Unachoona ujeuri pengine ni "tough love" tu.Unaonekana ni mshauri mzuri sana, ila tatizo lako jeuri, ushauri wako ni muhimu pia, tiririka tafadhali, unafikiri anahitaji mtaalam wa afya ya akili kati ya dada yetu na mume wake?
Mke huyo anatusindikiza mwacheni.Yupi dada au shemeji?
1.Kuingilia ndoa ya mtu mzima mwenye akili zake ni kazi sana.Sio za kaka ni dada na shemeji, ndio maana nasema umekurupuka hujasoma ukaelewa
[emoji106] [emoji106] [emoji106] ndio maana nimesema unaonekana una ushauri mzuri.1.Kuingilia ndoa ya mtu mzima mwenye akili zake ni kazi sana.
2. Kama umempenda sana ndugu yako na unaona kuna haja ya kuingilia, sehemu husika ni vikao vya familia.
3. Kama umeleta hapa ili upate ushauri, ushauri wangu ndio huo, habari hii itafaa kuwapata wazee wenye busara na kukaa vikao vya familia, kama kuna muafaka wa kufanya hivyo kutoka kwa wenye ndoa.
4. Zaidi ya hapo onesha mfano wewe kwenye ndoa yako.
5. Samahani kama nimekubwenga visivyo, simakusudi, ni kuwekana sawa tu.