Dada ni jina halisi la tatu la Idi Amini?

jina halisi lilikua idd amin kaidada lkini akaondoa kai baada ya kuingia jeshini. soma reign of terror by henry kiemba or kyemba
 
Mkuu upo dunia gani? Wanubii hutumia jina kama majina yote ya kawaida DADA kwao ni jina maarufu.... Huko Barazil "kaka" ni jina kiume lakini hata waRussi hutumia kwa wanawake....AFU eti tulimpa kichapoo!! Soma historiya!! tena Fatilia matokeo...... afu ukishindwa ULIZA (?) siyo aibu kuuliza....!!
Kwaiyo unataka kusema Nduli Dada hatujamtia dozi?Ahahahah..Waulize Saudi Arabia.
 
jina halisi lilikua idd amin kaidada lkini akaondoa kai baada ya kuingia jeshini. soma reign of terror by henry kiemba or kyemba

Jina lake kamili ni Idd Amin Kaidada alipewa jina la DADA January 26,1970 na yy akalikubali!

ILIKUAJE kupewa jina hili?:

January 25 usiku aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Uganda Brigedier Pierino Yere Okoya na mkewe Anna waliuliwa kijijini kwake Kora nje kidogo ya mji wa Guru!Kundi la kimafia la "Kondo"lililokuja gundulika baadae linafadhiliwa na Gen Idd Amin kipindi hicho ni Mkuu wa Majeshi ya Uganda lilihusika na mauaji haya!

Baada ya taarifa za kifo cha Brig Okoya kuvuja;maafisa wote waandamizi walikutana usiku huo huo Makao Makuu ya Jeshi Malire kutuliza hali ya mvutano wa askari wa kabila la Acholi walio chukizwa sana na kifo cha ndugu yao Brig Okoya lkn Mkuu wa Majeshi Gen Amin hakuwepo kikosini!

Mkuu wa Usalama wa Jeshi Kanali Nyangweso akampigia simu mara kadhaa Gen Amin aje haraka Malire bila mafanikio ndipo akaamuru yy na wasaidizi wake Capt Kitumba na Lt Avudria waende nyumbani kwa Gen Amin huko Bamunika kumpa taarifa!

Walipofika getini walinzi waliwahakikishia kuwa Gen Amin yupo ndani lkn walipoingia waligonga sana mlango bila kufunguliwa na kuamua kurudi kikosini!

Kesho yake asubuhi Gen Amin akafika Malire akiwa na bandeji mikononi na michubuko kadhaa na kukuta maafisa wenzake wanaendelea na kikao!

Col Nyangweso akamuuliza Gen Amin kuhusu safari yao ya jana usiku kwake na kwa nn hakufungua mlango?Gen Amin kujitetea akajibu kuwa alihisi walio muua Brig Okoya wamekuja pia kumuua yy na ndipo aliposikia mlango unagongwa akapitia mlango wa nyuma na kuruka ukuta na kujiumiza na seng'eng'e!

Maafisa wenzake walishangaa sana kusikia kuwa bosi wao aliogopa na kwa kumtania wakamuambia kuwa kitendo cha afisa mkubwa wa jeshi kuogopa adui hata kama anakuja kukudhuru ni sawa na uoga wa akina DADA watembeapo wenyewe usiku!Toka siku hiyo jina la DADA likamganda na yy akakubali

INTERESTING ENOUGH;tarehe kama hiyo hiyo mwaka uliofuatia yaani January 25,1971 Gen Amin kwa kusaidiwa na askari wa kabila lake la Kakwa na majirani zake Lugbara toka kikosi cha Simba mjini Moroto akatwaa madaraka kwa hila na kuanza kutimiza ndoto yake ya kuwaua maafisa wasomi wote wa jeshi toka kabila la Acholi na Langi
 
Mimi nilivyosikia ni kuwa Iddi Amin hili jina la Dada alipewa siku moja jeshini
wakatu huo Uganda inatawaliwa na wakoloni Wazungu
Iddi Amin alifumaniwa na mwanamke huko jeshini
yeye akiwa kuruta tu bado..so mkuu wa kambi mzungu alipomuuliza
'who is this' Iddi Amini alijibu 'dada' ya kiswahili kama huyo mwanamke ni dada yake
so alipoadhibiwa kwa kosa hilo hao wazungu jeshini ndo wakawa wanamuita
Iddi Amin Dada kumtania kwa ishu hiyo...
Ahahahah..very interesting inaelekea jamaa alikuwa kicheche sana.
 
Just a theory,

Majina mengi ya viongozi yanakuwa si yao halisi bali ya kupewa/ kujipachika. Kwa mfano, Kenyatta lilitokana na "Kenya Taa".

