Dada zetu kuweni honest, mtuonyeshe pia wanaowawezesha!

Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,320
17,823
Salamu wote hapa jamvini!

wakati tukiendelea kutafakari ya Mange na kamanda Sirro, na ugumu wa maisha kwa ujumla, kuna jambo kidooogo nimeona haliko sawa kimahusiano hasa upande wa dada zetu

Ni hivi, unakuta baadhi wa kina dada 'wanajinasibu' kuwa likizo na 'kula bata' sehemu 'za nguvu' kama mbugani na mahoteli makubwa,

wakiwa huko wanapiga 'maselfie ya kufa mtu' (GENTAMYCINE anayajua) na kutupia mitandaoni hasa facebook na instagram 'kutudolishia' kwama wako likizo au wanakula bata;)

Ambacho hawasemi au kuonyesha ni 'waambata' wao ambao kusema kweli ndio ma 'sponsor' wa hizo trip na bata zinazoambatana nazo.:confused:

hebu wadada kuweni honest kidogo, mseme kabisa labda hii trip iko sponsored na aidha 'mume wa mtu' au 'danga la mtu' ndio maana hataki kuonekana kwenye picha, (maana najua mtakuja kwa utetezi huo hapa) na kama vipi ni mtu wako halali basi tuone mmetokelezea kwenye hayo mapicha picha

Ilivyo wengi mnawaficha kisha kujifanya ni 'nguvu zenu' binafsi (sikatai) ila kwa hali ilivyokaza sasa hivi, napata mashaka sana:(

Hii sio kusema kwamba wanawake baadhi yenu hamuwezi, ila pia ukweli ni kwamba mnaojianika huko tunawajua 'hali zenu'!

halafu nione mtu anasema 'tunawaonea wivu' hapana, kuweni tu honest!:D:D

nawatakia mchana mwema wote.

Asprin nilikuona na Sakayo mahali sijajua 'categori' yako bado!
 
Kuna mdada mmoja tupo nae maeneo alikuwa chakula ya marehem mzee 6...siku ya msiba alilia mpk tukambeba.


Mrija ndio umekatika tena majanga tu na hali hii ya magu hamna rangi utaacha kuona

ukimkuta mtaani anavojishebedua sasa...unafiki mtupu
 
Back
Top Bottom