Dah,kama utani ila niuhalisi jamani

Dah,kama utani ila niuhalisi jamani

mkuu naona kama umetumia neno kubwa sana unaposema unampenda sana wakati no strings attached. Hapo hasa ndio panaponipa mashaka kwani nijuavyo mimi love ni 2 way traffic sasa hii ya kupenda kwa imani mmmh. Pengine unataka kusema huyo dada anakuvutia zaidi kuliko huyo wa 2 sasa unachoweza kufanya kwanza tafuta namna ya kuongea na huyo unayeona anakufaa ili uweze kusikia toka kinywani mwake yeye anasemaje juu yako. Funguka mkuu huenda na yeye anakutamani . Kama utapata jibu la hapana usijilaumu kwani mungu anajua kipi bora kwako huenda
wewe unamuona kwa nje huyo mdada anakufaa kumbe hapana jua kuwa mungu huona vyote nafsi mwili na roho.
Huyo wa 2 kama hujisikii chochote juu yake ni heri ukamuachilia kwani hatuoani kwa kuhurumiana kumbuka ndoa haivunjiki kirahisi hasa kwetu sisi wakristu ukioa/kuolewa ndio imetoka. Hivyo yakupasa ufanye uchaguzi wako kwa makini na ikiwezekana umshirikishe mungu . Kumbuka maisha ya ndoa yana picha yake tofauti kabisa na ambavyo huwa tunayaona tuwapo vijana/ single . Ili ndoa iwe nzuri ni bora ukaingia huko na mtu mnayependana kwa dhati otherwise utajikuta umeingia chama cha walalamishi na ukahisi ndoa ziko hivyo.

asante mkuu kwa ushauri. Hakika nitapita katika mtihani huu wa maisha ambao kila kijana hupitia.
 
Back
Top Bottom