Nahitaji dagaa wasio na mchanga kutoka Musoma. Kwa wenye kuelewa nngependa kujua bei ya gunia na gharama za usafiri kutoka Musoma hadi Arusha. Kwa ambao wapo kwenye biashara ya hawa dagaa naomba kujua faida kwa gunia nzima.
Naomba kuwasilisha...naombeni ushirikiano wenu
Kiujumla hali iko hivi.
Dagaa ya Binadam bei yake ni Tsh 12,000.00 mpaka 20,000.00 Kwa Bei ya Porini wanakopatikana na wanauza kwa kutumia kipimo cha dumu la lita 20 kwa bei hiyo.
Sokoni Dagaa wa chakula cha Binadam anauzwa Tsh 38,00.00 mpaka 5,000.00 kwa kilo. Inategemeana ubora wa dagaa , wakati husika na upatikanaji wake kwa wakati huo.
Usafiri kusafirisha Gunia la Dagaa kutoka Musoma mpaka Dar au Arusha ni Tsh 65,00.00 mpaka 75,00.00 bei kama hiyo ni Rafiki hata kwa mwanza inategemea maelewano yenu na Wenye Gari husika.
Gharama zingine ni kama vile ;-
1. Mfuko
2. Ushuru
3.Ushonaji
4.Upakiaji
5.N.k
N.B katika Gharama suala la kubana matumizi linahusika pia ili kupungza pesa zisiende sana.
Ifikie Tsh 14,200.00 tu kwa Gunia lenye Dumu ishirini au kumi na nane, na lenye kukadiriwa kufikisha kilo 90+.
Hivo basi kimahesabu ni kama hivi...
18×12000= 216000.Gunia zima
14200+216000=230200
230200 hizi ndo mtaji mzima wa Gunia zima.
Kumbka Gunia moja linakua na dumu zipatazo 18 au 20 na zinakadiriwa kuwa na uzito wa kilo 90+ hivo basi 90×3800=342000.
Mtaji ni wa gunia ni Tsh 230200.
342000.00-230200.00=111800.00
Hii ni faida 111800.000
Lakini bei inabadilika kulingana hali ya soko husika hivo ni lazima ukubaliane na mazingira halisi hiyo ni bei kadirifu .
Changamoto za Biashara ni kama
Uchawi , siku zote kwenye biashara chuki haikosi na mujini fitina afu hili kwa mfanyabiashara ni jambo dogo sana.
Wizi , umakini unahitajika wakati wote kianzia porini mpaka sokoni.
Muda na upatikanaji wa mzigo , kuna wakati Dagaa haipatikani na kuna muda inapatikana sana kufurika sokoni hivo hata soko kuharibika .
Suluhu ya yote ni kujipanga wewe mwenyewe kibiashara na kimalengo.
Mimi nimewahi kuifanya na kulifanyia kampuni la Rafiki yangu kwa sasa niko mbali kidogo na Musoma na Mwanza ila Connections na links zipo porini mpaka Sokoni.
Karibuni sana Dagaa inalipa Ukijipanga.
Mawasiliano 0767258286.
0785303473.
Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app