PostGE2025 Daffi: Tukiandamana dunia itashangaa kwanini tumeshindwa kukubaliana

PostGE2025 Daffi: Tukiandamana dunia itashangaa kwanini tumeshindwa kukubaliana

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,271
Reaction score
3,927
Mwanasiasa Peter Daffi amesema maandamano yasiyo na kibali hayawezi kuruhusiwa na serikali, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kuifanya dunia kushangaa kwa nini Watanzania wanashindwa kukaa, kuzungumza na kukubaliana kama taifa.

Akizungumza na wanahabari leo Desemba 05, 2025 jijini Dodoma, Daffi amesema waliotaka kutoa maoni yao tayari wametengewa nafasi kupitia Tume iliyoanzishwa na Rais, na hivyo ni muhimu wananchi kuisikiliza tume hiyo na kuwasilisha mapendekezo yao kwa njia iliyowekwa.

“Mlijaribu Oktoba 29, na kama mlikuwa mnataka kutuma maoni yenu, Rais ameunda tume. Ile tume sasa tuiisikilize ili itekeleze yale tunayodhania na tunayotamani yafanyike. Maana hata mkihamasisha kufanya vurugu tarehe 09 Desemba mnayoisema, baada ya hapo mnahitaji nini?” amehoji.

Amesema hadi sasa hakuna kibali cha maandamano, hivyo juhudi zozote za kuhamasisha vurugu haziwezi kukubalika kwa kuwa vinahatarisha usalama wa watu na mali.

“Vyombo vya serikali vyenye mamlaka ya kulinda raia na mali zao vitaendelea kufanya kazi. Serikali na vyombo vyake haviwezi kuruhusu maandamano bila kibali. Mnataka turuhusu tena hali ya kushangaza duniani kwamba tumesindwa kukaa na kuzungumza na kukubaliana?” amesema.

Daffi ameongeza kuwa Tume iliyoanzishwa na Rais ndiyo njia sahihi ya kusikiliza maoni ya wananchi, na kwamba ikifika katika maeneo mbalimbali wananchi wanapaswa kutoa maoni yao ili serikali iweze kutekeleza wanayoyahitaji.


 

Attachments

  • VIDEO-Mwanasiasa Peter Daffi amesema maandamano yasiyo na kibali hayawezi kuruhusiwa na serikali.mp4
    14.5 MB
Akili nyingine bhana, Ile sio tume ya kukusanya maoni, bali ni tume ya kuchunguza kiini Cha tatizo.

Na inachunguza nini wakati serikali imeshasema tatizo ni mabeberu wanaozitamani rasilimali za nchi yetu!!!

Majibu yameshapatikana ni Bora ikavunjwa tuu tuendelee na mambo yajayo.
 
Maandamano yani kibali ? sikia hili kubwa jinga, sasa tufanye serikali ni haramu na jeshi la polisi ni wauwaji bado utaenda kuwaomba kibali uandamane kudai haki zako ?
 
Dafi tangu aanze harakati za kuwa dekio la CCM hajawahi kukumbukwa kwenye uteuzi, atafute godfather aache kelele zake za kipuuzi.
 
Back
Top Bottom