Mimi nina imani kuwa kuhamia kwake CCM kuna mahusiano na jinsia yake kama mwanamke na sio nafsi ukizingatia kuwa akiwa Chadema wanaume wengi licha ya kumheshimu, pia walimwogopa kwa sababu ya kuwa ndugu wa Mwenyekiti wao Bwana Mbowe. Jinsia yake ilipata wakati mgumu lakini kwa sasa iko huru ingawa nafsi itaendelea kumsuta kwani haijahama wala haitahama Chadema. jibu litakuwa wazi pindi Chadema ikiingia ikulu na kaka yake akashika nafasi ya waziri mkuu. Isitoshe kaka yake anawindwa sana na mafisadi kwa mabomu na risasi ili auwawe, hivyo uwepo wa dada huyo CCM unaweza kuzima harakati hizo ... si atakuwa shemeji. Kwa hilo nampongeza huyo dada kwa kuhamia CCM maana amecheza kama messi na CCM kwa kutokujua wanashangilia bila kujua hilo ni bao la kisigino.