Daah! Kiukweli Ali Kiba anachosha sana

Daah! Kiukweli Ali Kiba anachosha sana

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
184
.
By Sangu Joseph
.
Mxieeeew! Ngoja nianze kwa kumsonya ndugu Mfalme japo nahofia sana Team Kiba kuja kunishambulia, kwa sababu tu ya kuandika mawazo yangu, Ila kiukweli Mfalme Alikiba ni moja ya watu ambao wananiangusha sana, sana, sana.

Kumradhi kumtusi mfalme Ila rejea andiko langu nililoeleza kwanini Harmonize atampita Ali Kiba. Kimsingi nimeshtushwa sana vijana wenye vipaji kama Killy na Cheed kuondoka katika kipindi cha ujenzi wa Label.

Kinachonisikitisha sana unajua tuko katika nyakati ambazo tunawatazama watu 3 (Harmonize, Alikiba na Diamond) tulitarajia kuona Kings Music ikijijenga zaidi kama tunavyoona kwa Konde Boy Harmonize kwa kumuongeza kwa haraka Ibraah TZ ili kuongeza mashambulizi kwenye Uwanja wa Vita.

The same kwa Diamond tunaona anajenga ngome yake WCB kwa kununua silaha mpya aina ya @OfficialZuchu made in Tanzania.

Kwa mfalme Alikiba imekua tofauti kidogo kwa sababu badala ya kujenga ngome, kwake inabomoka na Maaskari waaminifu wanamkimbia na wanavyokimbia hawaelezi cha maana zaidi ya kutuachia vumbi na sisi tukieendelea kuisoma namba.

Unaweza ukasema kwani hii ni mara ya kwanza Msanii kukimbia ndani ya Label mbona hata Diamond ilishamtokea kwa Harmonize na Rich Mavoko, lakini nitakujibu angalia life Span ambayo alikaa Mavoko na Konde Boy unagundua nizaidi miaka 4 acha ile ya kukaa benchini bila kupewa namba.

Kwa kumbukumbu huyu ni Msanii wa tatu kuondoka chini ya usimamizi wa Mfalme ukimuongeza na Young Boy Baraka the Prince na kwa uzoefu wangu wa kufuatilia burudani mara nyingi Msanii akiondoka ndani ya label wengine huwa wanakua na makosa lakini asilimia kubwa huwa wanakua na matarajio ya kuyafikia lakini wanaona management waliyokuwa nayo hawawezi kufikia ndicho ambacho Mimi nahisi Cheed na Killy kimewafanya wametuachia vumbi.

Next post nitaeleza anaposhindwa Ali Kiba mpaka wasanii wachanga wanaondoka katika kipindi kama hichi ambacho walihitaji kukua zaidi, Ila chakumalizia tu Ali Kiba anarudi nyuma hatua wakati wenzake wakijipanga zaidi.
.
INSTA : FB : TWIT : SANGUJOSEPH
.
#KijanaMzalendo #IloveTZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu upo katika industry kama nani?Au una uelewa wa masuala ya kiwanda cha muziki?
Unajua maana ya record label na kazi zake?Unajua music publishing company na kazi?
Tunaomba katika makala yako ugusie pia
 
Mkuu upo katika industry kama nani?Au una uelewa wa masuala ya kiwanda cha muziki?
Unajua maana ya record label na kazi zake?Unajua music publishing company na kazi?
Tunaomba katika makala yako ugusie pia
Mkuu Mimi ni mpenzi wa Burudani wa Burudani pia nafanyia media industry so nafuatili haya masuala ya muziki.

Nadhani kunifahamu zaidi karibu kunifuatilia Face au Instagram SanguJoseph nina biography nzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaonekana yule dada mtangazaji wa radio,amevunja mahusiano na Alikiba,na hivyo yaweza kuhusishwa na ushawishi wake kwa waimbaji vijana wawili kutoka 'Kings Label'
 
Nimejilazimisha kulielewa dodo la ndugu mfalme lakin wapi asee na huku quarantine ukata umetanda kifurush kimekata kila nikitune clouds nakutana na ndugu mfalme EaTV ametamalaki TVE nakutana na his majesty tu anaimba utopolo dawa yake ni kulipia kifurushi na kuukwepa unyonge wa ndugu mfalme
 
Ali Kiba anajua anachofanya ndio maana hakuwapa mikataba, na wale watoto ndio wamepotea hivyo masikini, walitakiwa wawe wavumilivu na pia wana managers wao wangeanza kujitafutia shows nyingi huku wanapenya na jina la Kings Music mpaka wawe na fanbase yao.Sasa safari yao itakuwa ndefu sana wakuu, biashara ya music bongo bado iko shapeless.
Mkuu tena kama uko katika media ndio utakuwa unajua vizuri jinsi gani hamna formalities nzuri za promotion na bakshishi ndio mfumo.
 
Back
Top Bottom