTI HUKO MOROGORO[/h]


DAKTARI wa meno Anorld Rimo (umri wa miaka kati ya 30 hadi 40) wa hospitali ya Sabasaba manispaa ya Morogoro, amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya Camel iliopo Kihonda.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 10 alfajiri katika


nyumba hiyo ya kulala wageni.

Alisema Daktari huyo alikuwa amepanga katika nyumba hiyo katika chumba namba 2, na kukutwa amejinyongea dirishani kwa kutumia foronya za mto pamoja na taulo.

Ameeleza kuwa usiku wa kuamikia siku hiyo marehemu alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo na kufanya fujo na kuonesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi kazi.

Kamanda huyo alisema marahemu alikuwa peke yake katika chumba hicho na haikufahamika mara moja anaishi wapi.

Chanzo cha kujinyonga hakijajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi.

---
Latifa Ganzel, Morogoro


DAKTARI AJINYONGA NA KUFA NDANI YA GESTI HUKO MOROGORO - MPEKUZI HURU
 
Jamaa kikojoleo kimegoma kufanya kazi kaamua kujitoa uhai...mbona hakuwa na kipimio au alitestia revolla...r i unapostahili dakitari
 
Jamaa namfahamu jamani kafunga ndoa majuzi tu!
Ni kweli mkuu, Marehemu Dr. Lyimo alifunga ndoa February mwaka huu. Binafsi nilishiriki kwenye maandalizi hadi siku ya harusi. Alimuoa Nesi ambaye ni Mchaga mwenzake ambaye anafanyakazi huko Moshi, baada ya kuachana na mpenzi wake wa awali. Inasemekana kabla ya kujiua alienda kuwakabidhi Masista funguo ya nyumba yake iliyopo Kihonda-Mazimbu road pamoja na vitu vyake muhimu. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Moshi kwa mazishi.
 
Wenye mishahara mikubwa nao wanajinyonga?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 


Saturday, May 25, 2013 | 11:03 PM


DAKTARI wa meno wa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro, Alnord Limo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amefariki dunia kwenye chumba cha gesti huku habari zikidai alijinyonga kwa shuka.

Mkasa huo ulimfika daktari huyo Jumatano iliyopita kwenye nyumba ya kulala wageni ya Camel iliyopo Kihonda, kandokando ya barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.
Mhudumu wa gesti hiyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, kwa kuwa si msemaji mkuu wa kazini kwake, alidai siku ya tukio marehemu alifika kwenye gesti hiyo na kukodi chumba namba 2 ambapo walimchukulia kama mteja wa kawaida.

”Alikuja na kuomba chumba, tukampa namba mbili. Aliingia akiwa peke yake, lakini baada ya muda alitoka na kuja mapokezi, sijui alikuwa na shida gani, halafu akarudi tena ndani,”

alisema mhudumu huyo.

Aliongeza kuwa asubuhi walipoona hatoki na muda wa kuondoka ulifika, ndipo walipoingiwa na wasiwasi na kwenda kufungua ambapo walimkuta amekufa.

Habari za ndani zaidi zilidai kwamba, daktari huyo alifunga ndoa miezi mitatu iliyopita na kwamba siku ya tukio mkewe alikuwa safarini.

Inadaiwa siku moja kabla ya tukio hilo alikusanya nguo zake na simu ya mkononi na kupeleka kwenye kambi ya kulea watoto yatima ya Mgolole iliyopo mjini hapa.



doktaajinyonga.jpg


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alipohojiwa na mwandishi wetu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote.



Read more: MKASA: DAKTARI AJINYONGA KWA KUTUMIA SHUKA AKIWA KWENYE GESTI BUBU HUKO MOROGORO...!! - GUMZO LA JIJI
 
Hivi karibuni wachaga wameiga sana mtindo wetu wahehe wa kujiua sijui ni kwa nini hasa
 
Back
Top Bottom