Dada kunawagharimu mno kuliko wanaume

Dada kunawagharimu mno kuliko wanaume

germve

Senior Member
Joined
Jul 22, 2017
Posts
126
Reaction score
132
BLEEDING LOVE

Isingekuwa rahisi kujizuia. Angewezaje kujizuia ikiwa mashoga zake karibu wote walikuwa na michepuko yao, na bado ndoa zao zikabaki salama vile vile?

Shoga yake aitwaye Amina alikuwa anachepuka na Mwarabu mmoja mfanyabiashara maarufu wa Arusha. Mchepuo wao ulianzia kwenye Precision Air, pindi walipokutana kwa mara ya kwanza angani.

Shoga yake mwingine anaitwa Mariam, yeye hakuwahi kuficha kuhusu kushirikiana kimapenzi na Kijana Robert, mtanashati na msomi waliyefanya naye kazi katika ofisi moja!

Hapo sijazungumzia mawifi zake, na hata baadhi ya ndugu zake ambao alijua fika huwa hawatulii NJIA KUU!

Kama unadhani hiyo ilikuwa sababu kuu, basi sijakueleza sababu ya pili....
Huu ni mwezi wa pili sasa tangu mumewe ahamishiwe Kahama kikazi. Na duru za kiofisi zilionesha kutokana na uzito wa kazi iliyompeleka huko Kahama angedumu huko kwa miezi mingine mitatu zaidi bila kurudi Dar! Sasa yeye angedhibiti vipi vichocheo vilivyousakama mwili wake?

Ni kweli ana mtoto mmoja wa miaka mitatu lakini wadhani angetosha kumfanya asihisi vichocheo? La hasha!

Kila saa ya kulala vichocheo vilimuandama kama maandamano! Na maskini hakujua kuwa huo mtandao wa xvideos ndiyo ulioamrisha vichocheo vyake kumsumbua.

Alijiwekea utaratibu mbaya wa kutembelea mtandao huo kila ifikapo saa ya kulala. Hakujua kama hiyo ingekuwa sababu ya tatu ya kumuondolea stamina ya "kujinyima"!
Matokeo yake alijiapiza kuwa asingeweza kujinyima zaidi.
Ndipo wazo la kumkubalia Arone, yule kijana chakaramu mwenye duka la nguo likamjia. Arone alishatumia kila msamiati wenye ladha mwanana ya kumlainisha kiumbe huyu wa kike bila mafanikio.

Akiwa katika vazi la usiku juu ya kitanda cha futi sita za mraba alijikuta akianza kumchokoza Arone kupitia namba yake ya whatsapp..... Uchokozi ambao ulifikia hatua ya kutumiana picha za usiku huo....

Haikushangaza pale kesho yake ilipowashuhudia wawili hawa ndani ya Lodge moja maarufu iliyopo nyuma ya kanisa katoliki pale Mbagala Zakhem wakihangaishana kuivunja mojawapo ya zile amri kumi za MUUMBA!

Rhoda hakujali kuhusu umri mdogo wa Arone. Umbo lake lenye idadi ya kuridhisha ya packs lilimfanya asiwaze kuhusu tofauti ya miaka kumi baina yao.
Alichomudu kukiwaza kama si kushangaa ni namna kijana yule alivyoweza kufuga nywele nyingi vile kifuani pake!? Wenye taaluma yao wanaita Garden love!

Ghafla akatabasamu kwa dharau baada ya kukikumbuka kifua cha mumewe kisicho na chembe ya unywele mithili ya ngozi ya nyoka!
Hapo tena alivipoteza vidole vyake ndani ya msitu ule. Ikampa raha ya ajabu!

Hakuna namna nyingine hapo, tendo ilibidi lifanyike. Na kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kuchepuka ilimpa furaha, raha, na ashakum si matusi.... Utamu wa ajabu!

Ikawa ngumu kukumbuka walichoahidiana kabla ya kuanza kuchepuana! Kinga!
Alichowahi Rhonda kukisikia pindi alipomkumbusha kuhusu kinga ni jibu la haraka haraka la Arone... Ntaweka... Ntahamishia... Ntamwagia.... Hakukumbuka vizuri, lakini lolote lililotanguliwa na mojawapo ya maneno matatu hapo juu lilifuatiwa na neno,.......nje! Bahati mbaya ahadi haikutekelezwa. Hiyo nje ikahamia ndani!

Tukiachana na hayo yaliyojiri Mkululu Lodge, tuhamie kwenye kilichofuata miezi miwili baadaye.

