Haloo wa JF,
Nina rafiki yangu ana gf wake, huyu mdada mie nashindwa kumwelewa kabisa.
kipindi wanaanzana mimi nlichangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha zoezi zima la kuwaunganisha na baada ya hapo nlikua msuluhishi mkubwa wa migogoro yao.
Jamaa anafanya kazi ya kusafiri safiri.
siku moja jamaa akiwa safari demu alikuja kwangu jioni nlikua ndio nimetoka job, ile nimefika nae ndio akaja. Ilikua kwenye saa mbili kasoro hivi, basi akaniambia kaja kupiga story na pia kula kwangu kwani hajiskiii kupika kwake.
Haikua ajabu kwa jambo kama hili kwani hata jamaa huwa anakujaga nae kwangu na wanakula then tunapiga story na kucheki movie baadae nawasindikiza so huwa ni kawaida.
Basi baada ya kula mda ukawa umeenda nkamwambie nimsindikize then nkamsindikiza but akaniambia taa yake inasumbua (tube light) so nkamsaidie kucheki.
Nikafika mpaka kwake nkaichek then nkatafanikiwa kuiweka sawa. Muda ulikua umeenda sana kama saa sita fulani usiku, so shem akanambia nilale tu, kwani yuko mwenyewe.
Mie nikakataa but akanilazimisha sana baaadae nkaona poa.kiukweli hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya mapenzi.
Jamaa alikua na chumba kimoja so ikabidi tulale na shem kitanda kimoja, but nlilala na suruali yangu na vest, mie ndio nlikuwa wa kwanza kulala yeye alikua anafanya kazi zake.
Bahati mbaya/nzuri nlipitiwa na kausingizi then nkashtuka aliponiamsha usiku na kunambia hana usingizi.
kutupa jicho, alivaa night dress transparent yaani nliona kufuli jeupe fyema kabisa.
Net work ilikata ghafla na shetani mchafu akaniiingia. but nilijikaza kiume na nikamwambia mimi nimechoka so tulale tu, Dah from that time sikupata usingizi, mpaka kunakucha nae pia hakulala kwani alijigeuza geuza mradi tu aniguse.
Asubuhi sana nilitoka na kurudi kwangu, kumbe kuna kijana jirani aliniona nkiiingia na nkitoka asubuhi, siakafikisha taarifa kwa mshkaji....jamaa alivyokuja akagombana sana na shem na kudai katembea na mimi, dah....UKWELI NINAO MIMI NA SHEM.. HAKUNA MTU ALIYETUAMINI. Jamaa hakuniuliza but alinichunia na kuanza kulewa kila siku, shem alinambia kila kitu. Mahusiano yao yakawa na matatizo.
Baada ya kuona mambo yanaenda vibaya nikamfuata mshikaji na kumueleza kila kitu jamaa hakuniamini but hakunifanya kitu.
Baada ya mambo kuwa mabaya zaidi shem akaamua kutoroka na vitu vyote vya ndani wakati jamaa hayupo.
Ila shem hakunambia huo mpango wake.
Baada ya jamaa kurudi akafikia kwangu na kuniambia alimpa mtaji shem ili afanye biashara so hajarudi yuko mkoa kapeleka bidhaa.
Jamaa akaka kwangu kama siku tatu then nkamuuliza kwanini usimwombe akutumie key, jamaa akampigia simu shem na kumuomba atume funguo, kumbe funguo shem aliacha dukani then jamaa kwenda kufungua mlango ndio akakuta chumba cheupeee. Akanipigia simu na kuniuliza kama shem alinambia chochote, mie sikua najua but jamaa hakuniamini akadhani mie nimemzunguka.
Mungu si athumani jamaa akaendelea na kazi akanunua kitanda na vitu vngine, baaada ya shem kuona mambo yanamwendea poa jamaaa, nkashangaa siku moja namkuta shem kwa jamaa wamerudiana? Nlimshangaa sana mshkaji.
But sikutia neno.
But shem huwa haongei na mimi but jamaa anaongea na mimi vyema.