Museveni lilitokana na baba yake Yoweri Museveni kuwa mpiganaji wa kikosi cha saba, hivyo "Museveni"

Jina halisi la Idi Amin ni Idi Amin Oumee

Brief History of Idi Amin Dada

Alternatively,

Kiingereza, neno "Dada" ni namna watoto wanavyomuita baba, yaani mtoto mdogo anaweza kumuita baba/ babu yake "Dada" badala ya "Daddy"/ Granddaddy, hasa watoto wale ambao hawajaweza kutamka maneno vizuri.

Idi Amini alikuwa mtu wa majigambo na alipenda kujulikana kama "Big Daddy".

Inawezekana akaja kuijumuisha "Dada" aliyopewa na "Daddy".
Duuh..Mkuu nondo zako ni za hatari.Vipi stori ya boss umeshawahi sikia?
 
Last edited by a moderator:
Jina lake kamili ni Idd Amin Kaidada alipewa jina la DADA January 26,1970 na yy akalikubali!

ILIKUAJE kupewa jina hili?:

January 25 usiku aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Uganda Brigedier Pierino Yere Okoya na mkewe Anna waliuliwa kijijini kwake Kora nje kidogo ya mji wa Guru!Kundi la kimafia la "Kondo"lililokuja gundulika baadae linafadhiliwa na Gen Idd Amin kipindi hicho ni Mkuu wa Majeshi ya Uganda lilihusika na mauaji haya!

Baada ya taarifa za kifo cha Brig Okoya kuvuja;maafisa wote waandamizi walikutana usiku huo huo Makao Makuu ya Jeshi Malire kutuliza hali ya mvutano wa askari wa kabila la Acholi walio chukizwa sana na kifo cha ndugu yao Brig Okoya lkn Mkuu wa Majeshi Gen Amin hakuwepo kikosini!

Mkuu wa Usalama wa Jeshi Kanali Nyangweso akampigia simu mara kadhaa Gen Amin aje haraka Malire bila mafanikio ndipo akaamuru yy na wasaidizi wake Capt Kitumba na Lt Avudria waende nyumbani kwa Gen Amin huko Bamunika kumpa taarifa!

Walipofika getini walinzi waliwahakikishia kuwa Gen Amin yupo ndani lkn walipoingia waligonga sana mlango bila kufunguliwa na kuamua kurudi kikosini!

Kesho yake asubuhi Gen Amin akafika Malire akiwa na bandeji mikononi na michubuko kadhaa na kukuta maafisa wenzake wanaendelea na kikao!

Col Nyangweso akamuuliza Gen Amin kuhusu safari yao ya jana usiku kwake na kwa nn hakufungua mlango?Gen Amin kujitetea akajibu kuwa alihisi walio muua Brig Okoya wamekuja pia kumuua yy na ndipo aliposikia mlango unagongwa akapitia mlango wa nyuma na kuruka ukuta na kujiumiza na seng'eng'e!

Maafisa wenzake walishangaa sana kusikia kuwa bosi wao aliogopa na kwa kumtania wakamuambia kuwa kitendo cha afisa mkubwa wa jeshi kuogopa adui hata kama anakuja kukudhuru ni sawa na uoga wa akina DADA watembeapo wenyewe usiku!Toka siku hiyo jina la DADA likamganda na yy akakubali

INTERESTING ENOUGH;tarehe kama hiyo hiyo mwaka uliofuatia yaani January 25,1971 Gen Amin kwa kusaidiwa na askari wa kabila lake la Kakwa na majirani zake Lugbara toka kikosi cha Simba mjini Moroto akatwaa madaraka kwa hila na kuanza kutimiza ndoto yake ya kuwaua maafisa wasomi wote wa jeshi toka kabila la Acholi na Langi
Duuh..Hii ndio Jf.Ahsante mkuu.
 
_

yuko dunia gani kivipi?
...ameomba aeleweshwe unamjibu shudu?
...je wewe unajua historia ya Eid Amin?
...unafikiri kwa yeye DADA lilikuwa jina kama ilivyo kwa hao wanubi?
...naomba na wewe urudi kutafuta historia ikiwezekana husisha na wazee waenzi za vita ya kagera watakusaidia xana..
....period!
Mkuu shukrani sana.
 
Wakuu salaam,
Kama mnavyojua kwamba Dada humaanisha ndugu mkubwa mwanamke.Sasa inakuwaje Idi Amini aliitwa jina la mwisho Dada?Je ni asili ya jina lake kweli au ni kejeli baada ya kumpa kichapo kizito?Wadau tujuzane.

wa Uganda walimbatiza ilo jina kutokana kuwa na wake wengi..kwenye utambulisho anatambulisha wake adi anaanza kuzuga engine anasema mydada...sister...ndo lilipo tokea
 
Back
Top Bottom