Huyu dada alinipenda, nikamweleza ukweli juu ya maisha yangu. Akasema amenipenda kwa dhati. Baada ya muda sio mrefu sana akapata kazi sehemu moja ya wachezesha kamari.Akaanza na maringo na kunipa mitihani ya kumtumia kiasi cha pesa ambacho sikupenda kumpatia kwani sikupenda kumzoesha pesa kwani baadae huenda nikifulia akanikataa.Nilipokuwa simpatii, akanigeuka na kuanza kunitusi kwamba eti alikuwa ananijaribu na hangeweza kuolewa na mimi maana nangekwenda kumfanya apauke na kwamba eti kwao hali yao kimaisha ni nzuri na eti yeye amekwenda kidato na ana jiwe moja. Nikamuuliza akasema eti anaweza kumpata mwenye pesa na anagawa wakati akiwachunguza wataompatia fedha je,HUYU ANA AKILI ZAKE TIMAMU?