Kuna kisa kimoja nimekisoma mahala kikanivutia kiasi nikaona si vibaya nikakiweka hapa na dada zangu wengine wakapata kufaidika, japo kidogo nao wakaweza kuchukuwa hatua stahiki.Hapo kitambo
kidogo paliondokea kijana mmoja akiishi na umbu wake (dada yake) wa kuzaliwa baba/mama mmoja. Mara kwa mara dada mtu akimshtakia kuwa kila akipita mitaani, vijana wanamsumbua kwa maneno ya kumtaka na wakati mwingine akipita wanapiga miruzi na
mambo kadhaa wa kadhaa.Kaka mtu baada ya kusikiliza mashataka ya dada mtu, siku moja akamchukua kunakouzwa mavazi ya kisharia
akamnunulia vazi la heshima na akamkabidhi dadake...!Muda ukapita takriban mwezi na zaidi. Kaka mtu akamuuliza umbu wake:"Je vijana bado wanakusumbua na kukutongoza?"Dada Mtu Akajibu:
"La Wallahi, tangu nivae vazi hili wote wananiheshimu. Na hata nikipanda kwenye basi kama nimekosa kiti, basi wapo wanao nipisha ili niketi"Kaka mtu akamwambia dadake:
"Wewe ndiye uliyekuwa ukiwatongoza kwa mavazi yako yasio na heshima.Dada mtu akashtuka na kushangaa, ni vipi mimi mwanamke nithubutu kuwatongoza mabarobaro barabarani!Kaka mtu akamfahamisha:
Kama ingekuwa ni wao ndio chanzo cha kukutongoza na kukusumbua na hata kukuvunjia heshima yako, basi wangeendelea
kukusumbua pamoja na kuvaa kwako vazi la heshima.Lakini tangia ujistiri, wamekuwa mbali na wewe kwa sababu wanakuona kuwa wewe ni mwanamke mwenye kujiheshimu."