kitongoroso
Member
- Nov 3, 2013
- 29
- 4
Mbunge wa moshi vijijini juzi aliumbuka kwenye mkutano aliowakutanisha makada mbalimbali wa chama cha mapinduzi kutoka kwenye matawi ya ccm ndani ya jimbo la moshi vijijini. Mkutano huo uliofanyikia YMCA mbunge chami alipandwa na gadhabu kali sana kiasi cha kushindwa kuendelea kuongea baada ya mjumbe mmoja kumtaka mbunge huyo kuwaelezea wajumbe wa mkutano huo kwa nn alifukuzwa kwenye nafasi yake ya uwaziri.
Baada ya swali hilo mbunge huyo alianza kufoka kwa kumtuhumu mjumbe huyo alaiyejulikana kwa jina moja tu la massawe kuwa ametumwa kuharibu mkutano huo. Wajumbe toka ndani ya mkutano huo walisema kuwa mbunge chami amekuwa hapati usingizi kwani anajua nafasi yake ya ubunge jimboni kwake hataipata tena kwani wakazi wengi wa jimbo hili wamechoshwa na utendaji wake mbovu. Kwa kujua kuwa hatarudi tena madarakani amekuwa akihaha kila siku kuitisha mikutano na viongozi wa matawi na kuwahonga fedha nyingi sana ili siku ya kura za maoni wampitishe.
Mjumbe mmoja alisema kama chama cha mapinduzi kitafanya kosa kumrudisha tena kugombea basi wasahau kushinda jimbo hilo kwani litakwenda upinzani na rekodi zinaonyesha kuwa jimbo hilo huwa halitabiriki na upinzani watatumia udhaifu huo wa ccm kushinda jimbo hilo.