Mume wa Rhoda alikuwa amerejea kutoka Kahama akiwa na fedha nyingi sana alizovuna kutoka Kahama. Bahati mbaya hakuweza kuzitumia ipasavyo kutokana na hali aliyomkuta nayo mkewe mpendwa!

Kutapika na kupoteza hamu ya kila kitu kulimfanya Amos asimfurahie mkewe kwa jinsi alivyotaka. Ile mitoko ya usiku, kuogelea, muziki na ratiba nyingine za kustarehesha miili yao hazikuweza kufanikiwa!

Ambacho ndugu yangu Amos hakukijua ni kuwa mkewe alikuwa na Mimba ya Arone.
Lakini Rhoda hakuwa mgeni wa mimba, alishagundua mapema kuwa alinasa! Ambacho kilikuwa kigeni kwake ni namna ya kuinasua.....

Hapo ndipo alipohitaji ushauri wa mashoga zake ambao kwao michezo ya kuinasua mimba ilikuwa sawa na kujitia vidole mdomoni ili kutapika! Haikuwahi kuwa shida kwao.

Sasa ushauri uliopatikana ili kuinusuru ndoa ya Rhoda ndio uliomfikisha Rhoda asubuhi hii ya saa nne mbele ya huyu mtu ambaye ni vigumu kumtambua kama alikuwa Mzee au kijana! Ndevu zake shabishabi zilijaa mvi, uso wake ulienea makunyanzi, macho mekundu! Na japo inadhaniwa alikuwa mweupe kwa ngozi, basi weupe ulishanyoonywa siku nyingi na pombe kali alizoziruhusu kuuharibu mwili wake.

Tabasamu lake lilifichua meno ya njano yaliyojutia kukutana na mataputapu ya kila siku. Naam! Huyu ndiyo Dokta John aliyepaswa kumtolea mimba Rhoda ili kuinusuru ndoa yake.

Usimuone hivyo, huyu ni dokta mzuri sana!
Hiyo kauli ilimtoka Amina katika kumtoa hofu Rhoda.....

Utoaji mimba ulifana vilivyo na Rhoda akarudi nyumbani akiwa fiti kalikiti! Usiku huo Rhoda alikuwa na amani tele kwa kufanikisha....
Na usiku huo Rhoda alikuwa na furaha sana ndiyo maana hata mumewe alipohitaji chakula cha usiku walishirikiana kukila kwa "umoja ni nguvu! "

Nusu saa baadae Rhoda alishangaaa kuona matone ya damu yakimtoka "chini"!

Akajaribu kuyadhibiti kwa vipande vya kanga lakini havikufua dafu. Damu iliongezeka kutoka kwenye matone na kuwa mabonge!

Kulia alishindwa kucheka alishindwa! Akakumbuka kumtumia SMS shogaye Amina kuwa damu zilikuwa zikimtoka!

Kabla amina hajamjibu mumewe alirejea kutoka sebuleni alikokuwa akiangalia mechi ya mpira wa miguu! Akashangaa kumkuta mkewe akiwa dhaifu kama mhanga wa njaa ya Somalia!

Sauti yake ilikuwa dhaifu na hata msamaha aliojaribu kuomba ulisikika kwa tabu....

Mume wangu nisamehe......... Nilikusaliti...... Nakufa.... Nilitoa mimba!
Kwa jinsi alivyompenda mkewe Amos hakumuelewa mkewe akahisi Malaria imehamia kichwani. Jitihada za kumfikisha muhimbili hazikufua dafu, Rhoda aliaga dunia kutokana na mvujo wa damu usio wa kawaida!

germve himself
 
Kutoa mimba kuna utaalamu wake ,,,,,ila kwa wasioolewa ,ukiwa na ndoa tena ukamsaliti mmeo ukatoa mimba laana kama hizo ndio adhabu ya msaliti
 
Sio yangu nime c&p

germve himself
 
Stori nzurii yenye mafundisho mazuri
Haya mambo yapo katika jamii lisipo kupata kama hilo bc pengine magonjwaa
Mwenye masikio na asikie
Heshima kwako kwa mtoa uzi
 
Stori nzurii yenye mafundisho mazuri
Haya mambo yapo katika jamii lisipo kupata kama hilo bc pengine magonjwaa
Mwenye masikio na asikie
Heshima kwako kwa mtoa uzi
Thanks mkuu

germve himself
 
Back
Top Bottom