Daaah... yaaan!

Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,868
6,480
TAIFA STARS YAPOKONYWA USHINDI DHIDI YA UGANDA NA KUKOSA NAFASI YA AFCON

CAIRO MISRI

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepokonywa ushindi dhidi ya Uganda katika mechi yao ya mwisho ya kufuzu Mataifa ya Afrika baada ya kugundulika hujuma katika mechi hiyo. Habari nyeti zilizopatikana usiku huu kutoka Makao Makuu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) yaliyoko huko Cairo Misri zinasema kwamba hujuma hizo ni pamoja na kitendo kilichofanywa na Jeshi la Tanzania kupiga mizinga nje ya Uwanja kabla ya mechi kuanza, kitendo kinachochukuliwa kama ni kuwatisha wachezaji wa Uganda, na hivyo kuwa kinyume na kanuni za CAF na FIFA kwa Ujumla.

Pamoja na kwamba bado haijajulikana ni adhabu gani ambayo Taifa Stars watapewa na CAF lakini ni wazi sasa kwamba Uganda watapewa pointi zao tatu na hivyo Lesotho kuchukua nafasi ya Tanzania katika kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kufanyika June 2019 mwaka huu huko Misri.

Akihojiwa kwa njia ya simu kutokea nyumbani kwake Dar es Salaam usiku huu, Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Bwana Wallace Karia amesema kwamba bado hawajapata barua rasmi au taarifa yoyote kwa maandishi kutoka CAF juu ya uamuzi huo, hivyo hawezi kuelezea chochote kwasasa. Hata hivyo ameahidi kwamba pindi taarifa hiyo itakapokuwa Rasmi, TFF itaitisha mkutano na vyombo Vya habari ili kutoa maelezo juu ya taarifa hiyo.





















































































































































































































Leo ni Siku ya Wajinga Duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom