Dada huyo mwanaume siyo

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,968
Nilitamani kucheka, nikaamua kujizuia, ilikuwa jana usiku nakatisha mitaa fulani nikasikia mazungumzo wa watu wawili,

Dada na kaka, kaka analalama siku dada yake anaolewa kwa mujibu wa tamaduni zao kaka huwa anazuia dada asitoke siku ya harusi hadi wale waoaji wampatie zawadi,

Siku hiyo jamaa kakaba mlangoni, shemeji mtu akafungika elfu 5,

Kaka mtu akazidi kukomaa waongeze lakini wapi, kaka mtu alisimama hapo mlangoni hadi akachoka jamaa hawatoi kitu, ikabidi tu aachie dada yake atoke akaolewe, ilikuwa ndoa ya kiisilamu,

Siku hiyo jamaa ndo anamlalamikia dada yake, huyo mwanaume siyo.
 
Watu wengine wanadhalilisha kinsia zetu tu...
 
Watu wanapofanya ndoa za wenzao kuwa mtaji...

Huyo kijana aliyetamka hivyo anaonesha si mchapakazi ndio maana aliamua kushupalia fedha ya ubwete ubwete
 
kwa nini mkuu?
Yaani mahali ishalipwa, ndoa ishafungwa, halafu ukagande mlangoni, na bado umenyimwa ulichotaka.... Kama si ujinga ni nini..??? Ye mwenyewe hana alichotaka apewe..

Halafu analalama kwa dada eti mwanaume siyo, hivi anajuwa dada yake kampendea nini huyo mwanaume...??? Pengine mwenzie kapenda gegedeo..?? Anataka agawiwe gegedeo...???

 
Ana bahati sana alipata hiyo buku 5,kwangu asingrlamba hata mia na dada yange ningechukua
 
Alitaka mtaji akakuta shemeji mjanja....!!

huu kweli ni ujanja? hizi ni mila zetu, kama nyie mnaziona hazifai basi mzifute muwe watumwa wa wazungu.
 
Ana bahati sana alipata hiyo buku 5,kwangu asingrlamba hata mia na dada yange ningechukua

mkuu hujui hizi ni mila zetu? mimi tafsiri ni kuwa mwanaume alikuwa mchovu tu.
 
Hizi mila zingine zimepitwa na wakati naona kama zinadhalilisha.

kwa kizazi hiki tunakoelekea siko, haya mambo yana maana zake, sitashangaa na wanaume tukaanza kuolewa.
 
Ameeeeen,

Wamefanya wanachotaka for a long time na sasa wana-take things for granted! imefikia point wananchi wamechoka. Hali za maisha ni ngumu na wao wanatumbua tu na kuuza nchi!..........

Ningekuw mm ndo naoa naongeza mahali nawachukua wote wawili.
 
Hahahaaaaha angechelewa kidogo bibi harusi angempush atoke aseeeee
 
huu kweli ni ujanja? hizi ni mila zetu, kama nyie mnaziona hazifai basi mzifute muwe watumwa wa wazungu.
Sasa shemeji unataka upewe hela ya nini?? Nimechukua dada yako na nimetoa mahari inatosha...! Hayo mambo mengine kuchoshana na kupotezeana muda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…